Weka urafiki na wanajeshi (bakabaka) hutojutia

Hakuna mtu wa kumtoa Mtu mwingine kinguvu awapo kituo cha Polisi, hii yako ni Chai kama chai zingine
We sema hujawai kutana na hizi issue.

Kuna mjeshi wa 841kj alimpiga makofi mkuu wa kituo wa eneo hilo alafu we unasema nini
 
Kwenye mada,kuna kasomo kazuri. Ila,unataka kuharibu.
-Labda nisiingie kiundani zaidi,mambo yao hayanihusu, ila hawa jama hawanaga mafundi kwenye kambi zao? Kiasi cha kumzowesha raia kwenda kutengeneza magari! Navyojua mimi kama ni gari la jeshi, likiharibika njiani,bila kujali umbali,breakdown ya jeshi italifata,kama waliokuwemo hawana element ya ufundi au wao wasipoamua kumtumia fundi karibu,na pale wanapoona shida si kubwa.
-Si kwamba wanawake wanajeshi hawaolewi na raia. Kugegedwa sawa,inawezekana sana tu. Kwa hiyo,dogo kamzalisha tu huyo demu mjeda na akamuacha? Au walioana af akawa anafanya ujinga wake!
Wape staha yao, ila sidhani kama kuna mwanajeshi mwanamke anaweza kuzalishwa hivi hivi na akaachwa aendelee na kazi. Kama nfo hivo inawezekana,nidhamu kwao ni nini? Maana hata hilo ni moja wapo wa mambo ambayo ni mwiko kwa mwanajeshi mwanamke kutokujiheshimu.
Japo na kwa mapolisi sijui,ila haitakiwi.
Uongo punguza. Mpaka mtu anakuwa mkuu wa kambi, cheo chake si cha kuchukulia poa ujue? Hivyo, huyu mtu hata kama amestaafu yupo uraiani, bado anaongozwa kijeshi, huijiwa na Military Polisi(MP), polisi itamlipoti tu jeshini, watakuja wachukue mtu wao,lakini kuwekwa ndani kituo cha polisi!? Halipo na halitatokea.

Hiyo mikoa unayosema kambi furani na kambi furani wana ugomvi, kama Somalia sawa. Kwenyebkambi za mahalamia nakubali.
Ila jeshi la nchi,eti kambi zina ugomvi? Wa nini labda?
Weeee, kambi za jeshi si Simba na Yanga ndugu yangu.
 
We sema hujawai kutana na hizi issue.

Kuna mjeshi wa 841kj alimpiga makofi mkuu wa kituo wa eneo hilo alafu we unasema nini
Halafu kikifata nini? Japo uwezekano wa hilo jambo ni 0.00001%
 
Anhaa mkuu hayo si magari ya jeshi magari binafsi yao anaingia kota wanapoishi.

Dogo anaenda kuchukua gari anatengeneza na marekebisho mengine.
 
Huna akili.

Kwanza itoshe kusema hujasoma nilichoandika

Kaa kwa kutulia mdogo wangu, acha papara.
Haha yani we ndo unaniita mimi sina akili? Wewe unaesema wanajeshi wameenda kituo cha polisi na kuleta varangati mtuhumiwa akaachiwa? Unafikiri hao wanajeshi hawapendi ajira zao siyo?
Wao wenyewe wakifanya jinai wanakamatwa na kuwekwa lockup za polisi wakati utaratibu wa kuwarudisha kwenye kambi zao ukiwa unaendelea.

Kwa kifupi siyo kila askari unaemkuta Pale kituo cha polisi anaweza kumuachia mtuhumiwa kazi yake ni kumlinda mtuhumiwa awe salama asitoroke wala asitoroshwe , hakuna mtu anaeweza kuleta ubabe na mtu akatoka kwenye lockup ya polisi mzee, hata huyo polisi mwenyewe awe rafiki yako hawezi kukuachia bila utaratibu sasa ndo aje aamrishwe na mtu mwingine?

Mtu yeyote anaejua utaratibu wa kisheria huwezi kumdanganya hivi na akakuamini utaendelea kudanganya mtu ambae hajui chochote kuhusu utaratibu wa kisheria
 
Wapi nimesema varangati naomba unionyeshe sehemu nimesema walileta varangati?

Nilisema walisema mdogo wetu lazima atoke lasivyo hapatoshi hapa.

Walienda kumtoa dogo lock up.

Onyesha walipo leta fujo


Soma kwa kutulia mdogo wangu
 
Hapo tayari walivunja kanuni na sheria kwa kumtoa mtuhumiwa kwenye jela bila kuzingatia miongozo ya kisheria, wanapaswa wawajibishwe, msipende kuishi Kitaleban Taleban.
Kama dogo alionewa, kuna mbinu mahsusi za kisheria zilipaswa kufuatwa.
 
Ni kweli kabisa. Wako well drilled and trained. Poa sana.
 
Hizo ndio operation zao kubwa wakat wenzao Wana operation iron sword, operation Al aqsa floods.
 
Wapi nimesema varangati naomba unionyeshe sehemu nimesema walileta varangati?

Nilisema walisema mdogo wetu lazima atoke lasivyo hapatoshi hapa.

Walienda kumtoa dogo lock up.

Onyesha walipo leta fujo


Soma kwa kutulia mdogo wangu
Hayo maneno ya mdogo wetu lazima atoke hiyo ndo varangati yenyewe.

Yule polisi unaemkuta Pale kituoni hata awe rafiki yako au baba yako mzazi yeye mwenyewe akishakukuta umeingizwa lockup na taarifa zako zimejazwa kwenye vitabu hana mamlaka yoyote ya kukuachia achilia mbali kuwa yeye ni rafiki yako yaani hata awe baba yako

Sasa hapo ndo aende mtu mwingine kuamrisha kuwa mtuhumiwa aachiwe itawezekana kweli? Mbona utaratibu uko wazi mzee, njia pekee ya mtu kuweza kuachiwa hapo ni kufata utaratibu tu hakuna njia yoyote ya kibabe inayoweza kutumika

Njia yoyote kinyume na utaratibu ikitumika na ukafanikiwa kumtoa mtuhumiwa kituo cha polisi bila utaratibu na ukabaki hai basi nyuma yako utafunguliwa kesi ya kumtorosha mtuhumiwa na utafanyiwa msako siyo wa kitoto
 
Rudi soma nilichoandika mdog wangu .

Una tatizo kwani?

Soma tena kisa kilivyokuwa

Acha papara
 
Hizo ndio operation zao kubwa wakat wenzao Wana operation iron sword, operation Al aqsa floods.
Wewe unataka jw wafanye operation sword na nani?

Au al aqsa floods wafanye na nani?

Mkuu mbona hueleweki unaloongea?

😂😂
 
Sawa.
 
Hao unaowaona afya mgogoro ni hatari sana
Kaa nao mbali
 
Rudi soma nilichoandika mdog wangu .

Una tatizo kwani?

Soma tena kisa kilivyokuwa

Acha papara
Kisa chako ni cha kufikirika hakina ukweli hakiwezi kufanikiwa kwa njia hiyo, labda kama umeongeza chumvi na hiyo chumvi ndo imeharibu hii stori

Inawezekana jamaa walienda kiungwana na wakafata utaratibu na dogo akaachiwa ila wewe umekuja kuiwasilisha kwa njia ya kuwa walienda kibabe.

Ubabe pale haufanyi kazi mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…