Hakuna rais muislamu mzalendo kwenye nyanja yoyote ..video nimeku postia mfano
Ngoja nikuvumilie hivyo hivyo na bla bla zako,nitarejea kwenye video zako,nitachukua kama ndio hoja zako
Kwanza umeonyesha ujinga mkubwa kwa kusema waislamu wote hawana akili,lkn kumbe unazungumzia Maraisi,je waislamu wote ni maraisi?
Next time usikurupuke kwakuwa tu unauwezo wa kuandika
Hoja ya kwanza kutokana na video, ni Marehemu Magufuli anazungumzia kuunganishwa umeme kwa gharama ya shilingi 23,000
Ukweli ni kwamba gharama hizo haziendani na uhalisia,hizo gharama ni za umeme wa kule vijijiji
Kuweka tu umeme ndani bila kuvuta nguzo,kwa maana nguzo ipo hapo karibu inazidi 23,000
Huyo saveyer tu unalipa 50,000,bado luku
Kwahiyo kwa mifano hiyo utaona Magu aliongea kisiasa zaidi
Na ndio maana watu wengi walicheleweshewa kupata huduma hiyo
Je, hapo utamlaumu Mama Samia?
Hoja ya pili kutokana na video yako
Kwamba Magu alisema nchi inakopa,je Mkapa hakukopa? Je Mkapa hakubinafsisha mashirika ya umma?
Okay je kukopa ni kubaya au namna ya kutumia mkopo huo ndio kubaya?
Kama tunakopa na hatutumii kwa malengo husika basi tunafanya makosa kama nchi lakini usiseme eti maraisi waislamu hawana uzalendo