WHO: Corona Virus inaweza isiondoke
Wewe endelea kuishi nao hakuna tatizo maana kumbuka kuwa nyuki hapigwi busu
Shirika la afya duniani limekiri kupitia mkurugenzi wake mtendaji ( Executive director) kuwa ugonjwa huu wa corona haujulikana utaisha lini hivyo ni muhimu kujifunza kuishi nao

Rais Magufuli aliitoa kauli hii mapema kabisa akilihutubia Taifa la Tanzania kuwa tuondoe hofu na huu ugonjwa tutaishi nao kama magonjwa mengine

Tunampongeza kwa hilo

Hata hili la kufunga mji kuna siku tutakuja kumkubali hapa JF

Tupishane kwa hoja na sio kwa vyama

Video hii hapaView attachment 1451488

In God we Trust
 
Raisi wetu anaakili nyingi.
Kawa outsmart viongozi wengi Sana wa kidunia,
Napenda anavo jiamini na kuwapuuza waliotaka afuate nyendo zao.

Ukitaka kujua Raisi wetu ni genius
Fuatilia jinsi Rais Donald Trump anavoweweseka katika kufanya maamuzi juu ugonjwa huu.
 
Yaani kutwa mnapindisha kauli ili ionekane mzee yuko sawa au alikua sawa, mkuu kiufupi hali sio kama siku zote, hebu fikiria kwanza watoto wetu hawawezi kurudi shule, lakini huko kwa wazungu tayari wanarudi na wengine wanasomea online, hivi hawa utalingana nao?

Madereva wetu kila siku wanapatikana na ugonjwa huu mipakani na wengine nchi jirani, sijui wanaishia wapi? hivi ndio unataka tuonekane tuko sawa na wazungu?

juzi hapa wanataka kutoa muongozo wa mazishi ya covid, yaani ndio kwanza tunaazimia na sidhani kama umeshatolewa na kuanza kutumika, je bado tu unadhani hatua zinazochukiliwa na ziko sawa na wazungu au mataifa?
hata kama kauli zifanane je hatua za kuudhibiti huu ugonjwa zinafanana?

Kiufupi tuko nyuma sana kwa kila kitu, ni kama tumechelewa fulani hivi, maambukizo yanaweza kua mengi sana ila ni kwakua tunafichwa hii kitu, huku wakihubiri miti shamba ambayo kila siku inapigiwa promo!

Nchi nyingi duniani zinaaanza kukabiliana na maambukizo ya mara ya pili baada ya watu kuanza kulegeza mashariti, sisi hata ile inayoitwa awamu ya kwanza haifahamiki tumeimaliza au hatujaianza kabisa
hata hili unataka kauli ya mzee ifanane na ya mabeberu?
kututoa hofu ingekuja tu maana wanasaikolojia wasingeliacha lipite, kuna watu wana magonjwa ya kudumu, kuna makundi hatarishi, wote hawa wanahitaji mahubiri ya kuwato hofu kama tuavyoambiwa bongo
Na wamesema kabisa huu ugonjwa tutaendelea kuishi nao muda, maana haijulikani kinga itaanza kutumika lini

Mkuu mi naona nchi yetu bongo haina hela za kukabiliana na huu ugonjwa, na tusipindishe kauli za watu maarufu au mashirika zionekane ziko sawa ya mzee!
 
Shirika la afya duniani limekiri kupitia mkurugenzi wake mtendaji ( Executive director) kuwa ugonjwa huu wa corona haujulikana utaisha lini hivyo ni muhimu kujifunza kuishi nao

Rais Magufuli aliitoa kauli hii mapema kabisa akilihutubia Taifa la Tanzania kuwa tuondoe hofu na huu ugonjwa tutaishi nao kama magonjwa mengine

Tunampongeza kwa hilo

Hata hili la kufunga mji kuna siku tutakuja kumkubali hapa JF

Tupishane kwa hoja na sio kwa vyama

Video hii hapaView attachment 1451488
Wameona mwamba alishamwaga mabomu na wala hatoki na misimamo ya kujikomba!
 
Nitaamini tu pale akianza kutembea barabarani na Mikoba ya pesa na safari za kushitukiza ....Lini atatoka CHIMBO?
 
Tatizo kuu Kwa baadhi ya waTanzania na baadhi ya waAfrika na viongozi wengi ni utumwa wa kifikra, mpaka WHO (Mabeberu) waatafune ndipo wao humeza. Namheshimu Magufuli sababu jamaa anatafuna mwenyewe na kumeza, wengine wengi ama ni vibaraka au vilaza.
My president is Black and I will be got damn if brain ain’t too.
 
Yaani kutwa mnapindisha kauli ili ionekane mzee yuko sawa au alikua sawa, mkuu kiufupi hali sio kama siku zote, hebu fikiria kwanza watoto wetu hawawezi kurudi shule, lakini huko kwa wazungu tayari wanarudi na wengine wanasomea online, hivi hawa utalingana nao?

Madereva wetu kila siku wanapatikana na ugonjwa huu mipakani na wengine nchi jirani, sijui wanaishia wapi? hivi ndio unataka tuonekane tuko sawa na wazungu?

juzi hapa wanataka kutoa muongozo wa mazishi ya covid, yaani ndio kwanza tunaazimia na sidhani kama umeshatolewa na kuanza kutumika, je bado tu unadhani hatua zinazochukiliwa na ziko sawa na wazungu au mataifa?
hata kama kauli zifanane je hatua za kuudhibiti huu ugonjwa zinafanana?

Kiufupi tuko nyuma sana kwa kila kitu, ni kama tumechelewa fulani hivi, maambukizo yanaweza kua mengi sana ila ni kwakua tunafichwa hii kitu, huku wakihubiri miti shamba ambayo kila siku inapigiwa promo!

Nchi nyingi duniani zinaaanza kukabiliana na maambukizo ya mara ya pili baada ya watu kuanza kulegeza mashariti, sisi hata ile inayoitwa awamu ya kwanza haifahamiki tumeimaliza au hatujaianza kabisa
hata hili unataka kauli ya mzee ifanane na ya mabeberu?
kututoa hofu ingekuja tu maana wanasaikolojia wasingeliacha lipite, kuna watu wana magonjwa ya kudumu, kuna makundi hatarishi, wote hawa wanahitaji mahubiri ya kuwato hofu kama tuavyoambiwa bongo
Na wamesema kabisa huu ugonjwa tutaendelea kuishi nao muda, maana haijulikani kinga itaanza kutumika lini

Mkuu mi naona nchi yetu bongo haina hela za kukabiliana na huu ugonjwa, na tusipindishe kauli za watu maarufu au mashirika zionekane ziko sawa ya mzee!
Hapa tatizo sio serikali,Tatizo ni wewe binafsi

Shule ya kusoma mwanao online zipo nyingi sana na wanasoma na kutumiwa notes kupitia wazazi wao

Huu ugonjwa ni mpya kaka,Hata Marekani anahangaika sana

Wewe nani?una teknolojia kuliko Marekani?

Italia nchi bora ulaya kwenye afya wameshindwa,wewe nani?

Yakupasa kusifia pale Rais anapofanya vizuri

Sasa wewe mtoto wako hasomi utasifiwa?
 
Mtaani watu hawataki kabisa kuvaa Barakoa. Tahadhari zimepungua sana.

Bar zimefurika mno. Watu wamerudi kwenye track aisee.

Nilikuwa Moshi jana. Watu wanakula sana bata kienyeji tu kama kawaida.

Yaani kama malaria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu,

Hii inathibisha kuwa JPM mwenye upeo mkubwa sana na Tanzania sasa inaoongoza Africa na Dunia kuweka mustakabali wa masuala ya kiuchumi na kijamii.WHO na mataifa ya magharibi walilazimika kukubaliana na kauli ya JPM kuwa covid-19 itaendelea kuwepo hivyo lazima tujifunze kuishi nayo.

Sasa WHO imetoa taarifa kuwa kupiga dawa mitaani si njia sahihi ya kudhibiti Covid-19 kama ambavyo JPM alisema.Tumeshuhudia mataifa mbalimbali yakipiga dawa miji yao ili kuua virusi vya corona.

Sio kazi ndogo WHO kukiri mambo waliyoyaficha ili kutajirisha makampuni ya dawa ulimwenguni.
Screenshot_20200517-105450.jpeg
Screenshot_20200517-105458.jpeg
Screenshot_20200517-105515.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM bana yaani WHO mnawasikiliza na kuwaona wa maana Kama wakiendana na tamko la Magufuli, Ila wakitamka vingine Kama dawa ya Madagascar haijathibitishwa Kisayansi WHO wanakuwa ni mabeberu

Japo kwa msimamo binafsi naona WHO sio wa kuaminika 100%, muhimu ni kufanya utafiti wetu binafsi na kuona Kama huko kupulizia kunafanya kazi ama la, kwani ni simple experiment tu. mnaambukiza virusi kwenye surface mahali kisha mnahakikisha hiyo surface ina virusi kweli, then baadae mnapulizia kisha baada ya kupulizia mnapima Kama bado mtapata virusi, Kama experiment simple Kama hii inatushinda basi haina hata ya kufundisha Sayansi

Ya Nini kuwatumia Kama reference watu ambao tumeshasema hatuwaamini??

WHO hawa hawa si ndio walikuwa wamesema virus hivi haviambukizi kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine (no human to human transmission) japokuwa Kuna nchi zilisema vinaambukiza kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu

WHO hawa hawa wakasema Africa watakufa watu zaidi ya 300,0000, wakaja kubadili Tena wakasema 190,000, wakaja kubadili tena wakataja sijui ngapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom