Wengi tunapenda kumiliki smartphone mbili na wakati mwingine hata zaidi ya mbili. Je, huu si uwendawazimu?

Wengi tunapenda kumiliki smartphone mbili na wakati mwingine hata zaidi ya mbili. Je, huu si uwendawazimu?

Inategemea na shughuli za MTU sio kila mtu ameajiriwa kwa wahindi
 
Hayo mambo niliyakataaga kitambo sana mkuu. Kwanza unakuwa na mzigo wa masimu. Mimi hata kumiliki simu mbili kwa pamoja napo sitaki. Namiliki simu moja tu ya line mbili. Simple
 
Ifike mahali tuanze kujiuliza hivi ni akili kumiliki simu janja zaidi ya moja tena huku kila moja ikiwa na line 2? Yaani line 4 kwa wakati mmoja?

Hivi hatuoni huu ni uwendawazimu kabisa hasa simu hizo zinapkuwa ni kwa matumizi ya kawaida tu kama vile kuwassiliana na ndugu, jamaa na marafiki?

Unatembea na simu mbili(line 4) halafu ndugu yako kijijini hata kilo ya unga kwake ni mtihani!!

Tunalia na tozo, ila hatujui kumiliki line 4, ni zaidi ya tozo za Samia.

Sielewi kabisa tunawaza nini!!
Acha ushamba. Kama huna matumizi makubwa ya simu nyamaza.

Simu moja nimeweka line mbili za mawasiliano. Na ni kwa sababu maalum kulingana na mazingira ninayoishi. Sehemu moja inashika voda tu na sehemu nyingine halotel tu.

Simu nyingine nimeweka line ya mpesa na halopesa. Sababu ya kutumia smartphone ni uwezo wa kutunza sms nyingi.

Wendawazimu wangu uko wapi hapo.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Hahahaaaa!!!
 
Swali la ajabu kwa iyo kumiliki smartphone mbili imekua nongwa watu bhana mmekosa vya kupost
 
Wafanyabiashara wenzangu SI kitu Cha ajabu kuwa na smartphone mbili au zaidi,
Ninarafiki yangu yeye anazo 5 ni mmiliki Kwa vyuo na Hospitali,
Suala si kumiliki kikubwa ni unazifanyia Nini?
 
Swali la ajabu kwa iyo kumiliki smartphone mbili imekua nongwa watu bhana mmekosa vya kupost
Na mimi nimemshangaa sana mwanaharakati wetu yaani simu zilivyo nyingi hizi second user mpaka za laki tatu au mbili unapata Leo roho inamuuma...kwa hiyo je na yeye amavyomiliki wanawake michepuko tumwuonaje
 
Nilivokuwa sina Pesa nilikuwa na mawazo kama yak, saivi ni tofauti kabisa, Pixel 6 Pro inakaa na line ya Voda, Iphone 13 ProMax inakaa na line ya airtel!
 
Kwako ni uwendawazimu maana huna uwexo wa kumiliki smartphone 2,siku ukimiliki pesa utanunua hata simu 4 kila simu itakaa na line yake
Tena kila simu itakuwa na line 2 jumla 8 sijui atajiitaje hapo 😀
 
Nakumbuka nilikuwa na miaka 21 nikanunua sim ya 500k ngj watu waongee kamavile hela yakwao 😀

Tuache makasiriko hela kama ipo ipo tu usimkasirikie mtu akitumia hela zake nawe pambana upate uone kama hizo sim 2 ni uendawazimu mkuu
 
Mi mwenyewe hapa nilikuwa na 5 na zilikuwa hewani ila nimebaki na 4. Nimetenganisha matumizi tu.
° Kuna ya biashara lipa namba
° Ya watu wa kazini tu
° Ya watu wote isipokuwa wa kazini. Hii inanisaidia nawazimia kazini halafu naendelea na mishe nyingine.
° nikimtongoza demu nampa namba ambayo hata home haifiki inaishiaga dukani tu. Hii hata kubeti ndio naitumia.
 
Back
Top Bottom