Who is INDO Power Solutions na ni nani Bw. Brian Mutembei?

Naishia hapa kwa leo.
Ingekua vizuri ukafanya juhudi ukauona huo mkataba
Kulikua na kabudi,mwanasheria mkuu na naibu waziri kilimo
kenya iliwakilishwana balozi Danny kazungu
Kwa sisi tunaoijua biashara ya korosho,ni wazi kuwa wanunuzi kadhaa wameweka pesa kwenye kapu wakaituma hiyo kampuni inunue kwa niaba yao,baada ya kutolewa mkuku na magufuli
Hapa cha muhimu korosho imeuzwa tena kwa bei ya juu kuliko mwanzo
 
Naomba kusaidia kidogo. Kwa mujibu wa hilo Tangazo la mirathi, Alice Wanjiku Karanja ndiye marehemu, the deceased na mali yake ndio inasimamiwa na Joyce Waithira Gatoho Muigai. Msiba umetokea 1986, kesi ya usimamizi wa mirathi imefunguliwa 2001. Jina la Marehemu ni Alice Wanjiku Karanja na kampuni imesajiliwa mwezi June 2016 share holders wakiwa Joyce Waithira Gatoho Muigai na Alice Wanjiku Gatoho, hivyo kisheria jina la Alice Wanjiku Karanja is not necessary Alice Wanjiku Gatoho, sometimes ni majina tuu kufanana mfano Rais wa kwanza wa Zanzibar ni Abedi Amani Karume, mkewe ni Fatma Karume, mtoto wa Abedi Amani Karume ni Amani Abedi Karume na binti yake ni Fatma Karume. Kampuni ikisajiliwa leo kwa jina la Fatma Karume is not necessary Fatma Karume mke wa Abedi Amani Karume bali ni Fatma Karume binti wa Amani Abedi Karume ambaye ni mjukuu wa Abedi Amani Karume. Mke wa Karume ni Fatma Karume na Mjukuu wa Karume ni Fatma Karume, ndio maana kisheria majina huwa ni matatu, yasipo fanana, is not necessarily is the same person no matter majina yanafanana vipi!.
P.
 
Julius Nyerere mtoto wa Burito na Julius Nyerere mtoto wa Makongoro Nyerere
 
Inafikirisha sana kuona kampuni kama ya INDO power solutions inajishughulisha na ununuzi wa korosho badala ya kutumia muda mwingi kutafuta vyanzo na masoko ya mafuta na nishati.
 
Kwa hiyo Mutembei ni Tanzanian citizen?
Je owners ni akina nani?
 
Nasubiri waje kukanusha. Wajiandae kuja na nyaraka zinazoonyesha kampuni tofauti na yenye uzoefu katika Sekta hii kama si Richmond nyingine
Mkuu mimi sijui kabisa kuhusu biashara ya korosho. Waweza nisaidia kujua ni kwa namna gani hapa kunaweza kuwa na utapeli wakati hawa jamaa wanalipa cash/upfront? Issue kama hiyo kampuni ina uzoefu na ununuzi wa korosho au kuna matatizo katika uhalali wa shareholders wake inatuhusu nini au itatuathiri vipi sisi kama wauzaji? Naomba shule kuhusu hayo mkuu
 
Hii ni zaidi ya aibu (if it is true) kwa jamuhuri kuingizwa mkenge mchana kweupee.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mke wa Karume ni Fatma Karume na Mjukuu wa Karume ni Fatma Karume

Kwa maneno mengine: Mjukuu wa Fatma Karume, (ambaye ni mke wa marehemu Abeid Karume) ni Fatma Karume, ambaye ni mtoto wa Abeid Aman Karume..

Ninakubaliana nawe kwamba Ex Spy hapa kakosea, aliyefariki sio Alice Wanjiku Gatoho aliyeko kwenye hiyo kampuni, bali ni Alice Wanjiku Karanga ndie marehemu. Lakini hili haliondoi uhalali wa mengine aliyoyaweka katika mchango wake hapa.

Ninasikitika tu kwamba mjadala huu unaelekea kufifia na kuelekea kwenye 'archive'. Sina shaka kuna siku utaibuliwa huko na kurudi hapa ukumbini kama kielelezo cha yale tutakayokuwa tunayashuhudia baada ya biashara hii ya ajabu iliyofanyika wakati huu wa sasa. Na ninakubaliana na Ex Spy kwa kusikitikia upepo ulioikumba idara ya usalama katika majukumu yake ya siku hizi.

Nashukuru sana kuwasoma watu kama Ex Spy; Mkirindi; Bungua na wengine waliotoa somo tosha kabisa juu ya 'koroshow' hii.
 
Tz inaathirika vipi kama hiyo kampuni haina uzoefu au ni madalali? Sisi cha muhimu pesa imeingia mzigo ukatoka, tunataka sasa kuwa viranja wa matepeli duniani au wafanyabiashara?
 
Tz inaathirika vipi kama hiyo kampuni haina uzoefu au ni madalali? Sisi cha muhimu pesa imeingia mzigo ukatoka, tunataka sasa kuwa viranja wa matepeli duniani au wafanyabiashara?
Kama Biashara inafanyika Na yeyote(KANGOMBA/MATAPELI wakiwepo) kulikuwa Nashida gani kuwabana mwanzoni ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda serikali ya tz haijafanya due dilligence nzuri. Kenya kuna Phd za utapeli na ufisadi. Singa wa iptl alitumika na hao phd kupiga dili la kuliza taifa kenya lakini akaja au kuletwa tz akatupiga iptl. Wakenya watatupokonya tena pesa nyingi kwa robbery wahusika na mauzo ya hizo korosho please vuteni pumzi kutafakari.
 

Hapo kwenye kufa aliekufa ni wanjiku mwengine ila huyu wanjiku share holder yeye ni lawyer aliefungua shauri la kusimamia mirathi.
Hivyo hapo point yako sio kweli


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Lakini, kinachoshangaza kidogo hapa ni kuwa pamoja na uchanga wa kampuni hii; Joyce anayedaiwa kuwa shareholder ni marehemu kitambo sana

mkuu kulingana na maelezo ya kwenye picha aliyefariki sio Joyce hebu pitia tena kwa umakini post yako
 
Hiv Hivi kuwa mchawi wa taifa lako unalipwa tsh ngapi haswa.. M
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…