Tatizo na upungufu wako ni mmoja tu. Kwamba kwa akili na ufahamu wako unadhani Paul Makonda ana moral authority ya kuwa treat viongozi wenzake kwa namna ile.
Tunasema hivi;
Likely, (labda) ni kweli kuna weaknesses kwa uongozi wa TARURA hapo Arusha ktk usimamizi na utendaji wa shughuli zao
Swali ni, Je hiyo inampa uhalali gani wa kimaadili Paul Makonda kushughulikia mapungufu hayo kwa staili hiyo?
Je, Hakuna taratibu za kawaida za kiutumishi za kumwajibisha kiongozi mzembe na asiyetimiza wajibu wake ipasavyo?
Iko hivi.
Mimi sina shida kabisa na kiongozi wa juu kumsimamisha kiongozi yeyote wa umma, taasisi au shirika la umma mbele ya watu wengine, wananchi watoto kwa watu wazima na mbele ya kamera za TV ajibu maswali fulani juu ya majukumu na utendaji wake wa kila siku juu ya mipango, sera na utekelezaji wake ktk taasisi au shirika analoongoza/simamia.
Shida yangu mimi ni Moja tu. Na ofcoz ndio kiini cha hoja ya mleta hoja ndugu
Pascal Mayalla kwamba, serikali sio mtu mmoja bali ni mfumo unaohusisha mnyororo mrefu ktk utendaji wake.
Wewe unasema hivi👇👇
"...
..every responsible civil servant, with capacity or not, anywhere within or outside the country, must be fully responsible and very aware on their roles, duties and responsibilities.
they must understand very well their job descriptions, they must be fully aware on the status of programs and projects within their areas of work etc..."
That's right..
Unadhani huyu mtu hayajui yote hayo; job description yake? Roles and his responsibilities zake?
Unadhani hajui miradi anayoisimamia na status zake ktk eneo lake?
Paul Makonda angekuwa patient kidogo tu na kuomba taarifa ya anachokitaka kukifahamu au kuelewa ktk taasisi hiyo angeshindwaje kwa mfano kiasi cha kutumia njia dhalili na ngumu kiasi kile?
Kumbuka Meneja ni kiongozi mkuu wa taasisi ndani ya mkoa yenye wilaya kadhaa na miradi mingi inayotekelezea. Na chini yake wako wakuu wa idara wengi wengine huko wilayani.
Na kama alimshitukiza tu na kutaka awe na taarifa zote kichwani na kwa usahihi kumpa yeye na Mr TARURA kujitetea kuwa taarifa zingine ziko kwenye mafaili na bado RC akang'aka na kuporomosha maneno ya kashfa yenye nia ya kutweza utu na kudhalilisha, basi obvious shida iko kwa RC Makonda.
Na hiyo ndiyo bullying & intimidation yenyewe. Kwa sababu RC ametumia madaraka yake kusema lolote lisilofaa kwa ndugu huyu. Akatengeneza mazingira ya kufanya huyu kiongozi aonekane kwa jamii yote kuwa hafai, hawezi kazi na kumfanya awe na hofu, atishike. Hiyo siyo sawa hata kidogo!
Lakini nyuma ya RC kiuhalisia lengo si kuboresha au kutengeneza bali anakuwa na ajenda nyingine ya siri kabisa mara nyingi ikiwani ovu.
Wote tunajua tabia ya Paul Makonda. Ni kiongozi "populist", mpenda umaarufu. Ni aina copyright ya John P. Magufuli.
Makonda ni kiongozi mpenda madaraka kwa gharama yoyote hata kama ni kumwaga damu ya watu achilia mbali kudhalilisha kwa namna hii.
Makonda is a bully iwe unajua hivyo au hujui. Uongozi ni HEKIMA na BUSARA. Huyu ndugu yako hana hayo mawili. Hastahili kuongoza kabisa.!!!
NB:
By the way nikuulize swali Moja tu ndugu
Tlaatlaah kwamba, Itakuwaje iwapo Rais Samia Suluhu Hassan akimshitukiza RC Makonda hapo Arusha na kuanza kumshona maswali mbalimbali mfululizo kuhusu jambo lolote mkoani kwake mbele ya umati wa wananchi?
Unadhani huyu jamaa yako anaweza kuwa na jibu sahihi kwa kila swali bila kutegemea msaada wa watendaji na wasaidizi wake ndani ya mkoa? Na vipi sasa akikosea kujibu swali Moja au mawili? Je, unadhani ni halali Rais aanze kumvurumishia maneno ya kashfa na kumdhalilisha kuwa hajui job description yake au roles and responsibilities zake kama RC?
Ni halali Rais Samia Suluhu Hassan ajute hadharani kusema sijui ulipataje nafasi ya u-RC?
Hebu tafakari halafu njoo tusemezane..