Wazungu wana akili na maarifa, Waafrika tuna vipaji na nguvu

Hauwezi kuwa na kipaji bila kuwa na akili.
Na bila kuwa na kipaji then akili yako haiwezi kuwa manifested.

Hivyo hao uliowataja wenye akili wote walikuwa na vipaji kwenye wanayofanya.
Na hao uliowataja wenye vipaji wote walikuwa na akili au akili yao iliwekezwa kwenye wanayofanya.

Wewe umeshawahi kujiuliza kwanini watoto wa matajiri wanaosoma international schools wanaonekana wana akili kuliko watoto wa masikini wanaoishi uswahilini na kusoma kayumba?

Conclusion ni hakuna binadamu asiye na akili au kipaji bali mazingira, malezi na tamaduni ndio zinaamua mtu awe na akili au kipaji cha aina gani.

Kwa mindset ya kuamini wewe huna akili na mzungu amekuzidi ni acid inayowatafuna africans wengi.
Btw wao ndio walipandikiza hii acid kwa kutumia myths za dini kipindi cha ukoloni.
ni kama wale africans wanaosema wale nusu waraabu nusu wazungu wanaoishi Israel sasa hivi wana akili kuliko wao.

Just Pathetic.
 
Unachukiza kujidharau mwenyewe na hilo unawarithisha watoto wako. Toka huko! Hutukanwi unaambiwa ukweli. Mindset zipi first class ipi? Kuna mind first class? Ndio ikoje? Jiamini. Acha kujidharau na kujiona second class citizen kwa kumuweka mzungu mbele. Watu wote wako sawa.
 
Kuna researcher mmoja anaitwa Margaret Mead, aliishi Samoa kwa miaka 10, alijifunza Mila na desturi. Conclusion ya research yake aligundua kuwa binadamu wote ni sawa. Tofauti zetu zinatokana na mazingira tunayokulia.
Nakubaliana na hili pia
Mwanangu wa miaka 9 leo anaenda shule akiwa amebeba madaftari 8, akifanikiwa kufika A level itabidi aendelee na masomo 3 tu, kwa nini system inamfubaza mtoto huyu kwa kumsomesha masomo ambayo hatakuja kuyatumia huko mbele? , Hivi mtoto huyu anaweza kuja kushindana na wenzake ambao wamespecialize toka wakiwa wadogo, ?
 
A level ndiyo mtoto anabaki na masomo matatu. Akili ya mtoto anapofikisha miaka 5 Ina uwezo wa kunasa na kuhifadhi information nyingi sana. Hata lugha ya ziada ni muhimu kumfundisha mtoto kabla hajafika miaka nane hapa anaweza kumudu pronunciations.

Kama mtoto anaanza darasa la kwanza na miaka mitano-saba uwezo wa kumudu masomo anao lakini ni muhimu kama mzazi kugundua kipaji chake mapema ba kumsaidia kupata combination ya uwezo wake.
 
Huwa najiuliza sana na hili najua watu wengi hawalijui.

Akili au wingi wa akili au maarifa haupimwi kwa vigezo vya uvumbuzi au mfano wake,ndiyo maana unakuta katika vumbuzi kuna mengi ya uongo.

Siku ukijua maana ya AKILI,na ukatafakari na ukawa muadilifu unaweza kutuomba radhi hadharani.

Unavyo ongelea wewe ni vipawa na Mola wetu humpa amtakaye katika wanadamu.

Mathalani tukimpima mtu kama Einwtein ni mambo hata matano ambayo aliwahi kuyasema na ni kweli tupu. Sasa utakuta uelewa tu wa tamko Akili watu wengi hawajui. Hili tatizo kubwa sana.

Mathalani mimi naweza toka kifua Mbele nikasema nina AKILI kunzidi Albert Einstein na huwezi kunipinga kwa hoja. Huu ndito ukweli wenyewe.

Shukrani.
 
Wewe jambo gani alilofanya Newton lina ukweli na umeliona na ukalihakiki kuwa ni kweli au Einstein ?

Kuna vitu vingine vinahitaji watu wahoji. Ukifatilia katika ulimwengu wa nadharia za kisayansi kila uchwao wanapingana,mara leo huyu anasema hili mara kesho yule anasema hiv,na wote wanakuwa wamekosea.
 

Labda sijui maana ya neno 'fala ' kwamba ni kivumishi au kiunganishi , ila nina uhakika huwezi mwambia mkweo au mzazi wako let alone yoyote unayemuheshimu,

Si kuwa najidharau ila , nimefanyia kazi sana mapungufu yetu sisi blacks , sipo kwenye level za kuamini kuwa matatizo yangu yanasababishwa na mtu mwingine , bali naamini changamoto zangu natakiwa kuzitambua na kuzitatua mwenyewe, huoni albino na walemavu wengine kwenye koo za kimasai, si kwamba kweli hawapo bali wanauwawa ili kuficha udhaifu huo, hawatatui tatizo bali wanaficha tatizo.
 
Max amevumbua hii platform angefanya makubwa kiasi gani kama yeye na Mark wangekuwa kwenye mazingira sawa
Huoni kuna utofauti mpaka hapo? Hii platform unayosemea huduma na muundo umetoka wap?😁😁 Yan ww jamaa bana. Kila kitu matengeneza mzungu, haya ww mwenye akili umetengeneza nini?
 
Mzungu ni nani na unahakikishaje huyu ni mzungu?
 
Yanayoripotiwa toka Afrika ni uongo kwa hiyo?
 
Mm nakataa kama ni mazingira. Mbona leo SA haifanani na Tanzania? Wote si tuko Afrika? Kwanini wao wameendelea kuliko sisi? Aya angalia Nigeria na SA ni sawa? Nigeria ina uchumi mkubwa sana pengine kulikl SA ila SA imepangwa vizuri kuliko Nigeria. Mapaka hapo unaamini tuko sawa na wazungu?
 
Hata ukichunguza
-Islamic golden Age kipindi ambacho nchi za kiarabu na baadhi za North na west Africa Vumbuzi nyingi zilifanyika maeneo hayo kuliko sehemu nyengine duniani.

-kabla ya Hapo kulikuwa na Empire 4 kubwa Aksum (Ethiopia), China, Persia (Iran) na Roma. Vumbuzi nyingi zilifanyika kwenye hizi nchi kuliko mahala popote duniani.

Vumbuzi zinaenda sambamba na hela, jamii inayokuzunguka, elimu etc na hazina mahusiano yoyote na Rangi, kabila, uzuri, etc.
 
Mwanangu wa miaka 9 leo anaenda shule akiwa amebeba madaftari 8, akifanikiwa kufika A level itabidi aendelee na masomo 3 tu, kwa nini system inamfubaza mtoto huyu kwa kumsomesha masomo ambayo hatakuja kuyatumia huko mbele
Shida hapo ni nani sasa? Najua utasema ni system,kama ni system inaongoza na nani? Kwanini huko uzunguni hakuna changamoto za kiboya kama hizi?
 
Ningekuwa na uwezo mwanangu nilioendelea a specialize kutoka darasa la kwanza ,
 
Kidoogo hii comment imekuja na hoja sahihi. Mkuu hapa nipo na ww
 
Ningekuwa na uwezo mwanangu nilioendelea a specialize kutoka darasa la kwanza ,
Hii wanafanya China, kuna sports Academy. Wanachukua watoto wa miaka mitano wanawafundisha michezo na mazoezi. Watoto hawa wakifika miaka 14 wanakua kwenye viwango vya kimataifa.

Kwenye mashindano kama Olympic wanaondoka na medani za dhahabu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…