kakaangu mimi sizungumzii na wala siko hapa kuzungumzia dini.
Mimi siko hapa kuwakilisha ukirsto wala siko hapa kuueneza uislamu achilia mbali ubudha.
Niko hapa kukumbusha tu, Mungu yupo.. na miungu ipo... Tubu na urejee kwa Mungu wako achana na miungu kaka, acha kiburi, acha wizi, acha ulevi, acha unafiki, acha uchawi na ulozi, acha dharau kakaangu, Mungu haletewi kibesi chako kaka.. acha kabisa tena TUBU leo leo kakaangu kesho ni majaaliwa ya Muumbaji tu, mimi Namuomba Mungu akufanyie wepesi utubu kaka.
Duniani hapa palikua na miamba, duniani hapa palikua na wanaume, duniani hapa palikua na majabali, hapa duniani palikua na manguli, kuna watu walikuwa magwiji hapa duniani kaka lakini leo wako wapi?
Musa alikua mwanaume anaepiga story na Mungu moja kwa moja, sembuse mimi na wewe ambao hata shetani hawezi kukaa meza moja na sisi kwa sababu hatumfikii kwa uwezo wa kuutawala ulimwengu? Jinyenyekeze chini ya mkono wa MUNGU, tubu leo ndugu.
Mimi sio msafi, wewe sio mtakatifu... Sote tumetenda dhambi, ila mimi nakukumbusha tu (Kujisahau kupo) TUTUBU TUNGALI WAZIMA NA NGUVU ZETU HIZI TULIZO NAZO.
Mungu yupo hapo ulipo, yupo msikitini, yupo kwenye sinagogi yupo kila mahali.... NI JUKUMU LAKO KUMTAFUTA, NAYE ATAONEKANA KWAKO.
Narudia, acha kiburi TUBU.