nizakale
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,035
- 2,938
Wewe kama umeshindwa imani kaa pembeni endelea kutambikia na kufanya matambiko tuache sisi na imani yetu. Kafie mbele huko..
Ndugu zetu walokole tafadhari Sana mtaniwia radhi.
Ukizunguka mikoa na Miji mbalimbali hapa Tanzania kuna mikutano ya Injili iliyoandaliwa na makanisa ya Kilokole na wahubiri ni wazungu kutoka nchi zenye Korona,tuwe makini hawa huenda Wana ajenda ya Siri.
Hawa mabwana nchi zao zimepiga marufuku raia wetu kwenda kwao kwamba tutawapelekea covid 19 na wakati huo huo wameiblakilisti nchi yetu kama nchi hatarishi sasa iweje wawaruhusu raia wao eti kuja kueneza Injili kwenye nchi hatarishi?
Msije shangaa wimbi la tatu likazuka ghafla na biashara ya chanjo ikafanyika.
Sijawahi wakubali hao wazungu wenu,huko kwao kuna mashoga kibao na wengine ni viongozi wao kwa nini wasiwahubirie hao? Huku Afrika kuna nyumbu sana hadi inatia hasira.