Weka urafiki na wanajeshi (bakabaka) hutojutia

Weka urafiki na wanajeshi (bakabaka) hutojutia

Haya ni mawazo ya watu maskini. Ukiwa na mawazo ya kimaskini daima utajibebisha kwa wanaume wenzako.

Tafuta hela, ukiwa nazo hutakuwa na haja ya kujibebisha Kwa mtu yeyote Lisa sijui ye ni nani.
Huo ndiyo UKWELI, maana hadhi yako ndiyo ULINZI wako ndiyo maisha yako.

Ukiwa na fedha hadhi yako itakuwa ya juu, mahusiano yako yatakuwa na watu wa hadhi ya juu wawe WANAJESHI, POLISI, UHAMIAJI ,MANISPAA NK
Hutakuwa mtu wa kuanza kuhesabu huyu rafiki !! Huyu simpendi ! Malalamiko chungu tele KUMBE tatizo ni MAOKOTO NEHIIII
 
sawa tunashukuru kwa mchango wako.

Tena sio kwa nguvu tu na vitisho juu.na dogo anaondoka

Nadhani kuna mikoa bado ujafika umekosa exposure.
Sio vitisho tuu, Kuna kituo kiliwahi kuchomwa na hao jamaa...Walienda pale na gwanda ila juu wamevalia fulana tu ili wasitambulike number zao...Walitembeza kichapo kwa poti wote kwenye kile kituo wakarudi kambini kama sio wao, Kesi ilifika kambini ila hakuna alietambulika.

Kisa ilikua demu wa mjeshi alinyanyaswa na polisi kwenye hicho kituo.
 
Ndiyo nimejifunza kuwa licha ya utandawazi na elimu kuwa bure bado kuna watu ni wajinga hawajui pindi wanapoonewa na polisi wachukue hatua gani wao wanaamini kuwa na urafiki na askari wa jwtz ndo salama yao
Nani kaonewa?

Nikikuambia unakosa utulivu unabisha.

Pole Rudi kasome tena mdogo wangu
 
Nani kaonewa?

Nikikuambia unakosa utulivu unabisha.

Pole Rudi kasome tena mdogo wangu
Kumbe hata ulichoandika hukijui? Njia pekee itakayo kusaidia ni kutafuta elimu juu ya haki zako ili unapoonewa na polisi ujue hatua za kuchukua, na siyo kuwa na urafiki wa wanajeshi hao hawana mamlaka ya kukutoa kwenye mikono ya polisi
 
Hata hao ndio wale wale tuu wanakuaga na ubabe wa kijinga kwa kifupi askari wote wa uswahilini ni kama walizaliwa na mzazi mmoja, unasifia hao jamaa kwa sababu walikusaidia lakini kwa wale walio pigwa matukio na hao mabaka mabaka ndio wanajua ushetani wao vizuri

hiyo mada kaipeleke kawe kwa wale walio onja joto la jiwe baada ya yule kiongozi wa mabaka mabaka kujichanganya kwa dereva bajaji alafu utatuletea majibu
 
Sio vitisho tuu, Kuna kituo kiliwahi kuchomwa na hao jamaa...Walienda pale na gwanda ila juu wamevalia fulana tu ili wasitambulike number zao...Walitembeza kichapo kwa poti wote kwenye kile kituo wakarudi kambini kama sio wao, Kesi ilifika kambini ila hakuna alietambulika.

Kisa ilikua demu wa mjeshi alinyanyaswa na polisi kwenye hicho kituo.
Hawa watu hakuna wanalojua mkuu.

Kwamba Sheria haiwezekani Hilo?

Nilishaingia kituo cha polisi mwaka Fulani kipindi Cha mwaka mpya zoa zoa ile ikanikuta.

Kufika pale tukaambiwa kaeni chini usiku huo, badala ya muda akaingia jamaa kachafuka kwenye mabega na wawili wakiwa nyuma yake.

Nikamuona mkuu wa kituo kaja jamaa akasema yupo wapi huyo, mkuu akatoa amri akatolewe.

Jamaa katolewa kituoni anaburuzwa analia kama mtoto. Wale mabakabaka wakambeba wakaondoka naye.

Wengi hawajakutana na hizo hadha kule ni pabaya sana, na utemi bado upo.
 
Ahahaha dogo hizi stori peleke fesibuku tena hata kule wanaweza wakaikataa hii chai
Kwa kifupi hamna mtu anaweza kumtoa mtuhumiwa magereza au kituo cha polisi akiwa detained bila utaratibu
Pale ubabe hauna nafasi mzee hata waziri wa ulinzi mwenyewe hawezi kutoa amri ya mtu kuachiwa kibabe eti kisa ni rafiki yake
Unaishi nchi gani ?
 
Kumbe hata ulichoandika hukijui? Njia pekee itakayo kusaidia ni kutafuta elimu juu ya haki zako ili unapoonewa na polisi ujue hatua za kuchukua, na siyo kuwa na urafiki wa wanajeshi hao hawana mamlaka ya kukutoa kwenye mikono ya polisi
Hakuna haki kituo cha polisi.

Ndio maana nakuambia wewe bado sana.

Kutoka polisi ni pesa lakini kuna Sheria hiyo kwamba kutoka polisi ni pesa?

Acha ujinga ndugu, polisi ni uwe na pesa au utumie mtu mwenye nguvu zaidi yako.

Polisi anasema embu mshuhurikieni huyu na wale watukutu wa mule ndani wanampga mpaka anavimba macho.

Acha ujinga. Hakuna haki polisi huo ni ukweli
 
Unavyoandika tu unaonekana kichwani ni mweupe ngoja nikuache kwa akili hizi lazima utaamini ukijenga urafiki na wanajeshi wanaweza kukutoa kwenye mikono ya polisi na siyo kutafuta elimu ujue haki zako za msingi ili uweze kujisimamia
 
Unaishi nchi gani ?
Huyo bado mtoto sana.

Mkuu wengine sisi tushapitia hizo sehemu tushajifunza kwa kuona yaliyomo humo ndani.

Ndani ya vituo ni matusi, udharirishaji na dharau.

Hajui hata kulala mchongoma ni nini.

Bado dogo huyo
 
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano?

KUna ndugu yangu alisema kataa kabisa urafiki na askari polisi. Naunga mkono hoja.

Mimi nasisititiza kama kichwa cha habari kinavyosema, tengeneza urafiki na askari wa mabakabaka, hawa watu wapo very humble, wana upendo na heshima katika jamii, japo wachache wanawaharibia.

Kuna ndugu yangu alikuwa ni fundi wa gereji za magari mkoa Fulani sio dar. Alikuwa anawatengenezea sana wanajeshi magari yao, ikafika kipindi wasipomkuta dogo wanamtafuta anaenda mpaka kambini kuchukua magari na anawatengenezea kwa uaminifu.

Siku moja katika viwanja vyake dogo vya starehe kuna polisi akamletea ubabe akampiga akaita wenzake wakaenda kumsweka ndani ishu ni ya wanawake.

Mimi napewa taarifa usiku saa5 na mtu aliyekuwepo mule ndani club dogo wamempga na wamemchukua, usiku huo huo nikavuta waya kwa jamaa mmoja mwanajeshi alikuwa anamkubali sana dogo, baba yake alikuwa mkubwa wa kambi katika huo mkoa,

Akaniuliza ilikuwaje nikamwambia kama nilivyoambiwa akaniambia ok tunakuja hapo, usiku saa5 inakimbilia saa6 wakaja wanajeshi watatu na yule jamaa wa nne.

Wakasema vaa twende kituoni, na gari mpaka kituoni wakafika reception wakasema tumekuja kumchukua mdogo wetu muda huu, polisi wakaanza hizo sio protocol dogo alikuwa analeta fujo, wakasema mkitaka pafungwe hapa leo huyo dogo msimtoe uone.

Ikabidi waende kumtoa selo usiku saa6, nimekaa mbali naogopa hapo, baada ya kumtoa jamaa akasema nitakutafuta, tukaondoka.

Nawapa hongera bakabaka wana nidhamu kubwa sana.bora urafiki na bakabaka.

Share kisa chako na bakabaka.

Mtu yoyote aliyepo kwenye chombo cha ulinzi na usalama sio mwenzako. Akipewa order ya kukinukisha akikukuta hatojali wewe ni rafiki yake. Order kwake ni muhimu kuliko urafiki wenu.

Don’t get too comfortable na watu wanaovaa sare. Jiepushe nao ikiwezekana.
 
Unavyoandika tu unaonekana kichwani ni mweupe ngoja nikuache kwa akili hizi lazima utaamini ukijenga urafiki na wanajeshi wanaweza kukutoa kwenye mikono ya polisi na siyo kutafuta elimu ujue haki zako za msingi ili uweze kujisimamia
Huna unalojua mdogo wangu.

Endelea kukaa kwa mama maisha yatakufundisha siku.
 
Hawa watu hakuna wanalojua mkuu.

Kwamba Sheria haiwezekani Hilo?

Nilishaingia kituo cha polisi mwaka Fulani kipindi Cha mwaka mpya zoa zoa ile ikanikuta.

Kufika pale tukaambiwa kaeni chini usiku huo, badala ya muda akaingia jamaa kachafuka kwenye mabega na wawili wakiwa nyuma yake.

Nikamuona mkuu wa kituo kaja jamaa akasema yupo wapi huyo, mkuu akatoa amri akatolewe.

Jamaa katolewa kituoni anaburuzwa analia kama mtoto. Wale mabakabaka wakambeba wakaondoka naye.

Wengi hawajakutana na hizo hadha kule ni pabaya sana, na utemi bado upo.
Hawajui na hawatembei..Wanadhani maisha yanaishia kwenye mazingira waliyoyazoea,
 
Mtu yoyote aliyepo kwenye chombo cha ulinzi na usalama sio mwenzako. Akipewa order ya kukinukisha akikukuta hatojali wewe ni rafiki yake. Order kwake ni muhimu kuliko urafiki wenu.

Don’t get too comfortable na watu wanaovaa sare. Jiepushe nao ikiwezekana.
Mkuu nalifahamu hilo.

Ndio maana urafiki wangu inakuwaga na mipaka sana.

Nashukuru kunikumbusha hilo.
 
Back
Top Bottom