Unatakiwa kabla ya kudate unamsisitiza kuwa huna malengo naye na mpo kibiashara tu
Oya mkuu kwa gia hii unataka nipige nyeto mpaka parachute iuzwe 30k?
Hawa wapuuzi hawatakiwi kuijua next step yako.
Ishi humu mkuu.
Nina mwanangu mmoja hivi mwanzo nilikuwa simuelewi kabisa itikadi zake. But muda unavyozidi kwenda naanza kumuelewa kiundani zaidi.
Iko hivi jamaa ni famous sana hapa town,
Hakuna connection inayomshinda.
Sasa wakati wife aliamua kusepa nilibaki na sonona sana.
Kwanza nilikaa ndani tu yaani sitoki kwenda mahali popote miezi minne mfululizo.
Hapo siendi kazini wala mishe yoyote ile.
Ikifika usiku naenda kuchukua maziwa mtindi tu ndio yanapita kooni chakula sina hamu nacho kabisa.
Mwana akanicheki hewani
Oya Sonko mbona sikuoni na wakati sio kawaida? Na vipi kuhusu biashara X uliyoniambia nitafute tenda?
Maana tayari nina tenda tatu hoteli A, hoteli B na hoteli C wameniambia nipeleke sample
Inakuwaje sasa?
Ndio nikampa mchapo kamili kuwa shemela kasepa lakini sio hivyo tu kuna mambo kibao ya pesa keshaharibu sana.
Yaani kuna namna kaamua kujilipa mwenyewe kwa miaka kumi tuliyokaa pamoja.
Mwamba ananiuliza uko wapi?
Namjibu niko B.... huku
Ananiambia njoo ofisini.
Namwambia poa.
Baadae naibuka pale.
Tunabonga sana atleast naiona nafuu kidogo.
Mwamba ananiambia twende kiwanja fulani.
Tunaibuka,, tunabonyea sana pale mpaka ngoma tano hivi.
Kisha mwamba ananiaga kidogo,, Oya Sonko nakuja one time,, nampa CCM(dole gumba) pale, anasogea kaunta anaclear bill.
Mi namcheki tu hatua zake baada ya yeye kusepa natoka maeneo yale nakodi boda mpaka home.
Ile naingia kwa bed tu hivi mwamba ananivutia waya.
Napokea, Mwamba : Sonko uko wapi? Maana nimekuja na shemeji yako nikutambulishe.
Mimi: King nishang'oa muda hivi niko pentagon.
Mwamba anasikika ile kinyonge sana : Poa Sonko but shemej nae alikuwa kaambatana na mwenzie halafu yeye hana mtu, nikawa nimesema nae akawa ameelewa nilitaka uwepo muonane.
Nikamwambia sio kesi kesho nitakuwepo waambie waje.
Akajibu poa akakata waya.
Niliwaza yaani mtu nina machungu ya kuachwa halafu huyu ananiletea wale wale?
Si aniache nipumzike kwanza? Kumbe najiongopea sitakiwi kupumzika kabisa inatakiwa nibandike kitu kipya ili hii hali iishe.
Na King ndie anahakikisha hilo linatokea.
Kiaje sasa? Nakuja kuelewa kuwa jamaa anaweza kukusimamisha na mwanamke yeyote yule na akahakikisha kuwa huyo mwanamke unambeba huo uwezo ni wachache sana wanao.
We mwambie tu kuwa nataka wanawake wa kiwango fulani sasa mimi wanawake wa hali ya chini yaani ambao hawana kipato zaidi ya M15-20 kwa mwaka siwataki.
Ila baada ya kukutanishwa na wale wa kipato cha juu nako kuna kikwazo nakutana nacho.
Hawa wamechoka kuwa single wanataka mtu wa kuwaoa yaani hitaji lao ni ndoa hawataki zaidi ya hilo.
Maana kama ni mijengo, magari, kazi na biashara za pembeni wanazo
Changamoto kwangu mi sitaki ndoa na mtu hata kama najicomit kwa mwanamke ila ndoa sitaki.
Na jamaa yangu akinikutanisha na hao watu ananitambulisha mpaka naogopa mwenyewe.
Akigundua kuwa huyo mwanamke ni msomi labda ana masters yeye atamwambia kuwa huyu ni Bro wangu karudi juzi tu kutoka Malaysia anakofanyia biashara zake na ana Masters ya kitu fulani.
Anamtajia mambo lukuki yaani mpaka unaetambulishwa unaogopa lakini sasa kwasababu wanamjua kuwa yeye mwenyewe ni Don wanaamini mazima.
Sawa hata kama nina vipesa lakini sio kwa kiwango hicho anachonipamba nacho King.
Siku nikamuuliza Bro mbona unanisakafia sana kwa hawa viumbe?
Akajibu kuwa we nakukutanishaje na mwanamke anaendesha gari ya milioni 200 halafu nikuache kizembe hivyo lazima nikubrand maana akili yako kwenye miradi naijua ukiongea au kumshauri mtu lazima aweke mzigo kwenye mradi na ukiwa mpenzi wake ndiyo anakufanya kiongozi wake hapo tunafeli vipi?
Mpenzi wako akikubali kuweka milioni 200 kwenye mradi wowote return yake huoni kama itatusapoti kwenye kuboost biashara zetu huku ukizidi kugain trust pamoja na connection kubwa zaidi kutoka kwa wakubwa wengine?
Huyu King kanifanya niyatazame mahusiano katika angle tofauti yaani mafanikio badala ya kuanzisha mahusiano for the sake of kumridhisha Abdallah kipofu tu.
Kama una watu au mtu wa sampuli ya King kwenye circle yako jitahidi kuwekeza time yako kwao.
Hata kama itakubidi kuteketeza 1m kwaajili ya kuspend nae we teketeza tu maana ukipewa cheo cha ubosi usikikatae huwezi jua mwenzako kaona ability gan kwako
Japo unaweza ukawa unajichukulia poa.
Angalizo usipende sana kuongea,, hilo jukumu muachie yeye maana watu wanamuamini yeye.
Akiongea yeye tu inatosha wewe baki kuwa bosi tu na matajiri au wasomi wakubwa huwa hawaongei sana wewe vaa tu ule uhusika kikamilifu hutaamini mlango utakapofungukia..Yaani kiulaini tu mnashoot.
Muhusika anapata faida na ninyi mnakua kupitia alichowekeza mwenye mtaji.