Mkuu dogo ana nyota sana ya kupendwa na wanajeshi.
Na mpaka demu aliyemzalisha alikuwa ndo anaanza ajira ni mwanajeshi ila dogo amekulia kwenye garage maisha yake.
Ishu ilikuwa ni mwanamke si kwamba dogo alikuwa na fujo au laaah ni kama vile askari ajue unaishi na demu wake akutafutie sababu akupige akuumize akusweke ndani.
Huyo demu alikuwa ni demu wa club sana na mwanachuo hivyo akawa yupo na dogo na mshkaji aliyenipa taarifa usiku huo.baada ya kuingia ndio akaona poti akaanza kumtafutia visa, dogo kapigwa akaita wenzake wakaenda kumsweka ndani.
Mkuu kuna mikoa haya mambo ya kwenda kutoana vituoni kwa ubabe yapo na yanafanywa na askari wa chini.
Jamaa aliyeenda kumtoa baba yake ni mkuu wa kambi ya jeshi mojawapo katika huo mkoa.
Hata kuona kambi Fulani na kambi Fulani wana ugomvi bado kuna mikoa haya mambo yapo.
Kwenye mada,kuna kasomo kazuri. Ila,unataka kuharibu.
-Labda nisiingie kiundani zaidi,mambo yao hayanihusu, ila hawa jama hawanaga mafundi kwenye kambi zao? Kiasi cha kumzowesha raia kwenda kutengeneza magari! Navyojua mimi kama ni gari la jeshi, likiharibika njiani,bila kujali umbali,breakdown ya jeshi italifata,kama waliokuwemo hawana element ya ufundi au wao wasipoamua kumtumia fundi karibu,na pale wanapoona shida si kubwa.
-Si kwamba wanawake wanajeshi hawaolewi na raia. Kugegedwa sawa,inawezekana sana tu. Kwa hiyo,dogo kamzalisha tu huyo demu mjeda na akamuacha? Au walioana af akawa anafanya ujinga wake!
Wape staha yao, ila sidhani kama kuna mwanajeshi mwanamke anaweza kuzalishwa hivi hivi na akaachwa aendelee na kazi. Kama nfo hivo inawezekana,nidhamu kwao ni nini? Maana hata hilo ni moja wapo wa mambo ambayo ni mwiko kwa mwanajeshi mwanamke kutokujiheshimu.
Japo na kwa mapolisi sijui,ila haitakiwi.
Uongo punguza. Mpaka mtu anakuwa mkuu wa kambi, cheo chake si cha kuchukulia poa ujue? Hivyo, huyu mtu hata kama amestaafu yupo uraiani, bado anaongozwa kijeshi, huijiwa na Military Polisi(MP), polisi itamlipoti tu jeshini, watakuja wachukue mtu wao,lakini kuwekwa ndani kituo cha polisi!? Halipo na halitatokea.
Hiyo mikoa unayosema kambi furani na kambi furani wana ugomvi, kama Somalia sawa. Kwenyebkambi za mahalamia nakubali.
Ila jeshi la nchi,eti kambi zina ugomvi? Wa nini labda?
Weeee, kambi za jeshi si Simba na Yanga ndugu yangu.