WHO yaitaka Afrika kujiandaa na usambazaji wa chanjo ya corona

WHO yaitaka Afrika kujiandaa na usambazaji wa chanjo ya corona

Ndugu, sijui uko upande gani wa dunia. Hivi unakumbuka BBC na radio za huko ulaya zimekua zikitangaza kuwa watu weusi na wahindi ndio waathirika wakubwa wa corona??
Mambo ya ajabu sana, kwa huku Afrika, nchi zenye asilimia kubwa ya weupe ndio ziliathirika, hata sijui walikuwa wanaongea upuuzi gani hao BBC 😂😂
 
Majaribio ya chanjo yanayofanyika ulaya na Marekani ni placebo tu, ila majaribio halisi huwa yanafanuika Afrika, tafuta maana ya neno placebo
Wewe ndiyo nikuambia utafute maana ya placebo! Daa basi ngoja nikupe somo: Moja ya chanjo ya covid ilihusisha watu 30,000. Nusu walipewa dawa ya chanjo halisi na nusu walipewa placebo i.e. boya a.ka. maji special tu yasiyo na dawa yoyote. Wakati wanawachanja watu waliyojitolea huwa anayechanja na anayechanjwa hafahamu ipi ni dawa halisi na ipi ni placebo ila kila chupa inakuwa na searial namba ambazo mtengenezaji ataweza kutambua baadae ni yupi alichanjwa kwa dawa halisi na yupi alipewa boya. Kwa nini wanafanya hivi? Unajua maana ya placebo effect kwa kuanzia? Bila shaka unajua kwa sababu ni wewe umenidharau na kuniona sijui kitu
 
Broken english is not an issue for Africans. Only an idiot can mind about it. Even Mzungus they do speak broken english mkuu!
It is an issue when the whole meaning of the sentence changes! Yeye Magu alisema ''Mr president I am trying to preech, but I cannot reach you...'' akiwa anamaanisha ''najaribu kufanya mahubiri lakini siwezi kukufikia (kiwango chako). Ukimwambia hivi mtu asiyejua kiswahili atadhani unamwambia ''siwezi kukufikia (kukushika, au kwa simu nk.) Kwa kifupi mzee wa Phd alitafsiri neno kwa neno kama zile enzi za watu wanasema ''one coconut'' wakimaanisha Mnazi mmoja.
 
Wewe ndiyo nikuambia utafute maana ya placebo! Daa basi ngoja nikupe somo: Moja ya chanjo ya covid ilihusisha watu 30,000. Nusu walipewa dawa ya chanjo halisi na nusu walipewa placebo i.e. boya a.ka. maji special tu yasiyo na dawa yoyote. Wakati wanawachanja watu waliyojitolea huwa anayechanja na anayechanjwa hafahamu ipi ni dawa halisi na ipi ni placebo ila kila chupa inakuwa na searial namba ambazo mtengenezaji ataweza kutambua baadae ni yupi alichanjwa kwa dawa halisi na yupi alipewa boya. Kwa nini wanafanya hivi? Unajua maana ya placebo effect kwa kuanzia? Bila shaka unajua kwa sababu ni wewe umenidharau na kuniona sijui kitu
Hiyo ni nusu yao, mimi nazungumzia wote 100% wanapewa chanjo hewa (maji kama ulivyoita) bila wao au hata sisi waAfrika kujua ili tuone kwamba mbona hata wao wanapewa hii chanjo ili tusishtuke, lakini ukweli ni kwamba wao wanapewa 100% placebo (sio nusu yao) kama kanyaboya tu la kutuzuga, wakati sisi huku ndio tunapogwa majaribio halisi kabisa, hilo hata wale wanasayansi wa kifaransa walilisesemamtena live kwenye kituo cha television, tafuta hiyo video ya ‘french scientists’ youtube uone!
 
Ebu waitumie wao kwanza wapone, siyo kutuletea waone kama yafaa au lah..tena tujihadhari hawakawii kuweka mambo ya ajabu kwenye hizo chanjo, HATUWAAMINI HAWA WENZETU KABISA KABISA..
 
Unajihami bure tu. Chanjo inaanzia Ulaya na Marekani na Afrika itakuja baadae sana. Na hata ikija sidhani kama watalazimisha watu kuchoma. Kuchoma ni hiari. Ulaya na Marekani hii chanjo ni muhimu sana kwani population yao ina wazee wengi. BTW unaweza usiwe unajua kuwa Ulaya na Marekani kila mwaka watu wanapata chanjo ya flu! Yes, hii kitu kama hujatoka nje ya Afrika na siyo mdadisi huwezi kujua kuwa mafua kila mwaka yanaua watu kwenye hizo nchi na kila mwaka kunawaga na chanjo hasa kwa wazee! Hivyo jambo la chanjo siyo kitu kigeni kama unavyodhani na kama wewe hutaki hakuna atakayekulamisha.

Kikubwa iwe hiyari, kusiwepo restrictions zozote. Anayetaka kuchanja achanje, asiyetaka matakwa yake yaheshimiwe as long as ni mwili wake. Tunasisitiza free will kwenye uchanjaji.
 
Shirika la Afya Ulimwenguni-WHO, Alhamisi limezisihi nchi za Afrika kuandaa mipango ya kusambaza chanjo za COVID-19 kadri zitakavyopatikana.

Utafiti mpya wa WHO uligundua kuwa nchi nyingi za Kiafrika haziko tayari kwa kile kitakachokuwa harakati kubwa zaidi ya chanjo barani humo.

Kupanga na kuandaa mikakati kutafanikisha au kuharibu shughuli hii ambayo haijawahi kutokea, na tunahitaji uongozi na ushiriki kutoka ngazi za juu za serikali na mipango thabiti, ya kina ya uratibu wa kitaifa na mifumo iliyowekwa, Dk Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa kanda wa WHO wa Afrika, alinukuliwa akisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wataalam walionya kwamba wakati maendeleo ya chanjo yanapaswa kusherehekewa, ni hatua ya kwanza tu katika kutolewa kwa mafanikio.

DW
Fimbo ya misaada kukatwa itatumika...
 
Watu weusi wa wapi? Utakuwa ulisikiliza vibaya. Mbona takwimu ziko wazi hata uki-search unapata kila nchi ina wagonjwa waliogundulika wangapi na vifo vinavyojulikana ni vingapi? Labda wewe ulisikia walipokuwa wanasema wamarekani weusi (kitu ambacho ni kweli) huko USA waliathirika sana. Bila shaka utakuwa unasikiliza redio mbao.
Soma hiyo 👇🏾 ndugu.

Soma na hiyo pia.
 
It is an issue when the whole meaning of the sentence changes! Yeye Magu alisema ''Mr president I am trying to preech, but I cannot reach you...'' akiwa anamaanisha ''najaribu kufanya mahubiri lakini siwezi kukufikia (kiwango chako). Ukimwambia hivi mtu asiyejua kiswahili atadhani unamwambia ''siwezi kukufikia (kukushika, au kwa simu nk.) Kwa kifupi mzee wa Phd alitafsiri neno kwa neno kama zile enzi za watu wanasema ''one coconut'' wakimaanisha Mnazi mmoja.
Unafanya direct translation mkuu! Unafikiri academically!
 
Soma hiyo 👇🏾 ndugu.
Sasa hili siyo Afrika. Ni Uingereza. Na sababu iko. Au hiyo lugha imekuchanganya? Marekani na Ulaya watu wenye background ya BAME (waafrika, wahindi na watu wa jamii nyingine ndogo )ndiyo wameathirika sana na huu ugonjwa. Ni Ulaya yote hasa zile zenye wesuis na wahindi wengi. Nilikuwepo na nilishuhudia. Na sababu zake zipo.
 
Hiyo ni nusu yao, mimi nazungumzia wote 100% wanapewa chanjo hewa (maji kama ulivyoita) bila wao au hata sisi waAfrika kujua ili tuone kwamba mbona hata wao wanapewa hii chanjo ili tusishtuke, lakini ukweli ni kwamba wao wanapewa 100% placebo (sio nusu yao) kama kanyaboya tu la kutuzuga, wakati sisi huku ndio tunapogwa majaribio halisi kabisa, hilo hata wale wanasayansi wa kifaransa walilisesemamtena live kwenye kituo cha television, tafuta hiyo video ya ‘french scientists’ youtube uone!
Lakini hii chanjo inanza kuchanjwa huko huko. Na hiyo placebo huwa ni njia inayotumika kwenye reasearch za aina hii! Nilifikiri ulivyojigamba post ya juu basi utakuwa unajua umuhimu wa placebo na ni kwa nini inatumika. BTW hivi unafikri wangekuwa wanataka kutufanyia majaribio kama haya wangekosa namna ya kufanya?
 
Umesema kweli ndugu yangu. Kama
ulikuwa unafuatilia siasa za COVID-19 utagundua kwamba kuna hila nyuma ya siasa hizi. Hivi ugonjwa unaobagua namna hii, ni ugonjwa wa namna gani. Kenya wafe kwa COVID 19 Tanzania hakuna COVID - 19. Hii imekaaje?.

Sweden hawakulock down na hatujasikia wana vifo vingi vya kutisha. Wanasayansi HALISI wanahoji kuhusu ugonjwa huu, wanahoji kuhusu uvaaji wa barakoa kama kweli unazuia maambukizi.

Wananchi wa mji wa London na kwingineko wanaandamana kuhoji siasa za COVID 19. Habari zao hazitangazwi sana kunani?. Kalaga bao ndugu zangu wanaounga mkono siasa za COVID 19 na kuchanjwa. Wahenga walisema UNACHOKIONA NI SEHEMU NDOGO TU. KIWILIWILI KIKO CHINI KIMEJIFICHA.
Mambo mengine mnakosa kwa sababu ya ukosefu wa maarifa. Ni nani kakumbia Tanzania hakuna Covid 19? Unamsikiliza Magufuli? Hujui hata sasa hivi tunavyochati hapa kuna watu wamelazwa hospital hapa Dar wana Covid 19? Hujui bado watu wanakufa japo kwa nchi zote za Afrika idadi ya vifo siyo kubwa? Unajua mazingira ya Sweden yalivyo? Unajua nchi nyingi za Scandinavia hakukuwa na lockdown ya amri bali ya hiari na watu wote waliamua kuji-lock down kwa hiyari?
 
Sasa hili siyo Afrika. Ni Uingereza. Na sababu iko. Au hiyo lugha imekuchanganya? Marekani na Ulaya watu wenye background ya BAME (waafrika, wahindi na watu wa jamii nyingine ndogo )ndiyo wameathirika sana na huu ugonjwa. Ni Ulaya yote hasa zile zenye wesuis na wahindi wengi. Nilikuwepo na nilishuhudia. Na sababu zake zipo.
Sasa huoni wanatumia kigezo hicho kuhamasisha serikali za nchi za Africa kuwachoma waafrika??
 
Sasa huoni wanatumia kigezo hicho kuhamasisha serikali za nchi za Africa kuwachoma waafrika??
Hapana. Hizo ni hisia zako. Ndiyo maana nakumbia aidha hujasoma au kuelewa hiyo habari. Chanjo imefanyiwa majaribio kwa asilimia kubwa Ulaya na Marekani na itaanza kutumika huko huko. Ondoa wasi wasi. Huku kwetu tuna matatizo mengi ya kuhofia tusiongeze hofu za kutengeneza.
 
Shirika la Afya Ulimwenguni-WHO, Alhamisi limezisihi nchi za Afrika kuandaa mipango ya kusambaza chanjo za COVID-19 kadri zitakavyopatikana.

Utafiti mpya wa WHO uligundua kuwa nchi nyingi za Kiafrika haziko tayari kwa kile kitakachokuwa harakati kubwa zaidi ya chanjo barani humo.

Kupanga na kuandaa mikakati kutafanikisha au kuharibu shughuli hii ambayo haijawahi kutokea, na tunahitaji uongozi na ushiriki kutoka ngazi za juu za serikali na mipango thabiti, ya kina ya uratibu wa kitaifa na mifumo iliyowekwa, Dk Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa kanda wa WHO wa Afrika, alinukuliwa akisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wataalam walionya kwamba wakati maendeleo ya chanjo yanapaswa kusherehekewa, ni hatua ya kwanza tu katika kutolewa kwa mafanikio.

DW
Wakajaribie mbwa kwanza
 
Back
Top Bottom