Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,855
- 189,385
Aisee!
Bonge la mtu,kitambi kule na suti kuubwa,anachomoza kwenye IST...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bonge la mtu,kitambi kule na suti kuubwa,anachomoza kwenye IST...
Jaamaa katibua watu na wamekubali kutibuliwa
Ah ah ah kweli mkuu asitufokee, mtu unanunua gari kama kiatu cha mtoto!
Watakwambia azili mafuta.
Wanahesabu zao wenyewe wanapigaga"1lt/15km
"Alafu vile mjini parking ni shida,so ukiwa na hatchback ni rahisi kupata nafasi.
Aiwezekani kubwa zima na vinyweleo kibao kifuani alafu unang'ang'ana na Passo sijui,Ist,Vitz wakati izo ni gari za mabinti tena mabikira.
Huu uzi umenikumbusha juzi, Tulikuwa pub na dingi mmoja hivi, yeye anamiliki V8, wakati tunaendelea kunywa, akatokea jamaa mmoja akashuka kwenye IST yule dingi akaropoka "Ukiwa unaendesha V8 afu ukamuona mtu anaendesha IST unamuona kama amechanganyikiwa hivi"
...watu tulicheka balaa[emoji23][emoji23]
NB: Tuache dharau wakuu gari ni gari ilrimradi ina matairi manne na inatembea
Aisee, kwa kweli mmeamua kunitusi mimi na starlet yangu
Hujamtajia na zile nyingine za watoto na house maid.Hunielewi ndugu. Nimekuambia ninazo gari zangu mm. Mke wangu ana gari yake, Nina v-shapes engine zenye horse power ya kutosha mbili. Na still hiyo baby walker naitumia pia pale ninapolazimika kuitumia esp siku ninapokuwa too busy mazingira ya mjini. Tofauti yangu mm na ww ni matazamo wa kwann tunamiliki magari. Pengine labda na maana ya neno mwanaume. Ila sikupingi as long as hizo fikra ni zako na ndivyo unavyojisikia ndani yako. Mm hisia zako hazina maana yoyote kwangu.
House maid hana boss. Watoto ya kwao hayanihusu mkuu.Hujamtajia na zile nyingine za watoto na house maid.
Hata ingekuwepo inamuhusu nin? Kama tu wenye nyumba na wanao pangahebu tuwekane sawa jamanii, kwani hata kwenye manual ya hao waliotengeneza hizo the so called gari za kike,kuna mahali pamenadikwa for male or female? [emoji2368]
Jaamaa katibua watu na wamekubali kutibuliwa
Absolutely!Watakwambia azili mafuta.
Wanahesabu zao wenyewe wanapigaga"1lt/15km
"Alafu vile mjini parking ni shida,so ukiwa na hatchback ni rahisi kupata nafasi.
Aiwezekani kubwa zima na vinyweleo kibao kifuani alafu unang'ang'ana na Passo sijui,Ist,Vitz wakati izo ni gari za mabinti tena mabikira.
[emoji23][emoji23] tuwaachie WatumishiNamuunga mkono mleta hoja!
Kiukweli tujibane bane tutembelee gari za kiume kama-
NISSAN X-TRAIL
KLUGGER
NISSAN DUALS
PRADO
SUBARU FORESTER XT
ONGEZEA...yaani unapita nalo maeneo kila mtu anapandwa na mizuka + wazimu.
lakini hivi vi IST,SPACIO,PASSO,HARRIER,CROWN,ALLION,PREMIO,VITZ etc.. itoshe sasa kuwaachia hawa dada zetu.
RAV 4 + SUZUKI,tuwaachie wazee wetu + watumishi wa Mungu.
Sikatai kama kipato kinaweza kuwa kidogo,chukua basi hata PROBOX ijulikane wewe ni mtu wa kazi kazi!...sio dume nzima una minywele kila mahali unatembelea VITZ aibu tupu!!
Kwahiyo hiyo anayepanda daladala anapanda kaburi la wengi sio[emoji1787]
Nimecheka kwa sauti.
Yeye atuambie anaendesha gari gani, au ndio wale "bora kupanda daladala kuliko kuendesha baby walker"
tusisahau kuwa kila mtu ana ndoto yake pia..hilo unalosema baby walker kuna mwingne ndo analiwaza lini ataendesha..tusiweke akilini kuwa hiki ni cha wale hiki cha kwetu mmhh tunakosea snaNdugu zangu
Inakuwaje mwanaume mzima anaendesha ka baby Walker?
Yaani jibaba nene linatumia kigari cha mkewe? Huoni aibu? Si bora hata upande daladala?
Hata Bashite alisema wazi vi gari vya IST ni vigari vya kuhongwa wewe mwanaume huoni aibu?
Hii tabia walikuwa nayo wanaume wa Kinondoni, ila sasa wameambukiza na wa mikoani..
Aibu sana
Hahaha,serious Mkuu..[emoji23][emoji23] tuwaachie Watumishi
Chukua Pepsi kwa Mangi Hapo Nitalipia
Halafu BAK na hapa atabisha na IST yake