#MICHEZO Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino amezungumza na waandishi wa habari huko Qatar kuhusiana na malalamiko ya kutokuwepo kwa pombe viwanjani kwenye michuano ya Kombe la Dunia.
Infantino amesema kuwa,“Kama pombe ndilo suala kubwa tulilonalo kwa Kombe la Dunia basi nitajiuzulu mara moja na kwenda ufukweni kupumzika."
"Usipokunywa bia kwa masaa mawili matatu, bado unaweza kuishi, kwa sababu utaratibu huu pia upo hata kwenye nchi za Ulaya, ukienda Ufaransa, Ureno hata Uswisi sheria hizi zipo.Hapa imekuwa jambo kubwa sijui ni kwanini au ni kwa kuwa sababu ni nchi ya Kiislamu."
#WorldCupQatar #
Sent using
Jamii Forums mobile app