Megalodon
JF-Expert Member
- Apr 9, 2021
- 5,233
- 12,398
- Thread starter
- #81
Hii ni fantasy ya kukataa responsibility,Nimewaacha muomboleze siku yenu kwa amani kwanza.
Kukaa kimya hakumaanishi kuwa sijaona.
Magufuli ni sehemu kubwa ya sababu nchi hii imefika hapo ilipofika.
Magufuli aliikuta nchi iko njiapanda, alikuwa na nafasi kubwa ya kuongeza demokrasia na haki, hakufanya hivyo, akaendeleza udikteta, kuua upinzani, kununua wanasiasa, na ujinga mwingi kama huo.
Huwezi kumtenganisha Magufuli na haya yaliyotokea.
Viongozi wa CCM na serikaki wa juu huko wanashindana kwa kushusha standards, kwa hiyo kuna standards fulani za demokrasia zilikuwapo kipindi cha Kikwete, si kubwa sana, lakini zilikuwapo, Magufuki akazishusha.
Magufuli akasema anataka kuua upinzani, akanunua wanasiasa wapinzani. Aka set a new low. Akafanya mambo ya utekaji na uuaji wa wapinzani kuwa kawaida.
Hilo ndilo lililomuwezesha Samia akafanya aliyofanya. Magufuli angeongeza demokrasia, Sania asingeweza kufanya alichofanya.
Sasa hapo unapousema utawala wa sasa kama kitu ambacho kimejiweka chenyewe tu bila kutumia msingi aliouweka Magufuli, nakuona huijui dunia tu.
Huelewi wapi?
Samia ameanzisha mabaya yake nasio muendelezo wa mabaya ya JPM
Kwa mfano, mauaji ya halaiki yaliyofanywa na Samia root cause ni JPM ni kujibu hoja kwa kukimbia responsibility
Unless tukubali pia JPM alifanya mass killing ndio akakalia kiti
Democracy inamipaka yake ila kwa Samia bali ni kupokonya kwa mabavu