Wenye uzoefu wa kuishi kwa ndugu nipeni muongozo

Wenye uzoefu wa kuishi kwa ndugu nipeni muongozo

Binafsi mwezi huu wa tatu hivi karibuni nilisafiri kwenda mkoa X ila ni ndani ndani mpakani na Msumbiji huku.

Kwakuwa ni kwa kaka yangu sikua na mashaka kwenda, bro ameshaoa tayari na pia ana watoto wawili sema anaeishi ni mmoja mwingine yupo kwa shangazi (yaani bibi)

Haya wiki ya kwanza picha linaanza sijui ilitokeaje dogo akavunja miwani yangu ni glasses alidondosha chini, nikamwambia bro akanizungushaa nikasema nitalimaliza mimi mwenyewe.

Sijakaa kidogo USB ya chaja imekatika ila nijua moja kwa moja dogo kaikata ni mtundu mno hili nalo niliongea nae akanizungusha.

Tangu nije hapa yaani ni ugali kwa kwenda mbele[emoji20][emoji20] ni almost wiki ya pili hii labda pasaka MUNGU asaidie niuone wali walau kwa mbaali.

Yaan huyu mama wa hapa najiuliza sijui ana ugomvi na mimi maana tangia nije hata kupika anataka nipike mimi, nikichat kosa anamwambia bro mi nachat tu eti sifanyi kazi ilihali namsaidiaga

Wenye uzoefu hii familia naishije nayo au nirudi tu kwetu [emoji2362]
Toa pesa anunue nyama nakwambia utapendwa husikae kizembe siku moja moja mnunulie mtoto biscuit na juice

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukitaman wali chukua buku mbili yako nenda mgahawa mzuri kajipigie zako wali rudi nyumbani.

kuhusu mtoto we ni aunty yake. siku moja moja unamshikia kiboko unampa za kutosha....ataanza kuheshimu vitu vyako.

Kuhusu shemela kusema ufanyi kazi, ni kwa sababu anakuona umekaa kilege lege...we changamka tu humo ndani penye kukwaza kwazika mhineshe kabisa penye kufurahi na kuchekesha cheka nae! Yani kuwa active tu humo ndani.

Ataacha kukuandama then heshima itafata
Mkuu bro hataki nitoe hata mia … hataki kabisa

pia usiniquote vibaya kazi nafanya sana tu …. naona yeye kakosa tu wa kumchatisha inakua ka kawivu fulani tu

Sijakaa lege lege kama unavofikiria wewe and niwie radhi sana mkuu
 
Back
Top Bottom