Weka siasa pembeni, tafakari "credibility" ya Mamlaka za Serikali katika sakata la CHADEMA

Kila kukicha chuki dhidi ya siasa inaongezeka. Kumbe hata wizi, dhulma, uongo, hila na vitu kama hivi katika siasa ni ruksa. Aisee mhh!
 
Lazima tuseme ukweli. Ikifikia hapa uzalendo hasa ni kusema ukweli. Huyu Magufuli ataiacha Tanzania pabaya, kama alivyoiacha Trump Marekani. Haiwezekani mtu mwenye dhamana ya kuwa mfano wa uadilifu, ukweli, upendo, huruma, usawa…..akawa mtu ovyo namna hii. Hajali sheria, utaratibu, ukweli, UTANZANIA wala mshikamano wa taifa.
Ingekuwa nchi nyingine yeyote iliyostaarabika aidha angechukuliwa hatua na kulazimishwa ajiuzulu au anguezuliwa na bunge moja kwa moja. Haijatokea TANZANIA kuwa namna hii! Pamoja na kuwa miaka yote iliyopita hatujaongozwa kwa uadilifu hivyoooo, lakini huyu hana mfano wake.
Swali hasa la kuuliza: yote haya anayafanya kwa kutaka nini hasa? Kuendelea kuwa madarakani? Kujenga nchi (kama anavyodai) au kuleta vita nchini?
Ni mtu mzalendo tu atakayesema ukweli na kukemea yanayoendelea bila ya kuogopa. Wako wapi marais, Mawaziri wakuu n. waliopita? Wanagopa?
 
Dunia lzm itegemeane, huwezi endelea kwa kuwa kisiwa huwezi endelea bila kushirikiana na mabeberu, maendeleo ni sawa na mchezo wa draft lzm uliwe ili ule USA inaliwa na china, afrika nk vivyo hivyo nayo inakula china inakula afrika.Siasa zetu ni za kumwaga damu lzm watu watolewe kafara,lzm watu waibe kura, Tume, vyombo vya dola usaidia chama tawala ushindi, huwezi linganisha na za wenzetu waliostaarabika.
 

Lengo kuu ni kuvuruga
 
Wee naona uko Ulaya lakini hujijui. Yaani wataka ubariki yanayoendelea Tanzania kwa kudai kama hayo yanatokea Ulaya, kwa vile' siasa ni mchezo hatari'? Usijekuwa uko huko kubeba maboksi tu!
 
Watu wengi hapa wanajibu, wanaandika, wakati hawajui chochote na wala hawana elimu ya kuwafanya waandike waandikayo….yaani 80%. HEBU NIWASAIDIE, ili ukibishana ujue haya:
Serkali ni 'unified entity' yaani ni ' Asasi moja' Kitu anachokifanya Mkuu wa Polisi, wa Bunge, Waziri...….anaweza moja kwa moja kulaumiwa rais…..hasa kama rais huyo hakuchukuwa hatua.
Hili la sasa, hata kama limefanywa na spika tu.….inachukuliwa moja kwa moja kuwa amefanya hivyo kwa kutekeleza 'mapenzi' ya kiongozi mkuu. Aidha kwa kauli au kwa kunyamaza tu.
Ndiyo maana Mawaziri wamestaafu, kwa sababu ya kitu kilichofanywa na ofisa tu (rais Mwinyi kwa mfano). Hebu someni historia ya Bolivia muone nchi za wenzetu zinazofuata sheria, zinaongozwa vipi. Evo Morales alitakiwa na mkuu wa jeshi aachie madaraka, baada ya uchaguzi uliohukumiwa na jopo la wa ukaguzi kuona kuwa haukutimiza masharti ya uhuru na haki! Na akawajibika.
Rais wa Peru, Manuel Merino, alijiuzulu siku moja tu baada ya wapinzani wawili kuuawa na polisi! Rais wa kabla yake, Martin Vizcarra, aliondolewa madarakani na bunge baada ya kukutwa amechukua rushwa!
Nchi kama hizo zinatia moyo hata kuwekeza fedha zako! Unajua wazi ukiwekeza, ukikosewa, utakwenda kwenye sheria na utapata haki yako.
Hapa kwetu ni maneno tu: ' Twataka wawekezaji!' Nani mwekezaji serious wa mabilioni atakuja? Haya mambo yanaendana, na kama hatutasafisha mfumo wetu wa siasa, sisi wananchi tukasimama wima kutaka kuongozwa kwa uadilifu, ukweli na haki…..wallahi hatutaendelea! Tutajengewa vituo kumi vya mabasi tuambiwe hayo ndiyo maendeleo! Wakati maendeleo ya kweli kabisa ni maendeleo ya mtu, kujiona huru katika nchi yake, hawezi kuonewa na mtu kwa vile tu amevaa magwanda, au ana cheo, na anahisi Amani yeye na watoto wake. Hayo yakitimia, pamoja na kutimia matakwa ya kawaida (basic needs) HAYO NDIYO MAENDELEO.
Tumeishi miaka mingi chini ya Julius Nyerere, bile ya umeme wala maji, lakini tulikuwa na furaha kwa wastani, kwa nini? Kwa sababu tulikuwa na Amani, tuna uhakika wa kiongozi aliyeko anatuonea huruma, anataka tuwe na Maisha mazuri, na kwa wastani alikuwa anasimamia kusiwe na uonevu wowote. Tanzania kweli ilikuwa KISIWA CHA AMANI, pamoja na umaskini. Hebu fananisha!
 
Hapana. Msifikiri kila mtu mtaweza kumuimbisha wimbo wa kumsifu Magufuli. Kwangu mimi ni rais mwenye maono finyu kuwahi kutokea Tanzania. Alipochukuwa madaraka hata mimi nilidhani tumepata rais msomi, asiyependa ku-apply siasa kila sehemu, mwenye vision na ataendesha nchi kisomi. Matokeo yamekuwa ni mengine. Badala yake tumepata rais anayeogolea kwenye cheap politics, anaye deal na petty issues na asiye na clue nchi inaendeshwaye. Hebu kweli tujiulize hizi sarakasi zooote anazozifanya kwenye vyama vya upinzani zina lengo gani? Mbona mimi sioni kama upinzani ulikuwa kikwazo kwake kwenye kuendesha nchi? Kwa nini anatumia nguvu kubwa kutengeneza upinzani anaotaka yeye? Si bora angeamua abaki na wabunge wa CCM tu kama hataki upinzani? Ukiona mtu anajitungia mtihani wa kufanya yeye mwenyewe basi ujue huyo mtu ana walakini mkubwa sana. Athari atakazoacha baada ya urais wake zitakuwa kubwa sana.
 
Acha kuropoka ww, tuambie Nusrat aliachiwaje
 
Nikiongoza, kibaya Zaidi ni kuleta ombwe la woga na vitisho. Hakuna nchi inayoendelea kwa wananchi wake kuwa woga. Wananchi wenye uhuru, upana wa fikra kwa kukumbtia experinces za watu, mataifa mengine…..hao ndio wanaosonga mbele. Nchi hizi: Japan, Singapore, Ujerumani na hata Uingereza zimeendelea kwa recipe hiyo. Hata baada ya kupigwa na kuumizwa vibaya, Japan haikusema achan na 'mabeberu' bali ilikumbatia ile mifumo iliyowafanya waweze kuipiga nchi yao!
 
Hivi chadema wakiwekewa ruzuku kutokana na wabunge waliowakataa watazikataa
 
This is a one man's show.
 
Tusubiri Ijumaa Mdee na GENGE lake wavuliwe uanachama,wabakizwe na ubunge kwa mbeleko ya Ndugai.

Kati ya Wanasiasa ambao sikutegemea hata siku moja wangekuja kufanya mambo ya hivyo na kujipaka kinyesi na kudhalilisha utu wake Halima Mdee sikuwahi kumfikiria.
 
Tatizo lipo kwa yule mhutu mpenda misifa
 
Hao wabunge wa viti maalum wote wafutwe uwanachama kabla hata ya kikao hasa halima mdee afutwe Sasa ivi itakuwa poa sana
 
Umeongea vema sana mkuu. Imagine yule aliyekuwa jela alitolewaje wakati majuzi kesi imesogwezwa mbele? Alitolewaje huko au mimi nimepitwa?
 
Viongozi wa CHADEMA wameshatoa kauli nyingi za uongo. Hawaaminiki. Usiache shughuli zako sababu ya kuipigania Chadema, utajuta...
Acha kukwepesha mada iliyoko mezani, kama Mnyika ni muongo si uweke hapa hiyo barua iliyoandikwa kwenda NEC?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…