Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 11,717
- 13,443
Bibilia na Quruan zina contradictions nyingi mno, hata ukizingatia context.Biblia haijipingi. Unatakiwa uisome kwa kuzingatia context. Habari ya Paulo kumwambia Timotheo anywe mvinyo nimeishaifafanua. Soma reply.
Sijakataza mimi. Aliyekataza ni Mungu aliyetuumba. Ndio sababu nimeweka MaandikoSasa ww unakataza tusinywe. na sio kusema tunywe kwa tahadhali.
Kwani maendeleo ya nchi ni lazima yaletwe na pombe? Mbona kuna nchi pombe imepigwa marufuku kabisa lakini wako juu kiuchumi? Saudi Arabia ni moja ya nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani lakini pombe huko imepigwa marufuku.Unatusimanga sana wakat tunachangia maendeleo ya nchi kwa kulipa kodi...
Ukisema hivyo hata wauza bangi wanaweza kusema wana familia zinazotegemea kula kutokana na mapato ya kuuza bangi na madawa ya kulevya. Hao wanaotegemea pesa za viwanda vya kuuza pombe, wakiwa na nia kweli ya kuacha, Mungu anaweza kuwapa kazi nzuri zaidi za kuwaingizia kipatoUnajua wafanya kaz wa hivi viwanda na wamiliki na wauzaji wa pombe wanafamilia pia au wanategemea kaz hii hii ya kuuza bia.
min -me bro. tunasengenywa sana aisee
Mimi sijasema kiwanda kifungwe. Usinilishe maneno. Ukiacha wewe kufanya kazi kwenye kiwanda cha sigara au pombe, Atheists watafurahi, wataenda ku-replace nafasi yako.Ni sawa useme kiwanda cha Sigara kifungwe wakati huo kimeajiri maelfu ya watu na wao waanafanya kazi na kuendesha familia kwa kazi hio hio ya kutengeneza stimulating materials
Duh, chanzo cha magonjwa ni dhambi iliyotendwa na Adam na Hawa. Mungu alipoiumba dunia haikuwa na magonjwa kabisa. Na Yesu alisema anaenda kutuandalia makao. Makao hayo hayatakuwa na magonjwa tena. Lakini ili tuingie kwenye makao hayo mapya ni lazima tuzingatie aliyoyaagiza. Mojawapo ya maagizo yake ni hilo la kujitenga na unywaji wa pombe na uleviHata kuzaliwa na kuishi ni chanzo cha magonjwa na vifo. Kwa kifupi tatizo ni mwili
Unafikiri kwa unywaji wake huo, sasa hivi babu yako yuko wapi. Mbinguni au motoni?Hatukatai pombe ni mbaya.
Sio pombe tu. kuna sigara. utumiaji sa Sukar na wanga kupita kiasi nk nk.
Ila pia wapo wanaokunywa pombe na wamefikisha miaka 90. babu yangu amefariki akiwa na miaka 105.
Kila weekend lazima umkute bar bad alipofika miaka 80 ndio kaacha na alikuwa analetewa bia had kitandani.
Kila kitu ukitumia kistaarabu madhara yanapungua.
Narudia tena. kila kitu ukitumia kistaarabu madhara yanapungua au yanakuwa hayapo.
Safi kabisa.Katika uislamu pombe ni haramu kabisa kunywa,kuuza,kusafirisha,kutengeneza,kuwauzia wengine,kupangisha nyumba yako,iuzwe pombe.Kwa hiyo Mtume Muhammad, aligundua ubaya wa Pombe,miaka
Karibia 1500 iliyopita,kabla hata wanasayansi wa sasa kugundua.
Aisee, unashauri kila mtu achague sumu yake? Hapana, mie nimemchagua Yesu wangu — nipate uzima!Hata soda ni sumu so kila mtu achague sumu yake ajifie taratibu. Waiter Lete safari ya baridiiiiiiiii
Ndo ukufe na yesu wako, watakao kufa kwa sumu ya pombe na soda na wao watakuwa wamefanya uchaguzi wao. By the way kifo ni kifo tu who cares.Aisee, unashauri kila mtu achague sumu yake? Hapana, mie nimemchagua Yesu wangu — nipate uzima!
Haya, safiri salama, lakini nakutahadharisha: hiyo "Safari ya baridiii" inakupeleka kwenye "shimo lenye motooooo."
1 Kor 6:9-11
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi."
Ni kweli sio wote wanaouguza ini au figo ni walevi. Lakini pombe bado ni sababu kubwa ya magonjwa hayo, na mara nyingi huongeza hatari hata kwa asiye na tatizo. Biblia haitukatazi pombe kwa sababu ni chanzo pekee cha maradhi, bali kwa sababu ‘ina ufisadi’ (Waefeso 5:18), inaharibu maamuzi ya mtu, na kumtoa kwenye utakatifu wa kweli. Kwa hiyo, hoja sio magonjwa tu, ni kutunza hekalu la Mungu (1 Wakorintho 6:19–20). Right?Hivi wanaouguza figo na ini ni walevi tu?
Sawa. Uchaguzi ni wako, mkuu. Mimi nikifa kabla yako naenda kupumzika. Kama wewe kwa pombez hizo unafikiri utawakuta totoz jehanam, songa mbele, utaukumbuka uzi huu.Mijagamaster kama kawa,mi seafoods,totoz kwa kwenda mbele,we usinywe na cha ajabu ukatangulia kufa kabla yangu.
Duh, miaka 123 tu umeona mingi?Babu yangu kafa mwaka juzi na miaka 123 na alikuwa mnywaji tena wa vitu vikali balaa
Pole sana unataka usizeeke? Hilo haliwezekani. Mungu aliishasema kila mtu lazima afe. Na uzee ni ishara ya kuondoka duniani.Hiyo sayansi yenu peleka kule,mbona imeshindwa tu kuzuia uzee achana na kuipata dawa ya ukimwi,fumbaf
Duh, kweli kama alivyosema Smart911 wanadamu siku hizi ni wabishi sana.Mambo yapo wazi acha kurukaruka vifungu. Yohana alikula nzige na asali tu wakasema anapepo. Yesu anakula na kunywa wakasema mlafi na mlevi( maana alikuwa anatumia hicho kinywaji kinacho levya na kula misosi mbalimbali) na kushinda na makahaba na watoza ushuri( walioonekana wadhambi) ndio maana hakukanusha hayo. Mantiki yake ni kukemea unafiki. Wanataka awe kama Yohana ambaye nayeye walimshutumu anapepo.
Ukweli ni kwamba Yesu alikula, alikunywa mvinyo, alishinda na makahaba(M. Magdalene) na watoza ushuri (Akina zakayo). Na si kwamba walimsingizia ni fundisho mpya anatoa.
Usitumie pombe Kwa discipline yako binafsi ni nzuri. Ila si dhambi katu. Hiyo ni swala la self discipline tu.
Mimi kilevi changu warembo. Wewe ni mrembo ?Jamani Kipangaspecial
mbona hujatoa maoni yako? Utaendelea na kilauri au utaacha?
Yesu hakuwa mlafi, hakuwa mlevi Wala hakutenda dhambi. Ila Yesu alikula, alikunywa mvinyo, alishinda na wenye dhambi.Duh, kweli kama alivyosema Smart911 wanadamu siku hizi ni wabishi sana.
Ni kweli Yesu alikula na kunywa, na ni kweli alishinda na watoza ushuru na wanawake waliodhaniwa kuwa wenye dhambi. Lakini Yesu hakufanya hivyo ili afanane nao, bali awalete kwenye toba.
Mathayo 9:13
‘Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.’
Yesu hakuwahi kulewa, wala kuhalalisha ulevi. Kuitwa ‘mlevi’ haimaanishi alikuwa mlevi. Hiyo ilikuwa ni kashfa ya wanafiki, kama walivyosema Yohana ana pepo (Mathayo 11:18-19). Yohana hakuwa na pepo. Tangu lini mtu mwenye pepo akabatiza watu?
Yesu hakuwa mlafi, hakuwa mlevi, hakuwa mchafu, bali mwenye rehema.
Samahani sana MoroGent kama mada imekukera. Lengo langu sio kuwakera watu bali kuwasaidia wasiende motoni. Ukweli ni huu: Sayansi na Biblia havipingani. Vyote vimekiri kwamba pombe ni sumu. WHO (2023) ilisema wazi: ‘There is no safe amount of alcohol use.’ Na Biblia ilitoa kauli kama hiyo miaka zaidi ya 3,000 iliyopita:Ulianza na Sayansi vizuri, ila ukaharibu ulipoaanza kutaja vifungu vya Kitabu na kuhusianisha na Mungu. Mm nimesoma mpk apo WHO 2023 There is no safe amount.......
Chagua kama ni sayansi au ni Mungu, tupe product moja.
Umenikera sana kiukweli kubadilisha mada feom science to God scripture