Kuna watu na sehemu za kuzungumza lugha ya kiungwana lakini siyo kwa CCM na machawa wa CCM. Kama mngekuwa waungwana mngekemea mauaji ya 29oct.
Mngekemea utekaji, mauaji na ufiraji unaofanywa na makundi ya watekaji wa serikali ya CCM.
Mngekemea uhuni unaofanywa na tume na vyombo vinavyosimamia uchaguzi kutotoa haki kwa watanzania wa vyama vya upinzani.
Mngekemea polisi wasivyotenda haki na kupiga, kuua na kutofuata sheria dhidi ya wapinzani.
Mngekemea DPP na mahakama kuwafungulia kesi za mchongo viongozi na wanachama wa CHADEMA kwa manufaa ya CCM.
Hadi mbadilike muonyeshe uungwana na kuheshimu haki za msingi za raia nchini.
CCM ni chama Dola hakuna wanachama hao unayosema, na kama lingekuwa na wanachama hao kisingeiba kura, kuteka na kuua wapinzani wake, kukataa uchaguzi huru na haki na kutumia polisi na mahakama kukandamiza wapinzani wake.
Mfumo wa maisha? Hujitambui au umechanganyikiwa, enzi za TANU kilipokuwa chama kimoja mfumo wa wajumbe kumi kwenye shina nk walitumia mfumo huu, lakini baada ya mfumo wa vyama vingi haupo.
Na CCM haipo kwenye mioyo ya walio wengi, jaribuni kufanya uchaguzi huru na haki mtapigwa saa mbili asubuhi. Sasa hii kweli utakuja na upotoshaji kutetea uongo halafu unataka uungwana.
Ukija na ujinga wako wa uchawa utakuwa unapakatwa.