Wewe mwanamke, kama una mwanaume asiyetumia pombe, mwogope sana huyo

Wewe mwanamke, kama una mwanaume asiyetumia pombe, mwogope sana huyo

Kilaji kinakufanya ujione unaongea madini tu, na unataka kila mtu asikilize unachoongea ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Noma sana mkuu, lakini nikigundua madogo wana enjoy sana nikiwapa simulizi wakati nikiwa nimepombeka...๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ
 
Noma sana mkuu, lakini nikigundua madogo wana enjoy sana nikiwapa simulizi wakati nikiwa nimepombeka...๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ
Kuna mwanangu huyo akilewa akiongea anataka umsikilize na kumuangalia. Endapo ukiangalia pembeni tu anaurejesha uso umuangalie...๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Unatusingizia mkuu we endelea na balimi zako tuu.

Kina Dada wala msisikilize na kumuamini huyu "mnywa pombe".
 
Mkuu Nakusalimu, kuhusu hoja yako nakujibu ifuatavyo:-

Pombe ni kiburudisho ambacho huleta starehe kwa mtumiaji kama ilivyo sigara au kahawa na vinginevyo (viburudisho uvijuavyo) lakini inatakiwa mnywaji aitawale (yaani anywe kwa kiwango chake), sasa basi binadamu wengi wanapenda starehe ikiwemo pombe lakini wanashindwa kuitawala hivyo kuwapelekea kwenye matatizo. Mitume na Manabii wa zamani baada ya kuona watu wao walio wengi hawawezi kuimudu pombe, kwa nia njema wakaamua kuwawekea makatazo ya kisheria ili wasiinywe kwa kuwambia kuwa ni dhambi (Dhambi hii ni kwa mujibu wa sheria zao na si amri ya MUNGU).

Sasa basi kuanzia leo naomba utambue kuwa kitendo cha kunywa pombe pekee siyo dhambi, bali dhambi ni matendo mabaya ambayo utayatenda baada ya kunywa kinywaji hicho. Pombe inatakiwa uitawale (uimudu) ikiwa huwezi kuimudu ni bora kuachana nayo kabisa.

Kwa taarifa yako wapo watu wanakunywa pombe toka utoto wao na wana maisha mazuri na mahusiano mazuri na watu kuzidi hata wasiokunywa pombe. Kinachotakiwa ni kujitambua na kujielewa tu.

Mwisho japo si kwa umuhimu nakushauri kuwa USICHOKIPENDA USIKITIE HILA.
Kwanza siyo "HILA" sahihi ni "ILA".

Nimeanzia chini nakuja juu. Kuna vitu kama hamvijui awla kuvikalia kimya, ulichokiandika kwanza huna ushahidi nacho kimaandishi.

Umewagusia mitume na manabii, nani amekwambia ya kuwa mitume wanajitungia sheria ?

Hakika huwezi kuwa na akili timamu ukaitetea Pombe, ndiyo maana huko juu nilitoa angalizo ya kuwa ukitafakari kwa kina tu achilia mbali kwenye maandiko ambayo yako wazi mno, ila akili inakiri ya kuwa Pombe ni dhambi.

Kadhalika hakuna mtu aliyesema ya kuwa wanywa Pombe hawaishi maisha mazuri, hili linaonyesha ni kwa namna gani Pombe inakufanya usiwe makini. Tunaongelea ya kuwa Pombe ni dhambi.

Hitimisho ni kuwa hujajibu hoja yangu zaidi ya kuonyesha ya kuwa mapenzi yako juu ya Pombe yamechukua nafasi ya akili yako na kushindwa kujibu hoja yangu, zaidi ya kutetea Pombs kichwa mchunga.

Ahsante, ukija uje na ushahidi unao onyesha ya kuwa hao mitume na manabii hizo sheria walizitunga wao au kuna sehemu walizipata ?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mkuu hujakaa na wanywa pombe tena ndo wanaoongoza kuliwa kimasihara.
 
"ILA" na "HILA" ni maneno mawili tofauti, yana maana tofauti na yanatumika sehemu tofauti (kwa hiyo sijakosea nina uhakika na ninalolisema)

Kuhusu mitume na manabii kutunga sheria pia nipo sahihi maana makatazo ya pombe yapo kwenye sheria ya Mussa maarufu kama Torati (Kiswahili), Taurat (Kiarabu) au Torrah (Kiebrania) hivyo yeye ndiye aliyekataza (ni dhambi kwa sheria ya Mussa siyo MUNGU)
na ukumbuke sisi hatuwajibiki kwa Mussa bali kwa MUNGU.

Unasema siwezi kuwa na akili timamu nikaitetea pombe (dhidi ya nani na nini!?). Pombe ni kitu kisicho na uhai ndani yake hivyo haiwezi kufanya chochote kwa kuwa haijitambui. Kazi ni kwa binadamu dhaifu wanaoinywa kisha wanafanya makosa na kuisingizia pombe. Nasisitiza kama pombe huiwezi bora uiache maana starehe zipo nyingi, kuhusu umakini ni kuwa mimi nipo makini na ndiyo maana nakujibu kwa utuo.

Hoja yako nimejibu ila kama hujaridhika waweza kuuliza tena, lakini hili ni jukwaa huru hivyo usilete hoja ukiwa na majibu yako kichwani halafu ukataka ujibiwe unavyopenda wewe.

Kuhusu "kichwa mchunga" sijakuelewa!!!
 
Hivi kuna combination inayokubali kama pombe na umalaya?

Labda ungesema kuhusu wavutaji, kidogo siyo sawa na wanywaji.
 
Huo uongo uliotukuka wewe kama ni mlevi hayo ndio maisha uliyoyachagua usidhani ni kila mtu ana mawazo kama yako wengine tumechagua fungu lililo jema. Nakusihi okoka njoo kwa yesu atakutua huo mzigo wa ulevi na kukuondolea hiyo kiu ya pombe.
 
"ILA" na "HILA" ni maneno mawili tofauti, yana maana tofauti na yanatumika sehemu tofauti (kwa hiyo sijakosea nina uhakika na ninalolisema)
Ukiwa unakosolewa kubali kukosolewa, unapo jitutumua ndoyo unazidi kukosea. Tamko "Hila" umeliweka sehemu ambayo si sahihi, na halileti maana iliyo kusudiwa.

Tamko "Ila" linaingia katika dhati ya kitu chenyewe na tamko "Hila" huwa kama tabia anayo sifika nayo mtu. Wewe umelitumia tamko "hila" kwa dhati ya kitu na si kama habari.
Kuhusu mitume na manabii kutunga sheria pia nipo sahihi maana makatazo ya pombe yapo kwenye sheria ya Mussa maarufu kama Torati (Kiswahili), Taurat (Kiarabu) au Torrah (Kiebrania) hivyo yeye ndiye aliyekataza (ni dhambi kwa sheria ya Mussa siyo MUNGU)
na ukumbuke sisi hatuwajibiki kwa Mussa bali kwa MUNGU.
Nithibitishie ya kuwa Musa alitunga sheria,acha kujitutumua kwa mambo usiyo yajua.

Niwekee matini ya andiko toka kwa nabii Musa akisema "Mimi nimekataza kadha... :.

Makatazo ya Pombe kuwepo katika vitabu vya Dini haimaanishi ya kuwa mamabii wametunga hizo sheria mpaka utupe ushahidi, na hili huliwezi mpaka unakufa.
Unasema siwezi kuwa na akili timamu nikaitetea pombe (dhidi ya nani na nini!?).
Dhidi ya UHALISIA. Mpaka unakufa,kutetea kwako kunathibitisha ya kuwa huna akili iliyo sawa, yaani una matatizo ya akili. Huwezi kuwa mzima na timamu wa akili kukitetea kitu ambacho kinakudhuru.
Pombe ni kitu kisicho na uhai ndani yake hivyo haiwezi kufanya chochote kwa kuwa haijitambui.
Nimecheka sana, inaonekana uko tungi maana unaandika ujinga,sasa hicho kisicho na uhai mbona kina kifanya ulewe na uburudike kama ulivyo kiri huko juu, maana yake kina athari unapo kinywa. Kijana acha Pombe, naona unaandika ujinga na hii ni athari ya pombe inayo thibitisha uhayawani wako.
Hoja yako nimejibu ila kama hujaridhika waweza kuuliza tena, lakini hili ni jukwaa huru hivyo usilete hoja ukiwa na majibu yako kichwani halafu ukataka ujibiwe unavyopenda wewe.
Hoja yangu huwezi kuijihi wala hutaweza kuijibi na ulichokiandika kimethibtisha hilo.
Kazi ni kwa binadamu dhaifu wanaoinywa kisha wanafanya makosa na kuisingizia pombe.
Kinachosababisha ulewe ukinywa pombe ni nini ? Sasa mbona jili dogo linakushinda kung'amua mzee, je hilo kubwa utaliweza kweli ?
Nasisitiza kama pombe huiwezi bora uiache maana starehe zipo nyingi, kuhusu umakini ni kuwa mimi nipo makini na ndiyo maana nakujibu kwa utuo.
Huo umakini uko wapi, kama unashindwa kutofautisha au kujua ya kuwa Pombe ina athari ?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mwanaume ambae hatumii pombe raha sana wakati mnatombana yaan unamuona kabisa anavyofeel K na mwili wa mwanamke yaan anakuwa realy
Sasa hawa wa walevi mpaka wanywe ndio wapate hamu,mpaka mtu abust na konyah ndio afeel mwanamke
๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Back
Top Bottom