Nkaburu
JF-Expert Member
- Mar 23, 2023
- 1,638
- 1,961
100%Suala hilo ni la kisaikolojia zaidi.
Waone wataalamu wa magonjwa ya akili/saikolojia haraka iwezekanavyo.
Kwa hali ya kawaida jambo la asili haliwezi kukuchukiza na kukuondolea amani kwa namna unavyojisikia wewe.
Watu wanahonga ama kutoa mahari juu ya jambo hilo hilo, ina maana wanafurahishwa nalo na wanainjoi, iweje kwako?
Ukibweteka, utafika muda hautahitaji kushiriki tendo, maana kwako ni kero na unaona ni uchafu.
Na ukijilazimisha, jongoo halitapanda mtungi, kila litakapotaka kupanda litaishia kuteleza na kudondoka chini.