Maelezo yake hayajitoshelezi, msaidie.
Kulingana na vile nilivyomsoma, amedai kuna sehemu ndani ya colon inayohusika kuchuja mara ya mwisho kipi kiwe taka, na kipi kitumike tena na mwili.
Ndio nawataka nyie madaktari mtuambie, hiyo sehemu ndani ya colon inayotumika kuchuja inaitwaje? hiyo colon haina parts?
Ok Ngoja Nimsaidie Kuelezea Kidogo kwa Kirefu kuhusu hiyo Process.. (Digestion yote ili unielewe zaidi)
Kwanza unapokula Chakula chochote Mmeng'enyo wake Huanzia Mdomoni ambao huwa mechanical Reaction (Kutafuna yaani Mastication) na Chemical Reaction (Enzymes zinazopatikana kwenye saliva "mate")
Hapa ndo hupatikana Chakula Kilichojibumba Kinachoitwa
Bolus
Unakimeza Kinapita kwenye Koo la chakula mpaka Tumboni kwa Msukumo unaitwa peristalsis..
Kikifika Tumboni Hivyo hivyo kuna Mechanical Rxn (Vibration and Mixing of Gastric juices and food) na Chemical Rxn (Secretion of Enzymes na HCL , Pepsin Etc)
Sasa Kutokana na Reaction hiyo kile Chakula Bolus hu "change" kuwa Chakula ambacho ni semifluid "chenye Mfano wa Uji" ambacho Huitwa sasa
Chyme.
Sasa Hiyo Chyme Huingia kwenye Utumbo Mdogo (Small intestine) ikitokea kwenye Tumbo la chakula (Stomach) na Hufika sehemu ya Kwanza ya Utumbo mdogo Duodenum...
Kwenye
Duodenum , chyme imachanganyika na Nyongo "bile" kutoka kwenye Ini na gallbladder (ambayo kazi kuwa Huwa ni kuyeyusha mafuta kwenye Chyme ) na Hukutana pancreatic juices kutoka kwenye Kongosho (ambayo kazi kubwa ni kuendelea Kumeng'enya carbohydrates, proteins, na fats)..
Sasa Baada ya Kufanyika Kwa Digestion ya kutosha au Ya kuridhisha mwili unaamua kuanza Kuabsorb baadhi ya Nutrients..
Na Absorption huanza hapa sasa kwenye Utumbo mdogo kupitia Kuta za (Utumbo mdogo Small intestines) yaani
Jejunum and Ileum..
Sasa Nutrients Hufyonzwa (Absorbed) kutoks kwenye Kuta hizo kupitia Villi au Vilus (Umoja) kwenye kwenye damu "bloodstream".
Fatty acids na glycerol hufyonzwa "absorbed" kwenda kwenye lymphatic system kama
chyle kupitia lacteals..(hizi ni lymphatic vessel zilizo kwenye Utumbo mdogo katika lymphatic sys..)
Sasa
Chyme itakayobaki bila kuchenjwa kuwa
chyle na kupelekwa kwenye bloodstream itaingia Kwenye Large Intestine (Colon) na mwanzo kabisa itaingia kwenye
Cecum..
sasa kazi kubwa ya
cecam ni kupokea Hiyo chyme iliyotokka kwenye
ileum na Kunyonya Baadhi ya Maji na chumvi chumvi ambazo hazikufyonzwa kipindi kunafanyika Ufyonzwaji Kwenye Utumbo mdogo..
Ikitoka hapo chyme Inaingia kwenye
Ascending Colon sasa hapa ndo maji na Chumvi Hunyonywa kwa Ajili ya kupunguza Ule usemi fluid wa Chyme na kuobadilisha ile chyme kuwa kwenye ugumu ugumu..
sasa kwenye Hatua Hii maji hunyonywa sana na kama kuna fluid nyingine pia hunyonywa na kuinguzwa kwenye Damu kwa kasi kwenye
Transverse Colon na kwenyewe absorption inaendelea ila humu pia bacterial fermentation hufanyika..
sasa kwenye
Descending Colon hapa ndo sehemu ya Mwisho ya Unyonywaji wa Maji kwa kasi sana
na ndo maana Jamaa kama ulimsoma alisema hiyo ndo sehemu ya mwisho na hutumika kuchuka kipi kiwe taka na kipi kiingie kwenye damu..
kwa sababu hapa ndo huingiza Fluid zote za Muhimu kwenye damu na hapa ndo hutengenezwa jina lingine kutoka kuwa
Chyme mpaka kuwa
Feacal Material au Feaces..
So ni hakika kwamba Unapoweka Fluid kwenye Colon Hufanya Absorption iwe kasi sana Kuliko na ambavyo ukinywa Kupitia Mdomoni na ikapita Process Zote hizo..
Natumanin kwa maelzo hayo marefu umeelewa?
Wako Katika Kukuelewesha..
DR Mambo Jambo