William Ruto avunja Baraza la Mawaziri Kenya

William Ruto avunja Baraza la Mawaziri Kenya

amka wakutufue..😂
hawawezi kuwatufua wote watajitawala ?

Serikali.jpg
 
Si afadhali Ruto ameshtuka na kuchukua hatua huko bongo hilo baraza la Samia unaona lina hali nzuri??
Kenya usiifananishe na Tanzania, kuuwana kisiasa hawjaanza leo wala jana.

Umesahau Kikwete alivyokwenda kuwapagtanisha? Au bado ulikuwa kinda tunduni?
 
Gen z wanataka Serikali ipunguze matumizi Ili pesa hizo ziende kutengeneza ajira.

Ruto anavunja Baraza Ili awakaribishe WAPINZANI Ili washirikiane kula,

Sasa hapo ni lugha gongana.
Hapana. Ruto kachukuwa hatua nzuri sana. Hata kabla ya kuvunja baraza alichukuwa hatua za kubana matumizi eg kupunguza safari, ununuzí wa magari mapya nk. Thread iko hapa.
 
Breaking news

Ofisi ya Deputy President na Prime minister haziguswi na maamuzi haya

Citizen TV

======

Rais wa Taifa la Kenya, William Ruto amewafuta kazi mawaziri wote wa Baraza lake, kufuatia shinikizo kutoka kwa vijana wa kizazi cha GenZ waliotaka mabadiliko.

Katika kutangaza mabadiliko hayo siku ya Alhamisi Julai 11, Ruto alisema kuwa ni Naibu wake Rigathi Gachagua na Katibu Mkuu wa Barza la Mawaziri Musalia Mudavadi wa wizara ya Mambo ya Nje pekee wanaosalia.

“Baada ya kutafakari na kuwasikiliza kwa makini Wakenya na baada ya kutathmini Baraza langu la Mawaziri, leo nimeamua kuwafuta kazi mawaziri wote,” Ruto alisema, “lakini Naibu wangu na Waziri Mkuu hawajaathirika.”

Pia, soma=> Rais Ruto asitisha kusaini Muswada wa Sheria ya Fedha 2024, aurejesha Bungeni
MUNGU WANGU NA BABA YANGU!!!

NAZIWEKA NCHI YA KENYA KWENYE KIGANJA CHA MKONO WAKO!!!

NAOMBA BABA, UKAWA LINDE, UKAWA HIFADHI, KWA MAANA FADHILI ZAKO NI ZA MILELE!!!

BABA, NAOMBA ROHO WAKO MTAKATIFU AKAMUONGOZE KATIKA KAZI YAKE YA KUNIONGOZA NCHI!!!

NAOMBA TOBA KWA AJILI YA RAIS RUTO PAMOJA NA UONGOZI WOTE ULIOPITA!!!

NAOMBA TOBA KWA AJILI YA VIJANA WA GEN "Z".

BABA MUNGU IBARIKI KENYA NA WATU WAKE!!!

NINAIFUNIKA NCHI YA KENYA KWA DAMU YENYE THAMANI NYINGI NA YA AJABU YA BWANA WETU YESU KRISTO WA NAZARETH ALIYE HAI.

AMINA NA AMINA 🙏🙌💖
 
Kwa haya mawazo wacha CCm itawale tu
 
Asante sana

Chura kiziwi wetu aendelee kujifanya kiziwi na kipofu ila upo wakati aibu zaidi ya hii itamtafuna na kizazi chake, msemo wa watz ni maiti siuoni miaka ijayo hawatoamini macho yao
 
Kenya usiifananishe na Tanzania, kuuwana kisiasa hawjaanza leo wala jana.
Tanzania hawauwawi watu??

Wasiojulikana hawakuwa wanaweka miili inaelea barabarani kwenye viroba?

Majuzi ITV wametoa ripoti kuanzia April mosi hadi Juni watu 45 hawajulikani walipo.

Hata majuzi ni nguvu ya mtandao ndio ilimuokoa Sativa vinginevyo angekuwa ameuwawa.
Umesahau Kikwete alivyokwenda kuwapagtanisha? Au bado ulikuwa kinda tunduni?
Kibaki alipopoteza referendum 2005 ilikuwa ni obvious watu hawana imani naye , yaliyotokea 2007 ni aina ya ushenzi wa viongozi wa kiafrika kulazimisha kutawala Kibaki hakushinda ule uchaguzi badala yake alitumia state machineries ilikuwa kituko nakumbuka tukio la kujiapisha alivyomleta jaji chap chap.

Wakenya waliingia mitaani ndio kilicholeta ile PEV 2007-2008 hadi walipokubali "nusu mkate" ili kuepusha madhara zaidi.

Hata katiba mpya 2010 ilichochewa kupatikana ili kuzuia ushenzi kama huo usijirudie leo hii Kenya mhili wa mahakama unao uwezo wa kutengua amri ya rais na bunge pia linao uwezo kutengua amri ya rais ikiwa ni kinyume na katiba maana katika imewapa wananchi mamlaka kwenye sura ya kwanza kabisa

Ndio maana vitu kama BBI vilipigwa chini.
 
Back
Top Bottom