Wengi mnatokwa povu tu ila huu ndio ukweli wa kwanini SA imeamua kutetea haki za wapalestina kwa kufungua kesi ya mauaji ya kimbari dhidi Israel

Hiv vita Kati ya Israel na Palestine na kutaka nani atambuliwe ni taifa au ni kati ya waarabu na Jews?
 
Wapalestina nimbwa towachawafe wanarohoo mbayasana walewachewafe ningekua mimi raisi
Wa islaeliwaleningewaua kwasumuwafe kizazikizima walenimbwa
 
Kwahy SA ndio wenye uchungu zaidi kwa Palestina zaidi ya nchi za kiarabu.?
Mbona unaongea mambo ya kitoto kaka. Mimi nilikuwa nakuchukulia kuwa wewe ni mmoja wa great thinker ambae hawezi kuandika kitu bila kushirikisha akili yake kwanza. Lakini sasa unanishangaza mkuu kwa kuuliza swali ambalo hata mtu aliejiunga leo JF hauwezi kuuliza baada ya kusome thread vizuri.

Eti kwahy SA ina uchungu kuliko waarab 😀😀😀
Kwani kuwa mwaarab au mtu mweusi ndio kigezo cha kumsaidia mwaarab au mtu mweusi mungine?

Wewe katika maisha yako haujawahi kuona au hata kusoma humu JF kuwa mtu kasaidiwa au anasaidia na rafiki au mtu baki baada ya ndugu zetu tena wengine wa damu wakiwa hawawajali wala kuwasaidia chochote?

Kuna jamaa alileta thread humu nimeisahau, anadai kuwa baada ya wazazi wake wote wawili kufariki alichukuliwa na mjomba wake akaletwa Dar es salaam kulelewa. Jamaa anakwambia baada ya miaka kadhaa mke wa mjomba wake (shangazi) na watoto aliozaa na mjomba wakaanza kumfanyia vitimbi, mbaya zaidi hadi mjomba akamgeuka na kuwa upande wa mke.

Jamaa alikuja kusaidiwa na mtu baki ambao hakuwahi kufikiria kukutana nae, jamaa alimsaidia katika swala la elimu na hadi kazi. Hivyo kuwa mwaarab haimaanishi kuwa ukipata matatizo basi waarab wenzako ndio watakusaidia kwani dunia ya leo hata ndugu wa baba mmoja wengine hawasaidiani.

Hivyo Afrika kusini imefanya kama alivyofanya huyo jamaa aliemsaidia dogo alietengwa na ndugu zake. Nimemwambia kuna sababu mbili hapo juu zilizopelekea Afrika kusini kufanya hivyo. Sasa wewe haujasoma sababu umekimbilia kuja kuuliza swali la waarab.
 
Mbona unaongea mambo ya kitoto kaka. Mimi nilikuwa nakuchukulia kuwa wewe ni mmoja wa great thinker ambae hawezi kuandika kitu bila kushirikisha akili yake kwanza.
Nimesoma nikaishia hapo, hilo ndilo jambo la muhimu kuliko hayo mengine 😎
 
Ndugu waungwana hapa jakwaani kwetu kuna vijana wengi ambao wamekuwa waki comment ujinga katika thread za watu wenye akili, na elimu kubwa kushinda wao,

Hizi dharau sasa🤣🤣 kama vipi ID zionyeshe detail ya kiwango cha Elimu kisha majukwaa yatengwe kwa level za elimu.m au akili.
 
Kenge kweli!
 
Point #1 kwani walitawaliwa na Taifa gani?
 
Acha kuandika upuuzi ndugu yangu, kama wangekuwa hawawataki leo hii nchi ile ingakuwa haina mgeni mweusi hata mmoja.

Kila nchi huwa na vijana wa hovyo kama panya road ambao huanzisha kizaa zaa kwa lengo la kupora, kuuwa, kujeruhi nk. Haya tunayaona hata hapa kwetu panya road watanzania lakini wanavamia nyumba za watu usiku wanajeruhi na hata kuuwa watanzania wenzetu. Sasa hilo nalo tusemeje?

Kama serikali ingekuwa haiwataki hao uliosema basi ingeanzisha operation maalumu madukani, mabarabarani, majumbani, kwenye mabasi nk. Lakini pia wasingejichosha kuwazuia raia wao kuwapiga wageni maana ingekuwa kama wamewarahisishia ya kuwatoa wageni. Za kuambiwa changanya na zako.

Kuhusu swala la Putin hata mimi ningekuwa raisi nisingemshika. Haiwezekani sheria zitumike upande mmoja na kuacha upande mungine.

Aliekuwa raisi wa Marekani ndugu George W Bush aliwahi kuivamia Iraq na kuuwa watoto, kina mama na watu wasiokuwa na hatia kwa kisingizio kuwa anaenda kutafuta silaha ambazo Umoja wa mataifa walienda kukagua na kusema kuwa hamna silaha, lakini Bush alipuuza walichoongea wataalam wa Umoja wa mataifa na badala yake akaenda kuivamia nchi hiyo kwa sababu anazojua mwenyewe.

Sasa mpaka vita vimeisha hakuwahi kukuta silaha, ameuwa watu, wengine amewaacha vilema, wengine hawana makazi tena alafu cha kushangaza mpaka leo bado anadunda na kupanga mpango wa kumkamata mwenzao kwa kufikiri kuwa yeye ni mnyonge.

Hivyo mimi nafikiri angeanza kwanza kukamatwa Bush alafu ndio afuatie Putin.
 
Kiki
 
Hiv vita Kati ya Israel na Palestine na kutaka nani atambuliwe ni taifa au ni kati ya waarabu na Jews?
Mbona ulichoandika hakieleweki brother?
Au ni typing error?
 
Wapalestina nimbwa towachawafe wanarohoo mbayasana walewachewafe ningekua mimi raisi
Wa islaeliwaleningewaua kwasumuwafe kizazikizima walenimbwa
Myahudi usiejua hata kuandika. Wewe utakuwa myahudi wa Nachingwea porini kabisa ambapo hakuna hata shule.
 
Point #1 kwani walitawaliwa na Taifa gani?
Afrika kusini ilitawaliwa na UK ambao wanaongea kingereza, pamoja na Uholanzi ambao wanaongea akrikans.

Ila miaka ya 60 waingereza walitoa uhuru kwa hawa wanaongea Afrikaans na hapo ndo kimbembe cha mateso ya mtu mweusi yalipoanza rasmi. Walipitia yale ambayo hawakuwahi kuyapitia huko nyuma.
 

Over 1,000 organizations unite in support of South Africa’s genocide case against Israel at ICJ​


Popular movements, political parties, unions, organizations call on states to back South Africa's genocide case against Israel​


Seda Sevencan | 11.01.2024
 
Kaka vita sio kitu kizuri, je ulilaani pia Hamas waliporusha makombora mia ngapi sijui kuipiga Israel?!
 
Chanzo cha hekima na maarifa ni Bibilia yote yanayotokea yameandikwa kwenye kitabu hicho, kinachoendelea kwa Sasa ni maandalizi ya Amani ambayo Israel nitakuja kufanya na hizo nchi za kiaarabu ndipo baadae Russia pamoja na wafuasi atakuja kuipiga Israeli, katika vita hivyo ismaili(ishara ya kiama) ndie atakuja ukamua
 
Na kuhusu SA kuhifadhi viongozi wa Hamas. Hili unalifahamu mtoa mada?
Kwani kumhifadhi mtu anaepambania uhuru wa nchi yake kuna tatizo?

Mbona sisi tuliwahifadhi viongozi wa anc ambao mkaburu aliwaita magaidi kisa wanapigania ardhi yao, faifa lao,haki zao na usawa wao.
 
Kaka vita sio kitu kizuri, je ulilaani pia Hamas waliporusha makombora mia ngapi sijui kuipiga Israel?!
Mkuu tusiangalie ya Hamas pekee, tukumbuke kuwa kabla ya 7 October kulikuwa na uvamizi wa usiku uliyokuwa unafanywa na askari wa Israel katika ardhi ya wapalestina huko West Bank.

Yani askari walikuwa wanaingia ndani ya majumba na kuwatoa watu usiku, kisha nyumba zile zikawa zinagawiwa waisrael, hiyo ni mbali na ujenzi waliokuwa wanaujenga kinyume na sheria za kimataifa.

Mbaya zaidi vijana wanaoondolewa katika nyumba zao wanapojaribu kuandamana kupaza sauti zao ili dunia ione kile kinachoendelea, jeshi la Israel linazima maandamano hayo kwa nguvu, huku likiwajeruhi, kuwakamata bila sababu ya msingi na wengine kuuwawa kabisa.

Sasa hebu fikiria kama wewe ndo ungekuwa mmoja wa vijana wa kipalestina au taifa lolote unafanyiwa hivyo ungefanyaje au jisikiaje? Maana kila binadamu ana haki ya kuishi kwa amani, lakini sasa hiyo amani hampewi, mkilala hamna uhakika wa kuamka asubuhi bila kuvamiwa na jeshi usiku, mkitaka kudai haki mnapigwa nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…