Wito kwa Serikali yetu, Huu ni Udhalilishaji wa Bullying & Intimidation. Mbona Rais Samia Hadhalilishi? Tusiruhusu Udhalilishaji Huu Uendelee!

Uko sahihi ila sio sahihi kabisa.

Wapalestina wanafanyiwa zaidi ya haya na watesi wao kula Gaza,West bank ila hao wenye Dunia wapo kimya tu.
 
mbona kwa hio link naona kama ilikua ni 2017 ndio alimsema mwendazake ni miaka minne kabla ya demise ya mzee wetu Dr Yohana au mimi nimeona tofaut?
 
Wewe unaona sawa kiongozi anaulozwa kuhusu Halmashauri yake, hata taarifa anajiumauma tu. Lazima atumbuliwe. Hii style ndo ilifaa sana coz viongozi walijisahau na kutowajibika

alikuwa na uwezo wa kumtumbua wakiwa ofisini, kwanini adhalilishe mbele ya Jamii?
 
Hao mnaosema wanafanyiwa bullying ukifika ofisini kwao kutaka huduma unaweza kumpiga risasi kwa huduma mbovu wanazotoa
 
Kwa kiingereza chako cha kuunga unga ni ajabu umefanya kazi huko unakodai. Labuda ulipewa kazi kwa nguvu ya personality yako na siyo kwa sababu una sharp intellect.
 
We expected a Manager to give a broader view of the roads he is responsible with as a Regional manager;in terms of how many kilometers his office currently is maintaining and how far have they gone, explain to the common Wananchi to understand what are gazetted roads and how do they look like and outline broader future plans to improving roads infrastructure in the region.
 
Kuna yule Mwamba alikuwa anasimamia ujenzi wa Barabara kule kusini na degree yake ya Philosophy na yule Mwamba alikuwa na Makamu wa Rais kule Mwanga anasimamia ujenzi wa hospitali akiwa ni Engineer wa Kilimo.
Inahitaji akili ya mwenda wazimu kuwatetea watumishi wa umma wa nchi hii!
 
Na lugha ya malkia inakusumbua kidogo.
 
mbona kwa hio link naona kama ilikua ni 2017 ndio alimsema mwendazake ni miaka minne kabla ya demise ya mzee wetu Dr Yohana au mimi nimeona tofaut?
Kwa magufuli hakufunguka, alijiweka mtu kati ni kama aliuliza swali vile, angalia aliweka na alama ya kuuliza.
 
Unaweza kutuambiia kwenye video uliyoambatanisha na uzi wako ni kauli gani za Makonda zimedhihirisha β€œbullying” na kauli gani ni ushahidi wa β€œintimidation?

Pia ingependeza kama ungefafanua tuhuma zako za sadist/sadiam dhidi ya Chalamila kutokana na ushahidi wa maneno pekee yake aliyotamka kuhusu vibaka.

Mwisho kabisa, kwamba umefanya kazi ya Ushauri Ubalozi wa UK Pretoria na dunia nzima kwa ujumla, ina umuhimu gani au uzito gani na hoja zako kwenye uzi huu? Na tuseme β€œMama Samia” angekuwa anafanya β€œbullying and intimidation”, jee ingekuwa okay kwa Makonda kufanya?
 
Mkuu. Wasomi wetu nao ni waoga kupitiliza. Kila baada ya neno moja anaweka maneno ''mheshimiwa mkuu wa mkoa''. Nidhamu ya woga kabisa. Anyways, nimufurahi sana kwa sababu Makonda anazidi kujichimbia kaburi mwenyewe. Ni laana ya ukatili aliofanya.
 
Tatizo na upungufu wako ni mmoja tu. Kwamba kwa akili na ufahamu wako unadhani Paul Makonda ana moral authority ya kuwa treat viongozi wenzake kwa namna ile.

Tunasema hivi;

Likely, (labda) ni kweli kuna weaknesses kwa uongozi wa TARURA hapo Arusha ktk usimamizi na utendaji wa shughuli zao

Swali ni, Je hiyo inampa uhalali gani wa kimaadili Paul Makonda kushughulikia mapungufu hayo kwa staili hiyo?

Je, Hakuna taratibu za kawaida za kiutumishi za kumwajibisha kiongozi mzembe na asiyetimiza wajibu wake ipasavyo?

Iko hivi.

Mimi sina shida kabisa na kiongozi wa juu kumsimamisha kiongozi yeyote wa umma, taasisi au shirika la umma mbele ya watu wengine, wananchi watoto kwa watu wazima na mbele ya kamera za TV ajibu maswali fulani juu ya majukumu na utendaji wake wa kila siku juu ya mipango, sera na utekelezaji wake ktk taasisi au shirika analoongoza/simamia.

Shida yangu mimi ni Moja tu. Na ofcoz ndio kiini cha hoja ya mleta hoja ndugu Pascal Mayalla kwamba, serikali sio mtu mmoja bali ni mfumo unaohusisha mnyororo mrefu ktk utendaji wake.

Wewe unasema hiviπŸ‘‡πŸ‘‡

".....every responsible civil servant, with capacity or not, anywhere within or outside the country, must be fully responsible and very aware on their roles, duties and responsibilities.

they must understand very well their job descriptions, they must be fully aware on the status of programs and projects within their areas of work etc...
"

β€ŠThat's right..

Unadhani huyu mtu hayajui yote hayo; job description yake? Roles and his responsibilities zake?

Unadhani hajui miradi anayoisimamia na status zake ktk eneo lake?

Paul Makonda angekuwa patient kidogo tu na kuomba taarifa ya anachokitaka kukifahamu au kuelewa ktk taasisi hiyo angeshindwaje kwa mfano kiasi cha kutumia njia dhalili na ngumu kiasi kile?

Kumbuka Meneja ni kiongozi mkuu wa taasisi ndani ya mkoa yenye wilaya kadhaa na miradi mingi inayotekelezea. Na chini yake wako wakuu wa idara wengi wengine huko wilayani.

Na kama alimshitukiza tu na kutaka awe na taarifa zote kichwani na kwa usahihi kumpa yeye na Mr TARURA kujitetea kuwa taarifa zingine ziko kwenye mafaili na bado RC akang'aka na kuporomosha maneno ya kashfa yenye nia ya kutweza utu na kudhalilisha, basi obvious shida iko kwa RC Makonda.

Na hiyo ndiyo bullying & intimidation yenyewe. Kwa sababu RC ametumia madaraka yake kusema lolote lisilofaa kwa ndugu huyu. Akatengeneza mazingira ya kufanya huyu kiongozi aonekane kwa jamii yote kuwa hafai, hawezi kazi na kumfanya awe na hofu, atishike. Hiyo siyo sawa hata kidogo!

Lakini nyuma ya RC kiuhalisia lengo si kuboresha au kutengeneza bali anakuwa na ajenda nyingine ya siri kabisa mara nyingi ikiwani ovu.

Wote tunajua tabia ya Paul Makonda. Ni kiongozi "populist", mpenda umaarufu. Ni aina copyright ya John P. Magufuli.

Makonda ni kiongozi mpenda madaraka kwa gharama yoyote hata kama ni kumwaga damu ya watu achilia mbali kudhalilisha kwa namna hii.

Makonda is a bully iwe unajua hivyo au hujui. Uongozi ni HEKIMA na BUSARA. Huyu ndugu yako hana hayo mawili. Hastahili kuongoza kabisa.!!!

NB:
By the way nikuulize swali Moja tu ndugu Tlaatlaah kwamba, Itakuwaje iwapo Rais Samia Suluhu Hassan akimshitukiza RC Makonda hapo Arusha na kuanza kumshona maswali mbalimbali mfululizo kuhusu jambo lolote mkoani kwake mbele ya umati wa wananchi?

Unadhani huyu jamaa yako anaweza kuwa na jibu sahihi kwa kila swali bila kutegemea msaada wa watendaji na wasaidizi wake ndani ya mkoa? Na vipi sasa akikosea kujibu swali Moja au mawili? Je, unadhani ni halali Rais aanze kumvurumishia maneno ya kashfa na kumdhalilisha kuwa hajui job description yake au roles and responsibilities zake kama RC?

Ni halali Rais Samia Suluhu Hassan ajute hadharani kusema sijui ulipataje nafasi ya u-RC?

Hebu tafakari halafu njoo tusemezane..
 
Huo ndio urasimu unaowalinda watumishi wasiozimudu kazi walizopewa. Mtaalamu akiifanya kazi yake inavyopaswa hakuna mwanasiasa anayeweza kumyumbisha. Engineer anashindwa kueleza majukumu yake kwa lugha rahisi.. halafu tumlaumu Makonda?
 
Mkuu. Watu kama huyo unapoteza muda wako kujadiliana nao. Fikiria: mtu mzima mwenye akili kama hawezi kuona tatizo kwenye hayo ''mahojiano'' unaweza kumwelimishaje akuelewe?. Kitendo tu cha kuona Makonda yuko right kinatakiwa kikufanye uone upeo wake wa kuchanganua mambo ni mdogo. Ajira, namna ya kufanya kazi nk zina taratibu zake. Japo Tanzania ina tatizo kubwa la utendaji kazini lakini kuna namna ya kushughulikia na siyo usanii wa namna hiyo.
 
Utendaji wa watumishi wa umma unaboreshwa kwa kuwahoji kwa kuwafokea kwenye vikao?
 
Huo ndio urasimu unaowalinda watumishi wasiozimudu kazi walizopewa. Mtaalamu akiifanya kazi yake inavyopaswa hakuna mwanasiasa anayeweza kumyumbisha. Engineer anashindwa kueleza majukumu yake kwa lugha rahisi.. halafu tumlaumu Makonda?

Huo ndio urasimu unaowalinda watumishi wasiozimudu kazi walizopewa. Mtaalamu akiifanya kazi yake inavyopaswa hakuna mwanasiasa anayeweza kumyumbisha. Engineer anashindwa kueleza majukumu yake kwa lugha rahisi.. halafu tumlaumu Makonda?
Siyo kosa lako. Ni upeo wako wa kuona na kuchanganua mambo. Pole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…