Wito wangu kwa Wanawake: Achaneni kabisa na usafiri wa bodaboda, sio salama kwenu

Wito wangu kwa Wanawake: Achaneni kabisa na usafiri wa bodaboda, sio salama kwenu

Ukion bodaboda
-kavaa kikaputula kinaishia mapajani,
-amesokota nywele,
-anavindala,
-boda yake ameweka nyimbo za singeli
-hana helmet

Ukipanda hiyo boda na wewe unakuwa mpumbavu. Maana hao vijana huwa wakishapanda kwenye boda utakuta anakaa upande hivi. Hapo utafurahia show.
Mim kuna dogo aliniendesha alifanya overtake kiasi kwamba angechelewa just a second ndo ingekuwa mwisho. Baada ya pale nikamwambia sikulipi hela yako ya nishushe,

Bora bodaboda wa bolt hawa mostly naonaga wanajielewa
 
Matumizi sahihi ya boda boda ni haya...
1. Usafiri huo utumike nje ya mji.
2. Barabara za vumbi/changarawe.
3. Mwendo wa polepole (speed isiyozidi 30km/hour)
4. Vaa kofia ngumu.
5. Dereva aliyefuzu.

Ninakuhakikishia, mambo hayo matano yakifuatwa kikamilifu, vifo vinavyotokana na boda boda vitafutika, ajali mbaya zitafutika.
 
Ubaya mwingine wa bodaboda anaweza kuwa makini ila gari ikamvamia. Tatizo wewe ndio body ya bodaboda.
 
Kuna mwanafunzi wangu alilazwa ICU miezi 6 kisa boda boda... Kikubwa kapona japo kabaki na kovu kwenye komwe.
Alafu wengi huwa wanawahi kwenda kugongwa tu hamna cha maana, umalaya ndo unawaponza.
 
NI saa saba na dakika tano, mataa ya Mwenge, ajali mbaya sana inatokea, mabinti wawili wakiwa kwenye bodaboda, wanapata ajali mbaya sana na kufariki dunia hapohapo.

Last week nilihudhuria msiba wa mrembo mmoja aliyefariki kwenye Kona ya Target akielekea Juliana, alikuwa kwenye bodaboda.

Sweet Ray rafiki yangu, kapata ulemavu wa kudumu akiwa kwenye bodaboda.

Wadada mkiwa kwenye bodaboda mnajiona mko salama sana, mnabinua vijikalio vyenu huku mkipekenyua kurasa za instagram.

Upekuzu huo huwapelekeni mbali kiasi kwamba mnasahau kuwa mna jukumu la kumuongoza dereva na chombo chake, maana madereva wa bodaboda ni bangi na dabokiki paseee.

Matokeo yake mnajikuta tayari ajali Isha wameza.

With wangu kwenu:-
1. Usimchukue dereva MWENYE kiduku au turn dread, tafuta dereva mtu mzima mwenye staha zake.

2. Usimchukue dereva MWENYE kuvaa ndala, tafuta mwenye viatu, utanishukuru baadae.

3. Mwambie mapema dereva aende mwendo wa pole hata Kama una haraka, ni salama zaidi kwako.

4. Usitumie simu kwenye bodaboda, itakuondolea concentration, utashindwa kumuongoza dereva.

5. Vaa kofia ngumu, usipande bodaboda ambayo haina kofia, na ni lazima uvae kofia.

6. Sali kabla hujaanza Safari yako, mwombe Mungu akutangulie na akufikishe salama.

Wishing you all the best
Watu wa chadema wako very constructive kwenye society Yani hata mada zao ni zenye kujenga jamii. Sasa ngoja wake nzi wa kijani; mada zao wao ni....
1.Lissu auwawe tu.
2.Mbowe anyongwe.
3.Hakuna Kama mama ssh kule unga.
Nk .
Yani mada za ujingaujinga tu.
 
Just imagine ndiyo kamtoko hivii, umetia kalkiti yako, na ka way pembeni anaelewa Depal ile namna, nywele inameremeta hivii, dereva anakupa helmet lake chafu utavaa..?
Naelewa dada si ndiyo mambo yetu 🤣 nini helmet chafu? Kitendo tu cha kunipa helmet ananivuruga maana nikiivaa tu nywele itavurugika mawimbi.

Na venye wako na tabia mbaya? Ukimwambia itaniharibia nywele inakwambia we ishike tu ukikamatwa shauri zako 😆
 
Ahsante kutukumbusha, hapo pa helmet umenigusa Mimi kabisa, Jana tu nimegoma kuivaa nimetengeneza tunywele twangu naanzaje kuziharibu na helmet jamani.!?
Ila anyways, tutajitahidi kwa usalama wetu ila nyingi huwa chafu sana jamani..!

NB; nanyoa, siyo nywele za bandia msije nishambulia..!
Dada ako ka style ka jana kanifate nyuma pls.
 
NI saa saba na dakika tano, mataa ya Mwenge, ajali mbaya sana inatokea, mabinti wawili wakiwa kwenye bodaboda, wanapata ajali mbaya sana na kufariki dunia hapohapo.

Last week nilihudhuria msiba wa mrembo mmoja aliyefariki kwenye Kona ya Target akielekea Juliana, alikuwa kwenye bodaboda.

Sweet Ray rafiki yangu, kapata ulemavu wa kudumu akiwa kwenye bodaboda.

Wadada mkiwa kwenye bodaboda mnajiona mko salama sana, mnabinua vijikalio vyenu huku mkipekenyua kurasa za instagram.

Upekuzu huo huwapelekeni mbali kiasi kwamba mnasahau kuwa mna jukumu la kumuongoza dereva na chombo chake, maana madereva wa bodaboda ni bangi na dabokiki paseee.

Matokeo yake mnajikuta tayari ajali Isha wameza.

With wangu kwenu:-
1. Usimchukue dereva MWENYE kiduku au turn dread, tafuta dereva mtu mzima mwenye staha zake.

2. Usimchukue dereva MWENYE kuvaa ndala, tafuta mwenye viatu, utanishukuru baadae.

3. Mwambie mapema dereva aende mwendo wa pole hata Kama una haraka, ni salama zaidi kwako.

4. Usitumie simu kwenye bodaboda, itakuondolea concentration, utashindwa kumuongoza dereva.

5. Vaa kofia ngumu, usipande bodaboda ambayo haina kofia, na ni lazima uvae kofia.

6. Sali kabla hujaanza Safari yako, mwombe Mungu akutangulie na akufikishe salama.

Wishing you all the best

Naunga mkono hoja ila hatari ya boda boda siyo gender sensitive.

Hatari iko kwa wote.

Muhimu:

1. Mwendo mdogo mdogo
2. Aende kama unavyotaka wewe muda wote
3. Helmet ni lazima
4. Dereva awe mtu mzima au mdada
 
Ahsante uncle Bujibuji kwa kutukumbusha pia ila ajali haina kinga, Ni kuomba tu Mwenyezi Mungu atuepushie.

We've to take cautious, maana najua route za Toyo ni nyingi kuliko za Hiace. Carleen
 
Back
Top Bottom