2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 3,130
- 4,735
1. Unafahamu ratiba yao ya mlo kabla hajaenda?Binafsi mwezi huu wa tatu hivi karibuni nilisafiri kwenda mkoa X ila ni ndani ndani mpakani na Msumbiji huku.
Kwakuwa ni kwa kaka yangu sikua na mashaka kwenda, bro ameshaoa tayari na pia ana watoto wawili sema anaeishi ni mmoja mwingine yupo kwa shangazi (yaani bibi)
Haya wiki ya kwanza picha linaanza sijui ilitokeaje dogo akavunja miwani yangu ni glasses alidondosha chini, nikamwambia bro akanizungushaa nikasema nitalimaliza mimi mwenyewe.
Sijakaa kidogo USB ya chaja imekatika ila nijua moja kwa moja dogo kaikata ni mtundu mno hili nalo niliongea nae akanizungusha.
Tangu nije hapa yaani ni ugali kwa kwenda mbele😞😞 ni almost wiki ya pili hii labda pasaka MUNGU asaidie niuone wali walau kwa mbaali.
Yaan huyu mama wa hapa najiuliza sijui ana ugomvi na mimi maana tangia nije hata kupika anataka nipike mimi, nikichat kosa anamwambia bro mi nachat tu eti sifanyi kazi ilihali namsaidiaga
Wenye uzoefu hii familia naishije nayo au nirudi tu kwetu 🤦🏽♀️
2. Je huo ugali nao wanakula au unalishwa peke yako?
Ndio maana mimi sitaishi na ndugu yangu kamwe, ndugu lawama ndio kama nyie.
Huoni ulifanya uzembe mpaka dogo kakwaribia miwani na usb yako? Mbona vya babake haaribu aharibu vya kwako tu? Linda vitu vyako acha kumchonganisha ndoa za watu.