Wazungu wana akili na maarifa, Waafrika tuna vipaji na nguvu

Mkuu miaka Mia kadhaa iliopita Mali ilikuwa nzuri, kubwa, ina elimu, ipo civilised kuliko ulaya ambayo wakati huo wanaua wanasayansi wakiwaita wachawi.



Mfano wa Timbuktu kama miaka 700 iliopita.
 
Mzyngu ni nani na unahakikishaje huyu ni mzungu?
Angalia gunduzi nyingi na tafiti nyingi wanaofanya ndio wazungu. Hata vitabu vilivyokufanya usiamini uwepo wa Mungu kaandika mzungu
 
Waafirka kweli ni mapopoma kujifariji tuu et onhhhoh tulikua tunaongoza kwenye kila kitu ila wazungu wakaja wakatudidimiza...🤣🤣🤣🤣 Waulize hao ma pro Africa kwenye mashindano anaepewa ushindi ni yule alianza kutangulia au aliyemaliza akiwa mshindi???
 
Wanajifariji tu lakini ukweli unaonekana wazi
 
Unisamehe kama lugha niliyotumia haikufaa.
Lakini haya masuala ni mitazamo na inakuwa changamoto zaidi ikiwa imani itapewa nafasi kubwa kuliko uhalisia.
Hoja iliyoko hapa ni kuwa sio kweli kuwa wazungu au watu wengine wana akili zaidi kuliko mtu mweusi. Hii ndio hoja hapa.
Lakini kinachofanya watu waanini Vinginevyo ni kuwa jambo au kitu chochote kizuri kinahusianishwa na watu weupe hasa wazungu. Katika hili ndio inakuja hoja kuwa, kihistoria, upo ushahidi kuwa mtu mweusi alidhibitiwa mapema kabisa kwa kuanza na ku-manipulate mindset yake. Mindset ikawa reprogrammed kuamini kuwa kuanzia kwenye rangi yake nyeusi inareflect kitu au mambo mabaya, dhaifu, misfortune n.k. Mtu anaweza kusema kwanini isingekuwa kinyume chake ili mwafrika aitawale dunia na kuwa superior? Hili swali linakosa mantiki na haliondoi ukweli huo kuwa kwa makusudi na malengo ya muda mrefu, wazungu waliweka mikakati ya kutawala juu ya mtu mweusi.

Na wamefanya hivyo kwa njia nyingi ila kubwa ni kupitia elimu waliyoitoa, kusambaza lugha zao na kuaminisha waafrika ukijua French au English au Portuguese unakuwa bora kuliko weuso wenzako wasiojua. Hivyo kwa sehemu kubwa elimu na lugha ya kwa nchi nyingi za Africa zinafuata alichopanga mzungu. Sio vya kwetu. Ndio sababu hata wewe huenda ulisoma kuwa kuna mzungu aligundua ziwa victoria. Na ukaamini. Hebu jiulize hivi ziwa unaligunduaje? Au mlima Kilimanjaro unaugunduaje?
Fikiria tu hata haya maneno yao na maana zake; “whitelist” na “blacklist” vitu vibaya vimepewa rangi gani?

maana ya kusema hivyo ni kuwa hata kama watu weusi wavumbuzi walikuwepo au wapo, ni kama walishachelewa maana anayedhibiti taarifa wewe ujue nini na usijue nini ndiye anapanga yote unayoyaamini wewe leo. Hata Biblia kaandika yeye na Quran kaandika yeye (kwa maana vyote hivi asili yake sio Afrika). Wewe cha kwako ni kipi? Kama hakipo utakwepa vipi kutawaliwa na kupewa fursa kadri wanavyotaka wao. Wakikuaminisha huna kitu sababu huna akili kama sisi utakataa vipi wakati vyote unavyotumia wanadhibiti wao.

Hata hivyo, watu weusi waligeukia sanaa na michezo ili waishi baada ya kutopewa fursa sawa kwenye mambo mengi hata huko ulaya na marekani. Ndio sababu wako zaidi kwenye maeneo hayo ni kwa sababu ya ubaguzi wakaanza kufanya vitu visivyohitaji elimu rasmi kama michezo na muziki. Huo ubaguzi kama huko Marekani usome au usikie tu, ni kitu kimesumbua na kuua weusi wengi. Na bado kipo hata jana tu ilikuwa maadhimisho ya mwaka mmoja ya kifo cha George Floyd Na kwa mwaka jana pekee Marekani kumekuwa na zaidi ya vifo 40,000 vjnavyohusisha silaha, lakini kwa mtu mweusi zaidi.
Unaweza kuamini Vinginevyo lakini ukweli ni kuwa watu wote wako sawa ila mazingira, nyenzo na tamaduni ndio huathiri ukuaji na uwezo wa mtu. Lakini vyote huanza na mindset.
 
👏👏👏👏kula kwanza 👊mkuu nimedaka iyo pointi. Huenda hii ikawa kweli kabisa. Cha kushangaza hata sheria za dunia katunga mzungu na ukitunga zako zinaonekana za kimila na hazifai😁😁

Kwenye gunduzi hata mm nashangaa unagunduaje ziwa lililoumbwa na Mungu? Kabla ya ugunduzi huo halikuepo?. Ni muda sasa umefika wa kubadilisha majina ya ya vilivyogunduliwa na wazungu vipewe majina ya asili ya eneo hilo
 
 
Angalia gunduzi nyingi na tafiti nyingi wanaofanya ndio wazungu. Hata vitabu vilivyokufanya usiamini uwepo wa Mungu kaandika mzungu
Hujajibu swali langu.

Mzungu ni nani na unahakikishaje huyu mzungu?
 
Hongeren sana mkiona mmefika hatua ya kujibizana wapi tunakosea na kwa nn hii pia ni hatua tunapiga tuendelee kufundishan na kupeana moyo

Muelimishe mtu kwa ustaraabu inasaidia zaid mtu kujifunza na kuuliza maswal tena na tena ule ujuaj tuache tuelimishane taratibu taratibu

Tumechelewa ila tutafika tuongeze nguvu tu
 
Kijana alikuja na hadithi aliyosimuliwa na babu yake akizania kwamba ina uhalisia kumbe porojo.
 
Soka PELE.
music MICHAEL JACKSON n.k.
tennis SELENA WILLS.
Golf ROGER FEDERA.
Boxing MOHAMMED ALI & MIKE TYSON.


Uwezo tunao tatizo uchawi tunalogana sana
 
Zamani waafrika walichukuliwa kwenda utumwani ulaya bila kupenda,leo waafrika wanapanga foleni embassy kwenda kuwa watumwa kwa hiari.
Laiti Ingekuwa ni bure kwenda ulaya si dhani kama kuna kijana angebakia afrika.
 
wazungu ni wezi wa maarifa
ni kama saiv kila binadamu ananunua land na kusema cha kwake kumbe Mali ni za Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…