Wenye uzoefu wa kuishi kwa ndugu nipeni muongozo

Wenye uzoefu wa kuishi kwa ndugu nipeni muongozo

Binafsi mwezi huu wa tatu hivi karibuni nilisafiri kwenda mkoa X ila ni ndani ndani mpakani na msumbiji huku.

Kwa kuwa ni kwa kaka yangu sikua na mashaka kwenda, bro ameshaoa tayari na pia ana watoto wawili sema anaeishi ni mmoja mwingine yupo kwa shangazi (yaani bibi)

Haya wiki ya kwanza picha linaanza sijui ilitokeaje dogo akavunja miwani yangu ni glasses alidondosha chini… nikamwambia bro akanizungushaa nikasema nitalimaliza mimi mwenyewe

Sijakaa kidogo USB ya chaja imekatika ila nijua moja kwa moja dogo kaikata ni mtundu mno hili nalo niliongea nae akanizungusha

Tangu nije hapa yaani ni ugali kwa kwenda mbele[emoji20][emoji20] ni almost wiki ya pili hii labda pasaka MUNGU asaidie niuone wali walau kwa mbaali

Yaan huyu mama wa hapa najiuliza sijui ana ugomvi na mimi maana tangia nije hata kupika anataka nipike mimi… nikichat kosa anamwambia bro mi nachat tu eti sifanyi kazi ilihali namsaidiaga

Wenye uzoefu hii familia naishije nayo au nirudi tu kwetu [emoji2362]
Unaonaje ukirudi kwenu?
Ukipewa ugali wao wanakula nini?
Wanakula kitu kingine? Kama wanakula unachokula basi binafsi wageni wa aina Yako ni wapumbavu tu.
 
Vyovyote vile, ukishakua unaishi kwa watu jitahidi kufata taratibu zao muende sawa vinginevyo hakuna rangi utaacha ona.
Kuishi kwa kaka ni mtihani mzito...lazima ajipendekeze kwa mkewe..
 
Unaonaje ukirudi kwenu?
Ukipewa ugali wao wanakula nini?
Wanakula kitu kingine? Kama wanakula unachokula basi binafsi wageni wa aina Yako ni wapumbavu tu.
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Sasa mambo ya chakula yamekujaje hapa? Wewe fanya issue yako uondoke vinginevyo Rudi kwako ukale wali ukisubiri issue yako.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Mkuu mtu anayelia lia kuhusu msosi maana yake hana hata uwezo wa kujimudu.
Ukienda kwa watu ukapewa heshima ya kulala pekee inakutosha wewe kula hoteli rudi umeshiba ulale tu.
 
ukitaman wali chukua buku mbili yako nenda mgahawa mzuri kajipigie zako wali rudi nyumbani.

kuhusu mtoto we ni aunty yake. siku moja moja unamshikia kiboko unampa za kutosha....ataanza kuheshimu vitu vyako.

Kuhusu shemela kusema ufanyi kazi, ni kwa sababu anakuona umekaa kilege lege...we changamka tu humo ndani penye kukwaza kwazika mhineshe kabisa penye kufurahi na kuchekesha cheka nae! Yani kuwa active tu humo ndani.

Ataacha kukuandama then heshima itafata
 
Huo ugali unakula peke yako? Kama mnakula wote hayo ndo maisha ya hapo. Wether you abide by the circumstances or quit. Shida yenu mnaenda kwa ndugu zenu na mategemeo ya kula mapochopocho everyday wakati huo uwezo haupo.

Halaf kwa nini unataka kaka yako akurefund vitu anavyoharibu mtoto?
Looh miwani ni almost 260,000 kwa fresh graduate siez afford kwa haraka hivo

Charge ya iPhone ni almost 15k huoni ni hasara

nimesema yeye cuz ana uwezo mkuu pia ni mtoto wake
 
Back
Top Bottom