WHO wathibitisha pombe ni sumu. Sasa nina ujasiri wa kusema: "kunywa pombe bila kulewa ni dhambi."

Ni sumu lakini haizidi ndoa
 
Yesu alikuja kwa ajili ya hao pia ili kuwapata ilibidi achanganyikane asiwatenge kama tunavyofanya sisi.Ila najua kitu kimoja baada ya kuwapata hao wanywaji hawakuendelea kunywa tena kwa sababu waliijua Kweli.Tunaokunywa sasa hatuijui kweli kwamba pombe ni mlango wa mapepo ndani ya roho zetu.
 
Usisahau kutia barafu.
Tangu lini barafu ikaondoa sumu?
Duh, poleni sana wanywaji, mna mahangaiko mengi.
Ila tuwashukuru WHO wametusaidia kuujua ukweli.
 
Haya mambo yanakanganya sana, Mitindo yetu ya maisha na lifestyle sijui kama itatuacha salama, imagine mtu asiyekunywa pombe anabugia energy, soda, anakula mafuta Kila siku,anatumia simu muda mrefu, anaendesha chombo Cha moto muda mrefu etc. what's negative effects of those?? Tuombe mwisho mwema Adam na Hawa walitukaanga, akhera inacombine mambo mengiii.
 
Siku ya tatu kulikuwa na harusi katika mji wa Kana ulioko Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo 2 na Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa pia. 3 Divai ilipowaishia, mama yake Yesu alimwambia, “Hawana divai.” 4 Yesu akamjibu, “Mama, mbona unanihusisha kwenye jambo hili? Wakati wangu bado haujafika.” 5 Mama yake akawaambia watumishi, “Lo lote atakalowaambia, fanyeni. ” 6 Basi ilikuwapo hapo mitungi sita ya kuwekea maji ya kunawa, kufuatana na desturi ya Wayahudi ya kutawadha. Kila mtungi ungeweza kujazwa kwa madebe sita au saba ya maji. 7 Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Wakaijaza mpaka juu. 8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni maji kidogo mumpelekee mkuu wa sherehe.” Wakachota, wakampelekea. 9 Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yame geuka kuwa divai. Hakujua divai hiyo imetoka wapi ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu. Basi akamwita bwana harusi kando 10 akamwambia, “Watu wote huwapa wageni divai nzuri kwanza kisha wakianza kutosheka huwaletea divai hafifu.
Imekuwaje wewe ukaiweka divai nzuri mpaka sasa?”
11 Hii ilikuwa ishara ya kwanza aliyofanya Yesu. Muujiza huu ulifanyika katika mji wa Kana huko Galilaya, ambako Yesu alidhi hirisha utukufu wake, na wanafunzi wake wakamwamini.

Ina maana unasema Yesu aliwapa watu sumu? kama Yesu alijua pombe ni sumu kwanini aliwapa watu kwenye karamu? Setfree
 
Pombe si sawa sawa na ulevi.

Matumizi ya dutu yoyote kinyume na inavyotakiwa ni sumu/hatari.

Biblia inakataza matumizi yasiotakiwa ya dutu mbalimbali ikiwemo pombe.

Ukisema pombe ni sumu unakinzana na maumbile (biology)kuwa kwenye damu kuna kiwango maalimu cha pombe.
 
100 others Inaonekana hujasoma replies zangu zote, maana comment kama hii nimeishaijibu. Anyway, ngoja nikusaidie:

Yesu hakuwapa watu sumu. Nashukuru ume-bold hiyo sentensi yenye maneno "divai nzuri"

Kinywaji chenye sumu kinaweza kuitwa kizuri? Yesu alitengeneza divai njema/nzuri, siyo ile iliyochacha

Neno ‘divai’ katika Biblia linatumika kwa maana pana: Wakati mwingine linamaanisha juisi safi ya zabibu (Isaya 65:8). Na wakati mwingine ni divai yenye kilevi iliyochacha (fermented). Hivyo ukisoma maandiko yenye neno divai, inabidi usome kwa muktadha.

Yesu alikuja kuleta uzima, iweje tena awanyweshe watu kinywaji chenye sumu ya kuharibu ini na ubongo?

Kumbuka pia wakati wa arusi watu wanakunywa sana. Sasa kama divai ile ingekuwa na kilevi, ni wazi wangelewa. Hivyo Yesu asingetengeneza kinywaji cha kuwafanya watu walewe halafu aseme walevi hawataingia mbinguni.

1 Kor 6:9-10
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.
 
Dah, kujieleza nayo ni shule. Sijaelewa comment yako inaelekea wapi.
 
Dah, kujieleza nayo ni shule. Sijaelewa comment yako inaelekea wapi.
Kuna tofauti ya pombe na ulevi kama ambavyo kuna tofauti ya matumizi yanayotakiwa/ustawi na matumizi yasiyotakiwa/uharibifu, sumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…