Wenzangu mnaombaje mpaka maombi yenu yanajibiwa?

Wenzangu mnaombaje mpaka maombi yenu yanajibiwa?

Habari ndugu zangu

Naomba kuelekezwa namna ya kuomba maombi yangu yakajibiwa,kama kusali nasali sana,kufunga nafunga sana,kutoa sadaka natoa ila maisha yangu yameandamwa na magonjwa ya ajabu,kutofanikiwa na kukosa kazi

Sasa wapi ninakosea au mimi sijui kuomba ndugu zangu,kwani ninyi mnafanyaje?

Asanteni
Mkuu wewe unaweza ukawa huwa husali ila ukawa unaimba sala ya baba yetu ile sio sala haitokusaidia kwa sababu huombi matatizo yako ila unaimba wimbo tuu........

Wewe omba kwa mungu wako sehemu isiyo na kelele na uombe ukimaanisha halafu jaribu kusaidia hata ombaomba wa mijini hiyo itakusaidia kuliko kufunga sana .

Nb: omba ukiamini kwamba unasikilizwa.........
 
Kama ni mtoa sadaka Kuna watu wengi wana mahitaji hivyo wape hao, Kwa kiasi kikubwa ni juhudi zako ndizo zitakazo kutoa mavumbini, yaani juhudi zenye akili, bila juhudi zenye akili basi hata ukeshe uombe Kwa nani kamwe huwezi kufanikiwa...Lazima uwe imara kiakili na kimwili, usiwe na roho mbaya, wivu, kijicho, husda, chuki...kubali kujifunza, jifanye mjinga kwenye vitu usivyojua, acha majivuno.

Be positive, amini Kuna siku kutokana na juhudi zako kubwa utafanikiwa, mafanikio unayotaka ni process siyo bu ba, ni mchakato wa muda mrefu unaohitaji nidhamu, uaminifu na ukomavu. Je mitazamo na midomo ya watu inakuathiri?, usiruhusu Hilo.

Boldness, ni jambo muhimu sana kwenye maamuzi kuhusu maisha yako.
 
Hata Muislamu atakwambia wewe, ipo siku utakuja kumkiri Allah kama Mnyaazi Mungu wa Maisha yetu.

Ulicho kifanya hapa ni kutetea imani yako ya huyo Yesu Kristo.

Kitu ambacho hata mtu wa imani nyingine atafanya hivyo hivyo.

Huyo Yesu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Yesu alikuwepo ila ni kama Mzee wa Upako, Mwamposa and the likes
 
Kuna kitu kinaitwa kipimo Cha maombi na hicho kipo kulingana na hoja Yako kama ni Kubwa Kuna kipimo chake kikifika maombi Yako yanajibiwa Sasa ilikukifikia jaribu kuwashirikisha waombaji wengine ili mjaze kipimo haraka
 
Si historia inasema mama yake alishika mimba akam'bambikia Yusuph? Na nadhani ndo source ya wanawake kutubambikia watoto....
Historia inaweza pia kuwa Historia ya Uongo.

Ndio maana hata kuna Vitabu vya Historia vinavyo eleza binadamu tumetokana na Sokwe.

Sasa ili tuhakikishe na kuthibitisha ukweli wa Historia yako, Lazima uthibitishe kwa vithibitisho na evidence zisizo na utata wala ulakini.
 
Habari ndugu zangu

Naomba kuelekezwa namna ya kuomba maombi yangu yakajibiwa,kama kusali nasali sana,kufunga nafunga sana,kutoa sadaka natoa ila maisha yangu yameandamwa na magonjwa ya ajabu,kutofanikiwa na kukosa kazi

Sasa wapi ninakosea au mimi sijui kuomba ndugu zangu,kwani ninyi mnafanyaje?

Asanteni
-Omba hadi upate majibu
Kuwa na consistency katika maombi
-Ambatamisha maombi na sadaka
-Amini katika unachokiomba na amini kwamba Mungu anajibu
-Jua nguvu ya Mungu,amini Mungu ni mkubwa kuliko tatizo lako.
-Tembea katika njia sahihi..Kwa ndani ya Mungu na weka Neno lake ndani yako
 
Pray
Pray
Just Pray...
Japo binafsi nikiwa katika deep shit huwa nashindwa kabisa kuomba...
Mungu akukumbuke
 
Huna imani, una manung'uniko,umebeba watu moyoni, Kuna vitu viovu hutaki kuacha. Imarisha Iman yako
Sio kweli, maombi wengi wanaomba hela afu hawafanyi kazi hata kama we ndio Mungu lazima u mute.
 
Unamuomba nani unapoteza muda kama unaumwa nenda hospital watajua unasumbuliwa na ugonjwa gani kuhusu kazi kwani unajishughulisha na kitu gani ili tujue
Vinginevyo unapoteza muda kuomba kinyago ulichokichonga mwenywe
Maisha yangekuwa maombi ingekuwa raha sana kusingekuwa na hosp watu wakiumwa wanaomba tu wanapona amka kifkra acha ujinga
 
Ssi hatuombo, tunapambania kwa vitendo hadi mambo yanakuwa

Habari ndugu zangu

Naomba kuelekezwa namna ya kuomba maombi yangu yakajibiwa,kama kusali nasali sana,kufunga nafunga sana,kutoa sadaka natoa ila maisha yangu yameandamwa na magonjwa ya ajabu,kutofanikiwa na kukosa kazi

Sasa wapi ninakosea au mimi sijui kuomba ndugu zangu,kwani ninyi mnafanyaje?

Asanteni

Mchungaji wako yeye anaomba ulete mwenzio waumumini muwe wengi kwa kisingizo kanisa linakuwa na sadaka zinaongezeka halafu anaenda kununua gari yard kwa pesa ila ww unapewa baraka.

Nikuulize baba paroko anafanya kazi kwenye ofisi gani KANISA, inamaana liziki yake anaipata wapi, na wateja wake ni nani, ni wewe, ww unafanyia kazi wapi, wateja wako ni akina nani
Sasa kwann unaenda kwann unaenda kwa baba paroko badala ya kwenda kazini upate hela ufanye yako maombi yawe yamejibiwa
 
Back
Top Bottom