WHO wathibitisha pombe ni sumu. Sasa nina ujasiri wa kusema: "kunywa pombe bila kulewa ni dhambi."

Kila siku nasema huku,wanywa soda mn wivu sana!
Alafu mna umbea umbea sana
 
Mbona wahubiri wanasema Bwana Yesu alishitua kidogo kwenye harusi ya Kana
Hao waliokuambia hivyo ni wahubiri feki, mkuu. Soma mwenyewe habari ya arusi ya Kana. Imeandikwa katika kitabu cha Yohana 2:1-11. Yesu aligeuza maji kuwa divai njema. Kumbuka arusini watu hawashtui. Wanakunywa sana. Sasa kama divai aliyotengeneza ingekuwa inalevya, watu wangeondoka arusini wamelewa. Hivyo ingekuwa anajipinga: atengeneze kileo halafu aseme walevi mbinguni hawaingii. No. Ile ilikuwa divai tamu sawa na fresh juice ya zabibu.
 
Soda? Fanta orange je?
  • Hizi ndio hatari zaidi, Ugonjwa wa Kisukari bila shaka unaufahamu.
  • Kama unapenda afya yako: Maji na matunda halisi ndio vinafaa, Na sio hizo kemikali toka viwandani..
 
Usiweke mistari nusunusu kuogopesha watu andika mstari mzima hiyo Habakuki 2:15 Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
 
  • Hizi ndio hatari zaidi, Ugonjwa wa Kisukari bila shaka unaufahamu.
  • Kama unapenda afya yako: Maji na matunda halisi ndio vinafaa, Na sio hizo kemikali toka viwandani..
Ni kweli mkuu. Bora bia mbili kwa siku na maji makubwa na matunda ya kutosha.
 
1 Tim 5:23
Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.
Unapingana na Biblia?
Andiko hilo wanalitumia sana wanaotetea unywaji wa pombe. Je, ni kweli kwamba Paulo alihalalisha pombe kwa kumwambia Timotheo anywe? Jibu ni "hapana"

Context ya andiko hilo haitoi ruhusa ya kunywa pombe kwa raha au kwa burudani. Badala yake ule ulikuwa ushauri wa kitabibu, sio wa kijamii. Wakati huo, maji mengi hayakuwa safi. Watu walikumbwa na magonjwa ya tumbo mara kwa mara. Hivyo mvinyo (wine) ulitumika mara nyingi kama antiseptic, kusaidia kuua vimelea. Hivyo Paulo alikuwa anampa Timotheo ushauri wa kiafya, sio wa burudani.

Twende deep zaidi: Je, “Mvinyo” unaotajwa katika Biblia ni sawa na pombe ya leo? Sio sawa. Neno la Kigiriki lililotumika kwenye andiko ulilonukuu wewe ni "oinos", hilo linamaanisha ama juisi mpya ya zabibu (fresh grape juice), au vinywaji vyenye kiwango cha chini sana cha kilevi (low-fermented).

Pombe ya kisasa ni strongly fermented (imechacha kwa kiwango kikubwa sana), na mara nyingi inaongezewa ethanol kwa viwango vya juu, sio sawa na mvinyo wa wakati wa Biblia.

Paulo angekuwa amehalalisha kunywa pombe asingesema tusilewe kwa mvinyo.
Waefeso 5:18
“Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho.”
Andiko hilo linaonyesha wazi ndani ya mvinyo kuna ufisadi.
Mtu akiishakunywa macho yake yanaona mauzauza, na kinywa chake kinaanza kusema mambo yaliyopotoka. (Methali 23:33)

Methali 20:1
“Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima..”

Umenipata, mkuu?
 
Ss wanywaji wa pombe wanywee nn kupata burudaniiii kamili....
Burudani ya kweli haiji kwa kunywa pombe. Pombe inatoa furaha ya muda tu lakini inamuachia mtu maumivu na kumharibia mwili. Ukiokoka, unapata burudani kamili katika uwepo wa Mungu. Ndani ya Yesu hakuna hangover 🙂
 
Asante kwa taarifa
 
Yoshua bin sira 31:27
Pombe ni kama uhai kwa mtu ukinywa kwa kiasi.
Maisha yafaa nini bila pombe?
Imeumbwa iwafurahishe watu.
28Kunywa pombe wakati wake na kwa kiasi,
kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni.
29Lakini kunywa pombe kupita kiasi,
kunaleta kuumwa kichwa, uchungu na fedheha.
 
Hata dawa ni sumu,
 
ukitoka hapo hamia kwenye sex …
Duh, unamshauri aruke majivu akanyage moto?
Dhambi ya uzinzi haina hata mjadala
1 Kor 6:9
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti
 
Bibilia inajipinga yenyewe, kama ilivyo Kuruani.
Biblia haijipingi. Unatakiwa uisome kwa kuzingatia context. Habari ya Paulo kumwambia Timotheo anywe mvinyo nimeishaifafanua. Soma reply.
 
Uliona wapi wewe mtu aliyekula mihogo na kisamvu akili yake ikabadilika akaanza kuona mauzauza na kutukana wakwe? Uliona wapi wewe aliyekula ugali na samaki akitembea kwa kuyumbayumba? Lakini mnywaji wa pombe, ONA mpaka anachekwa!
 

And you think you can liv forever...walokole mna majanga sana 😂 😂 😂 😂 . Utakufa na kitu unachoona hakikuhusu, sijui utamwambia nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…