Wewe ndio chanzo cha umasikini katika familia yenu

Wewe ndio chanzo cha umasikini katika familia yenu

Kama vipi wasingetuleta duniani. Watoto ni jukumu lako uliamua mwenyewe kuzaa.
Watoto wangu hawawezi kuwa chanzo cha umasikini wangu, ningetaka utajiri nisingewazaa.
Kwa mantiki hiyo, na wewe unaamua kabisa kuendeleza umasikini kwa kuongeza gharama za matumizi (watoto)
 
Mbna matajili Wana Mali za kutosha na hawana watoto na hao tuwaweke kweny kundi lipi jamani, kama mnasema umasikini unaletwa na watot
Kutokuwa na watoto (gharama) ndio kimewafanya wawe matajiri
 
Kwa mantiki hiyo, na wewe unaamua kabisa kuendeleza umasikini kwa kuongeza gharama za matumizi (watoto)
Wewe ndo una mtazamo huo.
Mimi kwangu watoto ni utajiri.

Tajiri na mali zake
Maskini na watoto wake.
 
Katika familia, gharama hazipo kwenye kuzaa tu; bali gharama zipo kwenye malezi.

Na kwa mazingira ya sasa, unaweza kuta kijana ana miaka zaidi ya 30, lakini bado anaishi kwao, huku akiendelea kuwapa mzigo mzito wazazi wake.

Kwa nini nasema wewe ndio chanzo cha umasikini wa kwenu; ni kwa sababu gharama zilizotumia kukuza au kukulea wewe, ni gharama kubwa ambazo wazazi wako wangewekeza kwenye ujenzi wa viwanda, tungekuwa na bidhaa nyingi huko nje ya nchi na tungepata fedha za kigeni.

Mfano:-

Chukulia kwa siku unatumia 10,000/=

Mwaka una siku 365

Kukaa kwa wazazi mpaka kujitegemea, chukulia miaka 30


Fedha/nguvu zilizotumika kwa wazazi = 10,000 x siku 365 x miaka 30

=109, 500,000/=

Hii ina maana, mtu mmoja mpaka aje aondoke kwa wazazi wake, atakuwa ametumia kiasi kisichopungua Tsh. 109,500, 000/=

Kama mmezaliwa saba (7), ina maana wazazi wenu mmewabebesha mzigo wenye thamani ya Tsh. 766,500,000/=; kwa hiyo kama wanaishi kwenye mazingira mabovu, kaa ukijua, chanzo chao cha umasikini ni wewe.

Ndio maana matajiri hawazai watoto wengi, sio kwamba wana akili sana, bali wanaepuka gharama hizo nilizoziainisha hapo juu.

Kwa hiyo, usiwalaumu wazazi wako, kwa sababu chanzo chao cha umasikini ni wewe.

Karibuni kwa hoja.​
Kwani ukifa, cha maana mtu anachoacha hapa duniani ni nini? Na anawaachia akina nani? Au unataka mali zako zirithiwe na watoto wa bamdogo?
 
Kwani ukifa, cha maana mtu anachoacha hapa duniani ni nini? Na anawaachia akina nani? Au unataka mali zako zirithiwe na watoto wa bamdogo?
Kuna ka formula, chagua watoto chagua mali; watoto wakiwa wengi mali chache, watoto wakiwa wachache mali nyingi; 1/y = x
 
Basi kama wanaona wanapata hasara wanirudishe walikonitoa, sikuwaomba nije huku duniani mimi.

Kwahiyo mimi ni wajibu wao mpaka umauti.
 
Sijasema uzae watoto wengi, bali mtu anapaswa kuzaa watoto anaowamudu..., na watoto wasiwe chanzo cha umasikini
Uko sahihi, swali ninalojiuliza, ukiingia forbes, utakuta matajiri wakubwa lakini utakuta ana mtoto mmoja au wawili; kwa nini inakuwa vile?
 
Nje ya mada

Wasomi wabongo ni waongo sana
Utasikia profesa anakufundisha,kijana nakufundisha ujuandae kujiajiri, kujiajiri kutakufanya uwe huru, wakati huohuo yeye kaajiriwa unamuangalia unajiuliza Ina maana huyu hapendi uhuru?
 
Back
Top Bottom