Wito wangu kwa Wanawake: Achaneni kabisa na usafiri wa bodaboda, sio salama kwenu

Hivi nyie madereva bodaboda, kuendesha rough hizo pikipiki ni sifa nzuri kwenu? Kila siku ajali za bodaboda zinazopelekea vifo na ulemavu wa kudumu, hivi mnajisikiaje nyie kuwa wasababishaji? Acheni sifa za kijinga, endesha kwa ustaarabu kwa manufaa ya abiria, wewe mwenyewe na chombo chako. Kuendesha rough ni ushamba wa kiwango cha juu.
 
Nilinisurika na ajali ya bodaboda

,Nilivaa gauni ndefu lilikwama yaani lilijiviliga nikawa nahisi navutwa kwa nyuma,

Raia wakaniambia ninabahati sana ningesababisha ajali mbaya

Tokea siku hiyo naogopa bora nitembee au nipande bajaji.
 
Nilipata ajali tarehe 29.4.2021 nikavunjika mguu wa kulia,mpaka leo nipo kitandani

Dereve wa bodaboda alifariki palepale, kuja kichunguza naambiwa alikua kalewa pombe.
Duuh,Pole sana aisee
 
Kila unapokuwa barabarani tambua kuwa kuna ajari ,uwe alert na hali yoyote inayoweza kupelekea ajari.boda boda wengi hawana tahadhari wanapo kuwa barabarani.

Usiendeshwe mwendo zaidi ya 30 kph .
Kuomba Mungu akuepushe na hatari zote za kiroho na kimwili na kukuepusha na kifo cha gafla.

Tuwe wasafi ki mwili na kiroho,ili tupate msaada wa kuepushwa na mabaya tunapokuwa katika hali tete ambazo kibinadam si lahisi kuzitambua.
 
Muda mwingine naona pikipiki ndio kama zina mapepo maana mtu mwingine mstaarabu tu akishika pikipiki anaenda kama kichaa.
Kuna siku niko maeneo fulani barabara ya vumbi nikapishana na bodaboda anaenda mbio anaacha vumbi tu. Nacheck side mirror naona pikipiki iko kwake dereva yupo kwake. Katimua vumbi mpaka akawa haoni njia.
Hiki chombo cha usafiri kinasaidia kwenye emergencies lakini kama mleta mada alivyosema yatupasa kua makini. Ulinzi unaanzia kwako.
 
Uzi umejaa busara tupu! Binafsi nimekuelewa BUJI, na nitaufanyia kazi ushauri wako!
 
[emoji1756][emoji1756][emoji1756]
 
Wazungu tunasema well said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…