Yaani kutwa mnapindisha kauli ili ionekane mzee yuko sawa au alikua sawa, mkuu kiufupi hali sio kama siku zote, hebu fikiria kwanza watoto wetu hawawezi kurudi shule, lakini huko kwa wazungu tayari wanarudi na wengine wanasomea online, hivi hawa utalingana nao?
Madereva wetu kila siku wanapatikana na ugonjwa huu mipakani na wengine nchi jirani, sijui wanaishia wapi? hivi ndio unataka tuonekane tuko sawa na wazungu?
juzi hapa wanataka kutoa muongozo wa mazishi ya covid, yaani ndio kwanza tunaazimia na sidhani kama umeshatolewa na kuanza kutumika, je bado tu unadhani hatua zinazochukiliwa na ziko sawa na wazungu au mataifa?
hata kama kauli zifanane je hatua za kuudhibiti huu ugonjwa zinafanana?
Kiufupi tuko nyuma sana kwa kila kitu, ni kama tumechelewa fulani hivi, maambukizo yanaweza kua mengi sana ila ni kwakua tunafichwa hii kitu, huku wakihubiri miti shamba ambayo kila siku inapigiwa promo!
Nchi nyingi duniani zinaaanza kukabiliana na maambukizo ya mara ya pili baada ya watu kuanza kulegeza mashariti, sisi hata ile inayoitwa awamu ya kwanza haifahamiki tumeimaliza au hatujaianza kabisa
hata hili unataka kauli ya mzee ifanane na ya mabeberu?
kututoa hofu ingekuja tu maana wanasaikolojia wasingeliacha lipite, kuna watu wana magonjwa ya kudumu, kuna makundi hatarishi, wote hawa wanahitaji mahubiri ya kuwato hofu kama tuavyoambiwa bongo
Na wamesema kabisa huu ugonjwa tutaendelea kuishi nao muda, maana haijulikani kinga itaanza kutumika lini
Mkuu mi naona nchi yetu bongo haina hela za kukabiliana na huu ugonjwa, na tusipindishe kauli za watu maarufu au mashirika zionekane ziko sawa ya mzee!