Wazoefu wa mambo ya familia nipeni ushauri

Wazoefu wa mambo ya familia nipeni ushauri

Sanaa
Yaani napenda mwanaume anizidi Kila kitu Ili ani control kwenye Kila eneo!
Maana wanawake sisi bila hivyo tutakupand kichwani
Kumbeee akuzidi kila kitu au sio...wee sema akuzidi pesa tuu.
 
Huyu mwanamke tumekua kwenye mahusiano kwa zaidi ya mwaka. Katika kipindi hicho alikuwa anaishi kwao. Wakati tunaanza mahusiano alinieleza kuwa tayari ana mtoto wa kiume. Na kwasababu pia Mimi nilishapata Mtoto huko nyuma sikuona tatizo. Huyo mwanaye baba yake yupo na maisha yake mengine safi tu.

Baada ya kungoja sana mambo yake sawa, tukafikia kuamua kuishi pamoja angalau kwa kuwahusisha wazazi hasa upande wake. Binti ikabidi aje tuishinaye vkwangu. Hapo awali tulikubaliana kuwa huyo mwanaye atabaki kuishi kwa bibiyake na tutamuhudumia akiwa huko.Mimi mwanangu Yuko shuleni na akiwa likizo anakuja kusalimia na kurudi kwa mama, maana yeye ni wa kike.

Sasa baada ya miezi mitatu ya kuishi naye, huyu mwanamke alisubiri nikiwa safari akaenda kumleta huyo mwanaye aje aishi hapo. Pia hakuishia hapo akabeba na watoto wawili wa dada yake nao kaleta hapo na Sasa Kuna watoto watatu.

Nimesafiri tena na kurudi na bado nawakuta na hawana mpango wa kuondoka. Tayari anawaweja kwenye mipango na bajeti zetu kama wangu vile.

Binafsi napenda kuishi na Mtoto ambaye nakuwa huru naye. Yaani hata nikimuonya asichukulie kama namtesa. Kuna mambo yanafanyika nakaa kimya lakini nimegundua hiyo inanitesa Mimi.

Tafadhali nipe USHAURI wako. Hapo nifanyeje ili nipatie amani bila kuonekana Nina roho mbaya?
Fanya maamzi sasa hivi ili uwe na
amani baadae wewe ndo baba wa familia amua kama baba amua kama mwanaume
 
Back
Top Bottom