Lissu sio lazima awe Rais sasa lakini Lissu ni chaguo sahihi na ana uwezo wa kusukuma agenda ya mabadiliko ndani ya chama cha CHADEMA na Taifa hili. Lissu sasa tunamtegemea kuweka msingi mzuri na uongozi katika vuguvugu la kuanza kupiagania uhuru wa Tanganyika upya. Lissu anatakiwa aanzie pale alipokosea Nyerere ili nchi ipone na kuweza kuendelea kama nchi zingine.
Tundu Lissu ni mwanaharakati lakini mwanasheria mzuri na kwa maoni yangu angefaa zaidi kwenye mambo ya sheria,mambo ya utawala na ufuatiliaji. Kumpa urais, kuna hatari ya kumfunga mdomo kama ilivyo kwa Mwambukusi hivi sasa.
Vyama vya upinzani vitafute mtu yeyote mwenye uwezo na nia ya kulitumikia taifa hili akiwa na umri mdogo wa miaka 35-45 ndio agombee Urais. Kwa hakika ikifanyika hivyo nitatoka kwenda kupiga kura.... Otherwise: No reform, No election!!.