Labda sijui maana ya neno 'fala ' kwamba ni kivumishi au kiunganishi , ila nina uhakika huwezi mwambia mkweo au mzazi wako let alone yoyote unayemuheshimu,
Si kuwa najidharau ila , nimefanyia kazi sana mapungufu yetu sisi blacks , sipo kwenye level za kuamini kuwa matatizo yangu yanasababishwa na mtu mwingine , bali naamini changamoto zangu natakiwa kuzitambua na kuzitatua mwenyewe, huoni albino na walemavu wengine kwenye koo za kimasai, si kwamba kweli hawapo bali wanauwawa ili kuficha udhaifu huo, hawatatui tatizo bali wanaficha tatizo.
Unisamehe kama lugha niliyotumia haikufaa.
Lakini haya masuala ni mitazamo na inakuwa changamoto zaidi ikiwa imani itapewa nafasi kubwa kuliko uhalisia.
Hoja iliyoko hapa ni kuwa sio kweli kuwa wazungu au watu wengine wana akili zaidi kuliko mtu mweusi. Hii ndio hoja hapa.
Lakini kinachofanya watu waanini Vinginevyo ni kuwa jambo au kitu chochote kizuri kinahusianishwa na watu weupe hasa wazungu. Katika hili ndio inakuja hoja kuwa, kihistoria, upo ushahidi kuwa mtu mweusi alidhibitiwa mapema kabisa kwa kuanza na ku-manipulate mindset yake. Mindset ikawa reprogrammed kuamini kuwa kuanzia kwenye rangi yake nyeusi inareflect kitu au mambo mabaya, dhaifu, misfortune n.k. Mtu anaweza kusema kwanini isingekuwa kinyume chake ili mwafrika aitawale dunia na kuwa superior? Hili swali linakosa mantiki na haliondoi ukweli huo kuwa kwa makusudi na malengo ya muda mrefu, wazungu waliweka mikakati ya kutawala juu ya mtu mweusi.
Na wamefanya hivyo kwa njia nyingi ila kubwa ni kupitia elimu waliyoitoa, kusambaza lugha zao na kuaminisha waafrika ukijua French au English au Portuguese unakuwa bora kuliko weuso wenzako wasiojua. Hivyo kwa sehemu kubwa elimu na lugha ya kwa nchi nyingi za Africa zinafuata alichopanga mzungu. Sio vya kwetu. Ndio sababu hata wewe huenda ulisoma kuwa kuna mzungu aligundua ziwa victoria. Na ukaamini. Hebu jiulize hivi ziwa unaligunduaje? Au mlima Kilimanjaro unaugunduaje?
Fikiria tu hata haya maneno yao na maana zake; “whitelist” na “blacklist” vitu vibaya vimepewa rangi gani?
maana ya kusema hivyo ni kuwa hata kama watu weusi wavumbuzi walikuwepo au wapo, ni kama walishachelewa maana anayedhibiti taarifa wewe ujue nini na usijue nini ndiye anapanga yote unayoyaamini wewe leo. Hata Biblia kaandika yeye na Quran kaandika yeye (kwa maana vyote hivi asili yake sio Afrika). Wewe cha kwako ni kipi? Kama hakipo utakwepa vipi kutawaliwa na kupewa fursa kadri wanavyotaka wao. Wakikuaminisha huna kitu sababu huna akili kama sisi utakataa vipi wakati vyote unavyotumia wanadhibiti wao.
Hata hivyo, watu weusi waligeukia sanaa na michezo ili waishi baada ya kutopewa fursa sawa kwenye mambo mengi hata huko ulaya na marekani. Ndio sababu wako zaidi kwenye maeneo hayo ni kwa sababu ya ubaguzi wakaanza kufanya vitu visivyohitaji elimu rasmi kama michezo na muziki. Huo ubaguzi kama huko Marekani usome au usikie tu, ni kitu kimesumbua na kuua weusi wengi. Na bado kipo hata jana tu ilikuwa maadhimisho ya mwaka mmoja ya kifo cha George Floyd Na kwa mwaka jana pekee Marekani kumekuwa na zaidi ya vifo 40,000 vjnavyohusisha silaha, lakini kwa mtu mweusi zaidi.
Unaweza kuamini Vinginevyo lakini ukweli ni kuwa watu wote wako sawa ila mazingira, nyenzo na tamaduni ndio huathiri ukuaji na uwezo wa mtu. Lakini vyote huanza na mindset.