WHO yaitaka Afrika kujiandaa na usambazaji wa chanjo ya corona

Ndugu, sijui uko upande gani wa dunia. Hivi unakumbuka BBC na radio za huko ulaya zimekua zikitangaza kuwa watu weusi na wahindi ndio waathirika wakubwa wa corona??
Mambo ya ajabu sana, kwa huku Afrika, nchi zenye asilimia kubwa ya weupe ndio ziliathirika, hata sijui walikuwa wanaongea upuuzi gani hao BBC 😂😂
 
Majaribio ya chanjo yanayofanyika ulaya na Marekani ni placebo tu, ila majaribio halisi huwa yanafanuika Afrika, tafuta maana ya neno placebo
Wewe ndiyo nikuambia utafute maana ya placebo! Daa basi ngoja nikupe somo: Moja ya chanjo ya covid ilihusisha watu 30,000. Nusu walipewa dawa ya chanjo halisi na nusu walipewa placebo i.e. boya a.ka. maji special tu yasiyo na dawa yoyote. Wakati wanawachanja watu waliyojitolea huwa anayechanja na anayechanjwa hafahamu ipi ni dawa halisi na ipi ni placebo ila kila chupa inakuwa na searial namba ambazo mtengenezaji ataweza kutambua baadae ni yupi alichanjwa kwa dawa halisi na yupi alipewa boya. Kwa nini wanafanya hivi? Unajua maana ya placebo effect kwa kuanzia? Bila shaka unajua kwa sababu ni wewe umenidharau na kuniona sijui kitu
 
Broken english is not an issue for Africans. Only an idiot can mind about it. Even Mzungus they do speak broken english mkuu!
It is an issue when the whole meaning of the sentence changes! Yeye Magu alisema ''Mr president I am trying to preech, but I cannot reach you...'' akiwa anamaanisha ''najaribu kufanya mahubiri lakini siwezi kukufikia (kiwango chako). Ukimwambia hivi mtu asiyejua kiswahili atadhani unamwambia ''siwezi kukufikia (kukushika, au kwa simu nk.) Kwa kifupi mzee wa Phd alitafsiri neno kwa neno kama zile enzi za watu wanasema ''one coconut'' wakimaanisha Mnazi mmoja.
 
Hiyo ni nusu yao, mimi nazungumzia wote 100% wanapewa chanjo hewa (maji kama ulivyoita) bila wao au hata sisi waAfrika kujua ili tuone kwamba mbona hata wao wanapewa hii chanjo ili tusishtuke, lakini ukweli ni kwamba wao wanapewa 100% placebo (sio nusu yao) kama kanyaboya tu la kutuzuga, wakati sisi huku ndio tunapogwa majaribio halisi kabisa, hilo hata wale wanasayansi wa kifaransa walilisesemamtena live kwenye kituo cha television, tafuta hiyo video ya ‘french scientists’ youtube uone!
 
Ebu waitumie wao kwanza wapone, siyo kutuletea waone kama yafaa au lah..tena tujihadhari hawakawii kuweka mambo ya ajabu kwenye hizo chanjo, HATUWAAMINI HAWA WENZETU KABISA KABISA..
 

Kikubwa iwe hiyari, kusiwepo restrictions zozote. Anayetaka kuchanja achanje, asiyetaka matakwa yake yaheshimiwe as long as ni mwili wake. Tunasisitiza free will kwenye uchanjaji.
 
Fimbo ya misaada kukatwa itatumika...
 
Soma hiyo 👇🏾 ndugu.

Soma na hiyo pia.
 
Unafanya direct translation mkuu! Unafikiri academically!
 
Sasa hili siyo Afrika. Ni Uingereza. Na sababu iko. Au hiyo lugha imekuchanganya? Marekani na Ulaya watu wenye background ya BAME (waafrika, wahindi na watu wa jamii nyingine ndogo )ndiyo wameathirika sana na huu ugonjwa. Ni Ulaya yote hasa zile zenye wesuis na wahindi wengi. Nilikuwepo na nilishuhudia. Na sababu zake zipo.
 
Lakini hii chanjo inanza kuchanjwa huko huko. Na hiyo placebo huwa ni njia inayotumika kwenye reasearch za aina hii! Nilifikiri ulivyojigamba post ya juu basi utakuwa unajua umuhimu wa placebo na ni kwa nini inatumika. BTW hivi unafikri wangekuwa wanataka kutufanyia majaribio kama haya wangekosa namna ya kufanya?
 
Mambo mengine mnakosa kwa sababu ya ukosefu wa maarifa. Ni nani kakumbia Tanzania hakuna Covid 19? Unamsikiliza Magufuli? Hujui hata sasa hivi tunavyochati hapa kuna watu wamelazwa hospital hapa Dar wana Covid 19? Hujui bado watu wanakufa japo kwa nchi zote za Afrika idadi ya vifo siyo kubwa? Unajua mazingira ya Sweden yalivyo? Unajua nchi nyingi za Scandinavia hakukuwa na lockdown ya amri bali ya hiari na watu wote waliamua kuji-lock down kwa hiyari?
 
Sasa huoni wanatumia kigezo hicho kuhamasisha serikali za nchi za Africa kuwachoma waafrika??
 
Sasa huoni wanatumia kigezo hicho kuhamasisha serikali za nchi za Africa kuwachoma waafrika??
Hapana. Hizo ni hisia zako. Ndiyo maana nakumbia aidha hujasoma au kuelewa hiyo habari. Chanjo imefanyiwa majaribio kwa asilimia kubwa Ulaya na Marekani na itaanza kutumika huko huko. Ondoa wasi wasi. Huku kwetu tuna matatizo mengi ya kuhofia tusiongeze hofu za kutengeneza.
 
Wakajaribie mbwa kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…