Siku zote, wenye akili, wenye hekima na wenye dhamira njema ya kutatua tatizo lolote, wanapogundua kuna tatizo, hutafuta chanzo cha tatizo, kwani ukikidhibiti chanzo cha tatizo, tayari unakuwa umetatua matokeo yake.
Wasio na akili wala maarifa, wao hutazama matokeo. Watabakia kuhangaika na matokeo, na kwa vile chanzo hakijaguswa, basi kuhangaikia matokeo unakuwa ni mradi wao wa kudumu.
Kama kuna mgonjwa ana homa kali, halafu unakazana kumpa mgonjwa huyo dawa za kushusha homa tu, bila ya kutafuta tatizo linalosababisha hiyo homa kali, homa kali haiwezi kudhibitiwa, homa itaponzwa lakini siyo kuondolewa, na kuna siku huyo mgonjwa atapoteza maisha.
Leo kwenye siasa wamezuka watu wanaitwa machawa. Sifa kubwa ya machawa ni kukosa akili au unafiki. Hawa kutokana na kukosa akili, wanachojua ni kusifia tu, iwe ni jambo zuri au baya, wao ni kusifia tu. Ndiyo maana huwezi kumwona mtu mwenye akili nzuri, halafu ni chawa wa mtu.
Tanzania ya leo, kwa kiasi kikubwa imejaa dhuluma zinazofanywa na watawala na vyombo vya Serikali dhidi ya haki za wananchi. Wenye hekima na wenye akili wanazungumzia namna ya kuondoa dhuluma dhidi ya haki ili nchin yetu iwe na amani ya kudumu. Machawa, au kwa kukosa akili na maarifa au kwa kukosa dhamira njema, hawataki kusikia habari ya haki, wanapiga kelele juu ya amani!!
Hivi utaongelea amani gani wakati watu wanaotimiza haki zao za kikatiba, wanatekwa, wanauawa, wanapotezwa, na wengine kubambikiwa kesi? Hivi ni amani gani anaweza kuwa nayo mtu ambaye ndugu yake ametekwa, ndugu yake ameuawa, ndugu yake yake amepotezwa, ndugu yake amebambikiwa kesi, au watu ambao haki zao za uhuru wa maoni au mikusanyiko zinaminywa na kukanywagwa? Ni amani gani watu ambao wanapachikiwa viongozi wasiowataka kupitia chaguzi bandia, ambazo wananchi ama wananyimwa haki ya kuchagua watu wanaowataka, kupitia uenguaji batili wa wagombea, au uporaji wa moja kwa moja wa kura za wananchi?
Maadui wakubwa wa amani ya watanzania kwa sasa ni hawa wanaogandamiza haki za watu, na misingi ya demokrasia.
Tuimbe wimbo wa haki, maana ni haki ndiyo inayotengeneza amani, na siyo kinyume chake. Maadui wa amani yetu ni hawa wanaochezea haki za wananchi.