Wengi wetu ni wakopaji sana kwenye mabenki ila hili ni sikio la kufa

Hii kasunba mtu akipata tu chek namba mbio kuenda kukopa.nna jamaa yang amekopa 20 ana service deni mpaka llishe atakua kalipa milioni 53.6 anaishi kwa kuandika proposal
Hahahahaa mkopo ni noma! Nakumbuka mzee wangu alikopa hela ikawa inakatwa na akawa anapokea 67,000/= nikwambie alibaki viraka tu na aliteseka kwa miaka takribani 10!

Halafu hawa jamaa ni wajinga sana wana kitu kinaitwa kudouble mkopo ukikaribia kumaliza unachukua mwingine halafu hela kiasi unalipa deni la awali hapo ndo roho mkononi!
 
Nimejitahid kukuelewa ila nimeshindwa
 
Kuna benki zinajitutumua kufanya kama defined bank services providers lkn ni wazushi sana.
TZ asilimia 80 ya kila mtu au taasisi inaishi kwa utapeli.
Sitowataja ila ni kati ya benki mbili maarufu zinazotumiwa na serikali kuwakopesha watumishi.
Kutotaja hili ni unafiki. Mostly, wafanyakazi wa serikali wanakopa NMB, CRDB, ABC Bank, na vitaasisi uchwara Kama Fanikiwa, Maboto, Ultimate, Bayport etc
Niseme ukweli benki ni taasisi za wizi asikuambie mtu. Zaidi na zaidi hawa wamezidi ni wadanganyifu.
Utapeli ndio faida kwao.
Siku zote ukirafuta mkopo lazima wewe ndio uwe unacontrol mazungumzo. Ukiwaachia bank lazima wakuue.

Unaenda bank, wanakwambia wakuoe pesa ambayo hata mwenyewe hukupanga kuchukua na wewe unakubali.

Wakishakupa mkopo wa miaka 9 ( miezi 108) wanajua kabisa hutaweza kujinasua, utaishi kwa top up tu mpaka unastaafu.

Unastaafu bado utakopea pension.
Ukishataka kulipa deni, wanajua unataka kukimbia lazima ukabwe ubaki.


Na Kama una deni la miaka 9 wanajua hutaweza kuvumilia liishe, utaishi nao tu.

Siyo vizuri kukopa mkopo wa muda mrefu sana, na pia siyo vizuri kukopa mkopo kwenye vitaasisi ambavyo na vyenyewe hukopa bank.
 
Hii kasunba mtu akipata tu chek namba mbio kuenda kukopa.nna jamaa yang amekopa 20 ana service deni mpaka llishe atakua kalipa milioni 53.6 anaishi kwa kuandika proposal
Shida ni kwenda bank bila maamuzi. Bank wao ukiwaonesha salary slip yako, watakwambia kwa Mshahara wakonwatakupa milioni labda 20 kwa miaka 9.

Kwasababu wewe unachotaka ni pesa huwezi kuwaza hiyo miaka 9 itaisha lini Wala ndani ya miaka 9 utakuwa umelipia riba kiasi gani.
 
kopa kwa lengo la kibiashara na uwe unaifahamu biashara

MKOPO SI HISANI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…