What are random interesting facts about yourself?

What are random interesting facts about yourself?

😌😌😌aisee wewe ni mimi kabisa. .

yaani unaishi ndani yangu
ila mimi nina ogopa ng'ombe
Ng'ombe nilikuwa namuogopa nilivyokuwa mdogo, nilianza kuwazoea taratibu hadi leo sina uoga nae. Simpendi Nyoka, sio kwamba namuogopa, wala sitakagi utani na hiko kiumbe tena ukitaka unichukie maisha yako yote. Niletee utani wa hiko kitu
 
.mkuuu apo kwenye kuona mahusiano ni kero kma tunalandana uwa nakinai mahusiano harak san sijui shida ni nn
Mimi wala hata sitaki kujua kama ni shida wala nini, ila kuna wadada huwa nikiwapenda, nawapenda kweli ila nikishampa mgongo kwa kuona kumpenda kwangu ni udhaifu, atapenda tu
 
Vyote mkuu, Yaani mvua yenye NGURUMO NA RADI daah iman inashuka inakuwa 0%, nanyong'onyea, nakuwa mdogo, nakuwa mkimyaaaa najjikatia tamaa.
Hapa kwenye Radi unanigusa mimi pia😅, wakati nipo mdogo nishashuhudia radi inachana mti kuwa mbao 😤since that day ile picha haitoki akilini, nikianza kusikia radi tu nalose confidence kabisa.
 
Nikiwa na miaka minne ilikuwa mitaa ya uswahilini flani hivi nilizama kwenye karo(shimo) la maji machafu ya choo kabisa.nikanywa vikombe kadhaa humo akaja bibi ambaye watu walikuwa wanamuogopa kuwa ni mchawi ndo alinitoa humo.sijui niliponaje ila namshukuru M/Mungu tu.
Kingine ambacho huwa nashindwa hata kuelezea nikaeleweka ni kuwa huwa nala ili niishi,yaani sienjoy chakula hata huwa naona hakuna tofauti kati ya kula wali au ugali,samaki au mchicha yani huwa nala ili tu chakula kingie tumboni.Muda mwingine kula huwa naona kama kupoteza muda tu.
 
Sijui hesabu.

Yaani sijui hesabu hata kutamka zile namba naona uvivu. Mfano humu kuna username zina namba zile namba hua sizitaji yaani mfano username ina jina castr123 mi natamka tu 'castr' bila hizo namba.

Damn.
Izo majina ya username waga unayatamka wapi?
 
Well kwa watu smart. Hili swali lako litawafanya watu wengi wa spill details zao binafsi bila wao kujua.
Details hizi zinaweza kuchukuliwa na watu au mtu .. ana akatengeneza character yako kupitia uliyo yasema.

Pia inaweza kutumika kumsoma muhusika na id yake.

So to me no thanks man. Ningeweza but it too risky kuweka character yangu on public.
Wewe kwa impact gani uliyonayo mapka unajiogopa Ivyo?
 
Simpendi kiumbe nyoka dizaini zote!.. Tena chatu anaeviringisha ukitaka uone mbaliga zangu nilione hilo dubwana chatu ila hawa wadogo wadogo napambana nao akiingia ndani ni ama mimi nile kona au yeye😅
Narudia tena chatu namuogopa maana kama hata simba tu akizubaa anamezwa je mimi mbavu mbili..?
Si bora nikimbie km 1 kwa sekunde ili niione kesho kuliko kujitia ununda kwa kupigana na chatu..😅

Nilishawahi kuzama kwenye mto bwawa tulikuwa tunaogelea wenzangu baada ya kuona huyu mtu ndo anaenda sasa wakanikimbia majinga Yale!!
Nilivyoona hapa ntakufa nilipiga mbizi si za nchi hii! Tokea hapo maji nayoyapenda ni ya kuoga na sio ya kuogelea..😂
Nilikunywa vikombe viwili vya ujazo na maji yalivyo yanakupeleka chini yanakurudisha juu na kwenye kurudi ndipo unapokunywa kikombe sasa..
Maji nakuheshimu nitabaki kuwa baharia wa nchi kavu tu karagabao..
 
😄😄😄😄 ndio usinicheke madame..ng'ombe na waogopa tena sana
Unaogopa wale wanaopiga? Au hata kama hapigi?
Kweli na ujanja wako wote ng'ombe anakukalisha chini?😂😂😂
 
Ngoja na mimi niandike.
Tangu darasa la 3 hadi la 5 nilikuwa "monitor".
Darasa la sita na la saba nilikuwa " Dada mkuu".

Form 1 na form 2 nilikuwa "Monitress" .
Form 3 nikawa kiongozi wa michezo na Monitress.
Form 4 nikawa kiongozi wa chakula na Monitress.

Five na six nilikuwa mweka hazina wa kikundi chetu cha dini.

Chuo nilikuwa CR miaka yote na Mbunge mwaka wa pili.

Kazini Mimi ni mwalimu wa nidhamu.
 
Unaogopa wale wanaopiga? Au hata kama hapigi?
Kweli na ujanja wako wote ng'ombe anakukalisha chini?😂😂😂
😄😄mimi namjuaje sasa anayepiga na asiyepiga. mimi naogopa wote tu
cause huwa naamini kuwa hatabiriki ule ukimya wake ni sawa na sleeping dog anytime anakugeukia
 
Back
Top Bottom