Wanabodi
Nimemsikiliza TAL kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV kuhusu falsafa yake ya No Reforms No Election.
View: https://www.youtube.com/live/u5PkOqrHdZI?si=Mtma0U4QBfJ8TJ6x
Sawa. Umeona mapungufu gani yanayohitaji maboresho...?
Japo hakuna ubishi kuhusu umahiri wa TAL kama mwanasheria, mwanasiasa, mbunge, mnadhimu mkuu wa upinzani, M/Mwenyekiti wa Chadema, lakini TAL kama Mwenyekiti wa Chadema, anahitaji msaada mkubwa kusaidiwa na watu wenye uwezo
Wamekuambia hawa watu wa kushauriana naye humo CHADEMA hawapo? Unajua anashauriana na kina nani? Na wewe kipimo chako cha kwamba huyu ana uwezo na huyu hana uwezo wa kumshauri Tundu Lissu na CHADEMA kwa ujumla ni kipi..?
ili aweze kubadilika kutoka TAL mwanaharakati into TAL Stateanship!.
Hivi Hayati Mwl. Julius K. Nyerere angekuwa "stateman" kwa wakoloni badala ya kuendesha siasa za harakati za kuikomboa Tanganyika toka ukoloni wa wazungu wa Kiingereza, kwa dhana yako ya "u - stateman" si mpka leo tungekuwa bado ktk aina hiyo ya ukoloni..?
Katika nchi iliyojaa ukandamizaji, kupuuza haki za binadamu, kutoheshimu maamuzi ya wananchi ktk maswala ya uongozi, resentment, kutesa na kuua wapinzani wako kisiasa (udikteta) nk, huhitaji statemen kujimboa bali unahitaji wanaharakati aggressive, wenye uelewa na ufahamu ulioshiba na majasiri...
Ili kuitiisha serikali ya CCM kuheshimu matakwa ya wananchi, huhitaji u - stateman bali unawahitaji activists wengi wa kisiasa, kisheria, kiuchumi, kijamii, haki za binadamu nk...
Chini ya serikali za kikandamizaji na onevu kama hii ya Tanzania, kama hujaitwa mchochezi, mhaini nk wewe bado si mpambanaji na ni ngumu sana kuung'oa utawala wa aina ya CCM hapa Tanganyika...!!
TAL lazime abadilike kuachana na vibwagizo vya uanaharakati
Ni vipi hivyo?
Je, ni hiki cha NO REFORMS, NO ELECTION? Ungependa CHADEMA wawe na kibwagizo gani? Hiki cha: "JAMHURI YA MUUNGANO, KAZI IENDELEE.??" Hiki ndo kinaitwaje kweli? Non utopian politics au..?
into real politics vinginevyo anakwenda kuizamisha Chadema kwenye a pit latrine!.
From your understanding, what are the real politics? Za kupora uchaguzi? Kuiba kura? Kuteka na kuua wapinzani wako kisiasa?
Mimi hapa kwa mbaaali nakuona kama mtu uliye kwenye "panic mode" na andiko hili linawakilisha hofu ya watawala na CCM ya ujio wa mtu huyu..!!!
Usijidanganye brother
Pascal Mayalla , CHADEMA shall never go into the pit of latrine, rather through this direction, CHADEMA is cruising into the glorious heights of politics...!
Wanaokwenda kwenye shimo la choo ni hawa watawala wenu wasio na kibali cha Mungu Yehova na CCM yao...
Kama huamini, wewe kaa pembeni paleeee 👉🏻👉🏻👉🏻chini ya mti wa mretemu ukila popcorn yako, na subiri hapohapo ili uone kwa macho yako jinsI watu wanavyoanguka anguko kuu....!
Hivyo hili ni bandiko la wito, kwa Watanzania wowote wazalendo wa kweli wa nchi hii, na wenye mapenzi mema na nchi yetu, wenye uwezo, wa kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL ili aweze, na kuisaidia Chadema ili iweze to play the real politics of reality, hii falsafa ya TAL ya "No Reforms No Election" is not real!, ni utopian politics!.
Nyie mna mapenzi mema na Tanzania?
Tangu lini wapenda uonevu, chuki, unyanyasaji, wauaji, wezi, wanaochukia haki na kupenda dhuluma wakawa ni watu wazalendo..?
Stop this nonsense brother...!!!!
Kwani unaona ugumu gani kuuona ukweli wa hoja za CHADEMA zinazochagizwa na kauli mbiu ya NO REFORMS, NO ELECTION...?
Kwanini hamjibu hoja badala yake mnakimbilia kumjadili mtu..?
BAADHI YA HOJA ZA CHADEMA NI HIZI:
1. Kutokuwepo kwa usawa wa mgawanyo wa majimbo ya uchacguzi wa wabunge. Mfano inakuwaje Zanzibar yenye wapiga kura 500,000 iwe na majimbo 50 ya uchaguzi huku DSM Tanganyika iliyo na wapiga kura 3,000,000 iwe na majimbo 10 tu ya uchaguzi? Usawa uko wapi hapo.???
2. Kwanini Mwenyekiti wa CCM ambaye automatic huwa mgombea U - Rais ndiye ateue wajumbe wa NEC ili wasimamie uchaguzi ambaye naye ni mshiriki kama mgombea? Does it make sense to you..?
3. Inawezekana vipi wagombea wasio wa chama atokacho Mwenyekiti wa CCM na Rais wote wawe wanajua kusoma na kuandika, wakosee kujaza fomu ya kuomba uteuzi wa kugombea ubunge, udiwani, uenyekiti wa kijiji, mtaa au kitongoji na hivyo 95% wakaenguliwa kwa kigezo hicho wakati wagombea wote wa CCM wakawa wanajua kusoma na kuandika vizuri, wakajaza fomu vizuri na 100% wakateuliwa kugombea nafasi hizohizo bila mizengwe? Je, hawa wote wa CCM na CHADEMA ama vyama vingine si wamesoma shule hizohizo walizosoma hawa wa CCM? Wakafundishwa na walimu walewale? Haya yote yana make sense kweli kwako au mzee umeamua kuwa chawa kabisa kwa uwazi na ujinga tu?
##Mbona nyie CCM hamjibu hoja hizi badala yake mnamshambulia Tundu Lissu as a person?
##Na hata mkiamua kumshambulia Lissu kama mtu badala ya hoja zake kwa akili zako unadhani mtaweza kuzima kiu ya mabadiliko waliyonayo watu baada ya kuwa wamemwelewa Tundu Lissu na CHADEMA..?
Think twice, before indulging yourself into deep darkness of stupidity and ignorance...
TAL alipoulizwa maandalizi ya uchaguzi, amesema Chadema haifanyi maandalizi yoyote bila reforms ni no election!.
Yes. What's wrong na jibu hilo..?
Maana msimamo ni: ILI TUSHIRIKI UCHAGUZI, NI SHARTI NA NI LAZIMA KAMA NCHI TUKAE CHINI TUFANYE MABADILIKO YA KISHERIA, KANUNI NA KIKATIBA ILI KUTENGENEZA MFUMO MPYA WA CHAGUZI ZETU ILI ZIWE HURU, ZA WAZI NA ZA HAKI KWA KILA MSHIRIKI..
Hii ndio exactly maana ya NO REFORMS, NO ELECTION....
Sasa unataka wajiandae kwa uchaguzi upi maana zilizofanyika 2019, 2020 na 2024 hazikuwa chaguzi zile bali ni uchafu mtupu? Au wewe hukuona hayo?
Nauliza tena: wajiandae kwa chaguzi upi na ili iweje? Wakaeunguliwe? Wakapigwe na polisi na kuuwawa? Ili iweje hasa...????
Hizi ni utopian politics,
Nina mashaka hata kama unaelewa maana ya hiki ulichokiandika...
sii TAL wala Chadema wana uwezo wa kuzuia uchaguzi Mkuu usifanyike!.
Really..?
Huamini siyo? Endelea kutoamini lakini mwisho wa siku haitakuwa kutoamini tena, bali UTAONA KWA MACHO YAKO...!!
Mmoja wa washauri hao wa bure wa kujitolea ni huyu Mwana JF Maarufu sana, Mkuu
Mzee Mwanakijiji , msikilizeni hapa amewashauri nini Chadema na amemshauri nini TAL.
View: https://youtu.be/GUjpxNTSdig Ushauri huu ulitolewa kwa TAL miaka 5 iliyopita, Chadema mtafuteni huyu mtu atawasaidia sana!.
Huyu na wewe mna tofauti gani..?
Tayari mmeshakodishwa na Abdul na mama yake a.k.a Chura Kiziwi wa Kizimkazi - Zanzibar , mmeuza utu wenu kwa vipande vya fedha au kwa ujinga tu ili mtetee dhuluma na uonevu...!!
Mimi pia kwa upande wangu, nimeisha wasaidia sana Chadema kwa kuwashauri,
- Nilimshauri Lissu aache uanaharakati aonyeshe statemamship JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship
- 2015 Chadema ilikuwa waingie ikulu lakini kuna makosa waliyafanya, Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... sasa Chadema wana fursa tena ambayo imejotokeza kama zali, wasiridie makosa!
- Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua hapa niliwashauri Chadema namna ya kujinasua, ushauri wangu umefuatwa ndio Chadema hii inayoiona sasa, umeutambua uchaguzi na sio uchavuzi, imelitambua Bunge, imemtambua rais, sasa Chadema inalamba ruzuku ndio hii ipo!.
- Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?
- Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane! hapa Chadema walikuwa hawamtambui mbunge wake, baada ya ushauri huu, sasa wanamtambua!.
- Ushauri wa bure: CHADEMA iachane na issue ya Wabunge wake 19, iwasamehe waendelee na Ubunge wao. Kwa muda uliobakia kuwatengua hakuna maslahi yoyote! hapa nimewaombea msamaha hawa wabunge, Chadema haina wanawake wowote wa calibre ya Halima Mdee, Ester Bulaya na Esta Matiko!.
- Uchaguzi 2020 - Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...
- Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini hapa niliilaumu Chadema hawajui wanataka nini na watapataje, hata sasa Chadema chini ya Lissu, bado hawajitambui!.
- CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena! hapa niliwalaumu Chadema hawajipangi!, hadi sasa chini ya TAL, Chadema haijajipanga na isiposaidiwa, haijipangi!. Huu ni mwaka wa uchaguzi, TAL anazungumzia no reforms no election, amepanga kusimamisha uchaguzi kwa maandamano!. Uchaguzi mkuu wa 2025 ni fursa kwa TAL na Chadema, badala ya kupanga mikakati ya kuchangamkia fursa, watu wanapanga kususia!.
- Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition? hili lilikuwa swali la 2020, hata hii 2025 Chadema hawajabadilika!, 2025 Chadema ina fursa, isipobadilika na kuchangamkia fursa, 2025 ni CCM tena!.
- Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli! Kama JPM alikuwa Dikiteta... TAL ni zaidi ya JPM!.
- Elections 2015 - CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu! hii ni hoja ya udikiteta Chadema, TAL ni kama JPM, hivyo TAL akipewa nchi 2025, Keko, Ukonga na Segerea kutafurika!.
- Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA hii ni moja ya Sifa njema za TAL
Natoa wito, kwa watu wowote wenye uwezo, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, uchaguzi mkuu wa 2025 ni fursa adhimu kwa Chadema kuichangamkia.
TAL na Chadema Wasaidiwe!.
Paskali
Mr
Pascal Mayalla, mengine yote ni ujinga na upuuzi mtupu as for now...
Hoja ni lazima iwe:
TUTAWASAIDIAJE CHADEMA NA TUNDU LISSU KUISHIRIKI NA KUITEKELEZA MOVEMENT YA KUDAI MABADILIKO YA MFUMO WA UTAWALA WA NCHI HII KWA KUPIGANIA MABADILIKO YA MFUMO BORA WA UCHAGUZI ULIO HURU, HAKI NA WAZI KWA KAULI MBIU YA NO REFORMS, NO ELECTION..??
Achana na utopian thoughts zako za kutaka tuendelee kukandamizwa na kulazwa mavumbini na CCM...!!