Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi


Kikubwa huyo mtoto alijua kazi ni kipimo cha utu regardless ya kazi ya kufanya.

Sasa huyo mtoto ambaye kaona mzazi kila siku anafanya kazi, umwambie asiwe daktari wala mwanasheria eti akae tu ndani kuwa goli nyanda, unadhani atakuelewa?

Ugoli nyanda unaandaliwa, mtu aliyelelewa mazingira ya kazi atahitaji kufanya kazi tu hata umpe kila kitu.
 
Napenda nijue maisha halisi ya mleta mada. Je ameoa? Mkewe anafanya kazi? Kazi gani? Je familia yale ikoje?
 
Maisha ya sahvi yalivyo magumu tufanye tu kazi wote tusaidiane wote mmetoka familia za chini aisee mtafute ili atleast watoto waishi maisha mazuri na kuwandalia kesho yao nzuri.
 
Yaani ulijuaje aina ya chupi za watu we nae
 
Kuruhusu mkeo kufanya kazi ni sawa na kupanda mwembe karibu na shule .

Kwa sisi ambao tumeshayaona mengi ya fedheha kwa wake za watu maofisini,,

Nasema kama unampenda mkeo mbakishe nyumbani,,au mfungulie biashara binafsi..

Ukimpeleka kazini basi umempelekea wanaume wenzio.
 
Kwanza umeoa??Una- miaka mingapi kwenye ndoa??
Shida tu na umaskini na hali ngumu ndo zinafanya wanawake wawe bizy na kazi kupita kiasi..kazi za kutoka nyumbani saa 1 asubuhi kurudi saa 12.
Kama wewe umeoa na unaishi na mkeo utagundua wanawake ni viumbe complex sana, miili yao sio kama ya kwetu, hisia zao sio kama za kwetu- hawakuumbwa wastahimili shuruba nzito nzito either physically au mentally - miili yao yenyewe na changamoto tosha.
Sasa hiko hivi kijana- mwanamke afanye kazi kwa uhuru na kwa kupenda mwenyewe na kurelax huku akipata muda mwingi wa kupumzika na kufanya mambo ya kike - apike, afanye shopping, afuatilie watoto, amuangalie mume wake, afuatilie miradi ya juujuu ya mume wake kama shushushu..kama mme ana vitega uchumi apite pale azugezuge, aende jumuiya, kanisani n.k...Jukumu la kuhangaika sio lao..Mungu aliwapa jukumu la kuzaa kwa uchungu, sisi kutafuta kwa jasho - Na ndio UANAUME huo..ukisikia BABA..ndo hiyo sasa...
Baba hupati heshima kwa sababu unamlala mkeo na kumzalisha but KUPROVIDE, KUMLINDA YEYE NA FAMILIA KIMWILI NA KIHISIA..
Ikienda kinyume na hapo..ugomvi utaibuka tu na vidharau vya hapa na pale kwa sababu inside deeply wanajua sio majukumu yao.
Kuna watu wake zao wanafanyakazi lkn ada ya watoto, kodi ya nyumba n.k lazima utaambiwa mwanaume - BABA akiona hauko vizuri n.k ndo nao wanajiongeza lkn hawafanyi tu...

Kwa hiyo usiongee vitu kirahisi hivi..
Tunawapenda wake zetu, dada, mama zetu na wanaume wengi wanajitahidi na wanapenda wakamilishe kila kitu..ilitokea mama anaingiza kipata - USIBWETEKE jiongeze na tumia akili.umsaidie kwa mawazo, maamuzi, ushauri n.k..ukijifanya et ni wajibu wake..- UTAPOTEA
 
Pia ukifikiri unaoa ili mke akusaidie hayo majukumu uliyoyataja..huelewi unaongelea nini..na hujapitia shuruba za wanaume wewe...Ukioa kichwa chako kimejipanga et mke wangu afanye kazi ili ajitimizie majukumu yake..wewe usioe tu.Hiyo ya mke kupata ije kama by the way tu....na akili yako wala isijali..FOCUS kama mwanaume..utajikuta hela zake anazitumia kwako indirectly tu...

LAKINI ET USEME-NINAO MKE ANAYEFANYA KAZI ILI ANISAIDIE AU AWEZE KUSAIDIA NDUGU ZAKE..wewe kijana- utalazwa nje
 
kama unaweza ku provide kila kitu kwenye familia, mke hatakiwi kufanya kazi
 
Wewe umeoa? Kama bado mambo ya ndoa yaache yalivyo. Ni case by case hakuna general principle.

N. B. Wanawake ni visirani sana.
Hahaha....ndo maana tumeambiwa tuishi nao kwa akili.Mwanamke atabaki mwanamke tu....ndo maana vile vi tomboy inafika muda vinasalimu amri..

TUNAONGELEA EQUITY SIO EQUALITY
 
Tafuta hela mkuu....umemuona Wapi Mke wa Mo anafanya Upatu?

Ni umaskini tu unatutuma lakini Mke anatakiwa akae Nyumbani ai njoy maisha.
 
kama unaweza ku provide kila kitu kwenye familia, mke hatakiwi kufanya kazi
Ndio umaskini tu unatutuma.

Wanaume wanapata pesa wanaishia kuhonga na kunywa pombe tu. Watoto siku hizi wanalelewa na Wanawake.

Hata wanawake wenyewe hawapendi hizi kazi.

Ukiwauliza wasema ukweli watakwambia.

Mke wa Mengi pamoja na Mume wake kuwa na miradi na Pesa za kutosha za Kufanyia biashara hutamkuta kamwe anahangaika na Nguo kariakoo.

Na ndio maana Mwanamke akipata Pesa zake we jifanye unazitaka uone cha moto.
 
Kwa akili za mtoa mada, yupo radhi mkewe afanye kazi hata ya "umalaya" Ili mradi tu apate pesa!

Tusilazimishane kuona vitu Sawa Sawa. Kila watu Wana mitizamo tofauti katika mambo mbalimbali
Wanaitwa wanaume wanaopenda mteremko......Wanawake hawapendi kabisa Mwanaume wa aina hii hata siku moja.
 
Hoja inamashiko vizuri, ukitaka lakini wewe unaamua kutoipa mashiko, ukitaka muishi vizuri na mkeo basi muishi Kwa kufata maandiko hasa kama mnaamini katika Imani. Mambo mengine yakimaisha ni Qadar tu, mnaweza kupambana wote lkn still mklala njaa.
Hahaha
 
Kwani akifanya kazi hawezi kuwa pambo au kumburudisha mumewe?

Kuna wanawake wanaofanya kazi na bado ni warembo kuliko wanaokalizwa nyumbani.
Hoja yako haina mashiko
Mtibeli umeonesha udhaifu mkubwa sana kwenye thread hii.

Watibeli hawapendi mteremko wewe ni Mtibeli wa Kabila gani?
 
Wanaume wote wanaotaka wake zao wafanye kazi ni wavivu.

Sababu inayofanya wanawake wengi hivi sasa kujihusisha na utafutaji ni wanaume wengi kutotekeleza majukumu yao ipasavyo ingawa wapo wanawake ambao wanahudumiwa kwa kila kitu lakini hawaridhiki.

Tafuta hela mkuu halafu muhudumie mkeo kwa kila kitu.

Maana halisi ya goli kipa siyo kusubiri aletewe ila ni kulinda himaya yake na kupoza mashambulizi yanayotoka kwa upinzani na kutazama upya namna ya kuanzisha mashambulizi mapya.

Mwanamke anapokuwa nyumbani anakuwa muangalizi wa karibu wa familia na mali ya mumewe.

Pale ambapo nguvu hasi inapotoka nje kuingia ndani kwake yeye huwa mtu wa kwanza kuipoza na pia yeye huwa wa kwanza katika kuongeza nguvu chanya kwa mumewe katika utafutaji.

Leo hii wengi wanatumia msamiati wa goli kipa kwa mwanamke bila kujua maana yake.

Nawapa pongezi wanawake wote ambao wanatekeleza majukumu yao kama mhimili wa nyumba bila hata ya kuwa na kazi na pia nawapongeza wanawake wote ambao wameamua kujishughulisha siyo kwa sababu ya kukidhi matakwa yao ila kwa ajili ya kuongeza nguvu kwa waume zao.
 
Wanaume wote wanaotaka wake zao wafanye kazi ni wavivu.
Nilikuwa nao marafiki wa hivi nikaachana nao.

Tabia zao ni za hovyo.

Ukiwauliza kwanini unataka mwanamke wa hivi wanadai eti Mwanamke awasaidie majukum na bills za nyumbani.

Yule jamaa mmoja alipigwa vibuti hadi akajuta.
Yeye alikuwa analazimisha lazima apate Mwl, Secretary na hata Yeyote mwenye Degree.....sasa mademu wakawa wanamlia pesa tu kumbe wana watu wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…