Wito kwa Serikali yetu, Huu ni Udhalilishaji wa Bullying & Intimidation. Mbona Rais Samia Hadhalilishi? Tusiruhusu Udhalilishaji Huu Uendelee!

Nielewe, ajira za serikali hazina kifungu kinachosema ukikosea utendaji wa kazi mkuu wa mkoa atakuhukumu hadharani, kila wizara na idara inawatendani wake na wakwanza aliye juu yako ndiye atakayekuhoji na si vinginevyo, bahati mbaya watanzania tunafurahia hizi mahakama za kina Makonda kiadi na yeye akatutaka tusikimbilie mahakama rasmi.
 
Uwezo mdogo Sana DAB.

Hii pia inawasumbua watz huwa wanaamini ili wafanikiwe lazima wamshushe thamani ya MTU ili thamani yao ipande

Wamekuwa wakifanya udhalilishaji kwa kigezo cha kujenga nchi na uchapakazi.
 
Kazi za serikali zinasimamiwa na waziri na katibu mkuu wa wizara husika, Makonda anaingilia majukumu ya watendaji wengine, kama kunajambo haliko sawa anatakiwa awaone hawa na si vinginevyo.
Barua za wajiriwa zina maelekezo yote na hatua mtumishi atazochukuliwa dhidi ya utendaji mbovu na utovu wa nidhamu, nazo ni za ndani ya ajira yake tu.
 
Tanzania sio masikini bali ni tajiri sana, ndio maana imekuwa ikifanywa ni shamba la bibi

Magufuli, ameonyesha nia ya dhati kwa kauli na matendo

Kuyatekeleza yote haya sio kazi ya lele mama, ni kazi ya shuruba

by nature Watanzania ni wavivu

Maadam sasa mkombozi tumempata, whatever the names, be it or not, twende naye ili tufike kule tunakotakiwa kufika, na safari nyingine ni ngumu, kuna wengine wataishia njiani, na kuna wengine watafika wakiwa hoi bin
'Tanzania imebadilika nyinyi'-In Job Ndugais voice
 
Lakini hawa wote ni role model wako Pascal Mayalla umewaandikia mabandiko mengi sana humu ya kuwasifia
 
Nimesikiliza clip husika na nimejifunza kitu zaidi kutuhusu sisi watanzania.
1. Tunapenda maelezo rahisi hata kwenye vitu vya kitaalamu. Meneja amekuwa jasiri kusimamia anachoelewa kiasi cha kuonekana hajui kujieleza.
2.Mh RC amekomaa ki utendaji ndio maana hakuvunja kikao chake.
Bullying language nimeisikia lakini sio kubwa kuliko language kwenye clip ya Mh. Magu.... Mimi mwananchi wa Arusha nitampima RC wangu baada ya kuona atakavyoyafanyia kazi mambo yote tunayoyasikia na kuyaona kwenye hizi clips.
 
Kwahio Samia akifanya au asipofanya right inakuwa wrong or vice versa ? Mbona tumekuwa watu wa kuunganisha mambo pasipo muunganiko ?!! Ukisema mbona Samia hafanyi unamaanisha akianza kufanya na wengine wafanye ?

Kwanini tusisimamie haki no matter the circumstances....

Kwahio sababu hapa Samia wakati anatoa Hotuba yake alitumia maneno makali ya Stupid na sisi waajiriwa wetu tuanze kufanya hivyo kwa ukali wa maneno ?; au pale alivyomwambia jamaa Nosense

View: https://www.youtube.com/watch?v=5qwv2XXiBjU
 
Kwa mtazamo wa Pascal itafika mahala ata Wabunge wakiwahiji Mawaziri wataambiwa wanafanya Bullying and intimidation.
Yaani Boss wangu ananiuliza kuhusu utekelezaji wa majukumu yangu nashindwa kueleza,then anyamaze tu,kweli!
 
Mkuu P sidhani kama kuna bullying hapo!ukweli lazima usemwe, viongozi wengi ktk taasisi za serikali hawafuatilii majukumu yao, hawana taarifa ya mambo yaliyo chini ya idara zao!pia serikalini huu utaratibu wa reporting hakuna so viongozi wengi hawajui hata kuandaa report!hvo Makonda lzm awachangamshe kidogo waache uzembeuzembe!serikali watumishi ni wazembe sana sana!business as usual
 
Dah
Nimeisikiliza nimejisikia vibaya sana kama ndo mimi

Sijajua mlengwa alikuwa na hali gan

Ni aina gani ya viongoz tulio nao? Hili ni tatizo na huzaa chuki kubwa sana
 
Kwa mtazamo wa Pascal itafika mahala ata Wabunge wakiwahiji Mawaziri wataambiwa wanafanya Bullying and intimidation.
Yaani Boss wangu ananiuliza kuhusu utekelezaji wa majukumu yangu nashindwa kueleza,then anyamaze tu,kweli!
umepigilia msumari wanmoto kwa mfano, lugha nyepesi na style nyingine ya kipekee sana ambayo haikutarajiwa. thanks very much πŸ‘ŠπŸ’ͺπŸ‘
 
Asante sana kwa ufafanuzi, umenitoa kwenye box. Ila nadhani pia ni muhimu viongozi kuhudhuria kozi za communication. Nadhani kwa ulivyofafanua basi ktk uongozi wangu nitakuwa msikivu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…