Wito: Watu Wenye Uwezo, Tujitokeze Tujitolee Kumsaidia TAL na Kuisaidia Chadema to Play Real Politics, No Reforms No Election ni Utopian Politics!.

Wito: Watu Wenye Uwezo, Tujitokeze Tujitolee Kumsaidia TAL na Kuisaidia Chadema to Play Real Politics, No Reforms No Election ni Utopian Politics!.

Wanabodi

Nimemsikiliza TAL kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV kuhusu falsafa yake ya No Reforms No Election.
View: https://www.youtube.com/live/u5PkOqrHdZI?si=Mtma0U4QBfJ8TJ6x

Japo hakuna ubishi kuhusu umahiri wa TAL kama mwanasheria, mwanasiasa, mbunge, mnadhimu mkuu wa upinzani, M/Mwenyekiti wa Chadema, lakini TAL kama Mwenyekiti wa Chadema, anahitaji msaada mkubwa kusaidiwa na watu wenye uwezo, ili aweze kubadilika kutoka TAL mwanaharakati into TAL Stateanship!.

TAL lazime abadilike kuachana na vibwagizo vya uanaharakati, into real politics vinginevyo anakwenda kuizamisha Chadema kwenye a pit latrine!.

Hivyo hili ni bandiko la wito, kwa Watanzania wowote wazalendo wa kweli wa nchi hii, na wenye mapenzi mema na nchi yetu, wenye uwezo, wa kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL ili aweze, na kuisaidia Chadema ili iweze to play the real politics of reality, hii falsafa ya TAL ya "No Reforms No Election" is not real!, ni utopian politics!.
TAL alipoulizwa maandalizi ya uchaguzi, amesema Chadema haifanyi maandalizi yoyote bila reforms ni no election!.
Hizi ni utopian politics, sii TAL wala Chadema wana uwezo wa kuzuia uchaguzi Mkuu usifanyike!.

Mmoja wa washauri hao wa bure wa kujitolea ni huyu Mwana JF Maarufu sana, Mkuu Mzee Mwanakijiji , msikilizeni hapa amewashauri nini Chadema na amemshauri nini TAL.
View: https://youtu.be/GUjpxNTSdig Ushauri huu ulitolewa kwa TAL miaka 5 iliyopita, Chadema mtafuteni huyu mtu atawasaidia sana!.

Mimi pia kwa upande wangu, nimeisha wasaidia sana Chadema kwa kuwashauri,

Natoa wito, kwa watu wowote wenye uwezo, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, uchaguzi mkuu wa 2025 ni fursa adhimu kwa Chadema kuichangamkia.

TAL na Chadema Wasaidiwe!.

Paskali

Paskali, kwa nini kushinikiza KURA ZETU KUHESABIWA NA KUHESABIWA KWA HAKI NA UWAZI kuwe swala la KUFIKIRIKA?
Wewe hutaki KURA ZIHESABIWE KWA uwazi?
 
Wanabodi

Nimemsikiliza TAL kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV kuhusu falsafa yake ya No Reforms No Election.
View: https://www.youtube.com/live/u5PkOqrHdZI?si=Mtma0U4QBfJ8TJ6x

Sawa. Umeona mapungufu gani yanayohitaji maboresho...?
Japo hakuna ubishi kuhusu umahiri wa TAL kama mwanasheria, mwanasiasa, mbunge, mnadhimu mkuu wa upinzani, M/Mwenyekiti wa Chadema, lakini TAL kama Mwenyekiti wa Chadema, anahitaji msaada mkubwa kusaidiwa na watu wenye uwezo
Wamekuambia hawa watu wa kushauriana naye humo CHADEMA hawapo? Unajua anashauriana na kina nani? Na wewe kipimo chako cha kwamba huyu ana uwezo na huyu hana uwezo wa kumshauri Tundu Lissu na CHADEMA kwa ujumla ni kipi..?
ili aweze kubadilika kutoka TAL mwanaharakati into TAL Stateanship!.
Hivi Hayati Mwl. Julius K. Nyerere angekuwa "stateman" kwa wakoloni badala ya kuendesha siasa za harakati za kuikomboa Tanganyika toka ukoloni wa wazungu wa Kiingereza, kwa dhana yako ya "u - stateman" si mpka leo tungekuwa bado ktk aina hiyo ya ukoloni..?

Katika nchi iliyojaa ukandamizaji, kupuuza haki za binadamu, kutoheshimu maamuzi ya wananchi ktk maswala ya uongozi, resentment, kutesa na kuua wapinzani wako kisiasa (udikteta) nk, huhitaji statemen kujimboa bali unahitaji wanaharakati aggressive, wenye uelewa na ufahamu ulioshiba na majasiri...

Ili kuitiisha serikali ya CCM kuheshimu matakwa ya wananchi, huhitaji u - stateman bali unawahitaji activists wengi wa kisiasa, kisheria, kiuchumi, kijamii, haki za binadamu nk...

Chini ya serikali za kikandamizaji na onevu kama hii ya Tanzania, kama hujaitwa mchochezi, mhaini nk wewe bado si mpambanaji na ni ngumu sana kuung'oa utawala wa aina ya CCM hapa Tanganyika...!!
TAL lazime abadilike kuachana na vibwagizo vya uanaharakati
Ni vipi hivyo?

Je, ni hiki cha NO REFORMS, NO ELECTION? Ungependa CHADEMA wawe na kibwagizo gani? Hiki cha: "JAMHURI YA MUUNGANO, KAZI IENDELEE.??" Hiki ndo kinaitwaje kweli? Non utopian politics au..?
into real politics vinginevyo anakwenda kuizamisha Chadema kwenye a pit latrine!.
From your understanding, what are the real politics? Za kupora uchaguzi? Kuiba kura? Kuteka na kuua wapinzani wako kisiasa?

Mimi hapa kwa mbaaali nakuona kama mtu uliye kwenye "panic mode" na andiko hili linawakilisha hofu ya watawala na CCM ya ujio wa mtu huyu..!!!

Usijidanganye brother Pascal Mayalla , CHADEMA shall never go into the pit of latrine, rather through this direction, CHADEMA is cruising into the glorious heights of politics...!

Wanaokwenda kwenye shimo la choo ni hawa watawala wenu wasio na kibali cha Mungu Yehova na CCM yao...

Kama huamini, wewe kaa pembeni paleeee 👉🏻👉🏻👉🏻chini ya mti wa mretemu ukila popcorn yako, na subiri hapohapo ili uone kwa macho yako jinsI watu wanavyoanguka anguko kuu....!
Hivyo hili ni bandiko la wito, kwa Watanzania wowote wazalendo wa kweli wa nchi hii, na wenye mapenzi mema na nchi yetu, wenye uwezo, wa kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL ili aweze, na kuisaidia Chadema ili iweze to play the real politics of reality, hii falsafa ya TAL ya "No Reforms No Election" is not real!, ni utopian politics!.
Nyie mna mapenzi mema na Tanzania?

Tangu lini wapenda uonevu, chuki, unyanyasaji, wauaji, wezi, wanaochukia haki na kupenda dhuluma wakawa ni watu wazalendo..?

Stop this nonsense brother...!!!!

Kwani unaona ugumu gani kuuona ukweli wa hoja za CHADEMA zinazochagizwa na kauli mbiu ya NO REFORMS, NO ELECTION...?

Kwanini hamjibu hoja badala yake mnakimbilia kumjadili mtu..?

BAADHI YA HOJA ZA CHADEMA NI HIZI:

1. Kutokuwepo kwa usawa wa mgawanyo wa majimbo ya uchacguzi wa wabunge. Mfano inakuwaje Zanzibar yenye wapiga kura 500,000 iwe na majimbo 50 ya uchaguzi huku DSM Tanganyika iliyo na wapiga kura 3,000,000 iwe na majimbo 10 tu ya uchaguzi? Usawa uko wapi hapo.???

2. Kwanini Mwenyekiti wa CCM ambaye automatic huwa mgombea U - Rais ndiye ateue wajumbe wa NEC ili wasimamie uchaguzi ambaye naye ni mshiriki kama mgombea? Does it make sense to you..?

3. Inawezekana vipi wagombea wasio wa chama atokacho Mwenyekiti wa CCM na Rais wote wawe wanajua kusoma na kuandika, wakosee kujaza fomu ya kuomba uteuzi wa kugombea ubunge, udiwani, uenyekiti wa kijiji, mtaa au kitongoji na hivyo 95% wakaenguliwa kwa kigezo hicho wakati wagombea wote wa CCM wakawa wanajua kusoma na kuandika vizuri, wakajaza fomu vizuri na 100% wakateuliwa kugombea nafasi hizohizo bila mizengwe? Je, hawa wote wa CCM na CHADEMA ama vyama vingine si wamesoma shule hizohizo walizosoma hawa wa CCM? Wakafundishwa na walimu walewale? Haya yote yana make sense kweli kwako au mzee umeamua kuwa chawa kabisa kwa uwazi na ujinga tu?

##Mbona nyie CCM hamjibu hoja hizi badala yake mnamshambulia Tundu Lissu as a person?

##Na hata mkiamua kumshambulia Lissu kama mtu badala ya hoja zake kwa akili zako unadhani mtaweza kuzima kiu ya mabadiliko waliyonayo watu baada ya kuwa wamemwelewa Tundu Lissu na CHADEMA..?

Think twice, before indulging yourself into deep darkness of stupidity and ignorance...

TAL alipoulizwa maandalizi ya uchaguzi, amesema Chadema haifanyi maandalizi yoyote bila reforms ni no election!.
Yes. What's wrong na jibu hilo..?

Maana msimamo ni: ILI TUSHIRIKI UCHAGUZI, NI SHARTI NA NI LAZIMA KAMA NCHI TUKAE CHINI TUFANYE MABADILIKO YA KISHERIA, KANUNI NA KIKATIBA ILI KUTENGENEZA MFUMO MPYA WA CHAGUZI ZETU ILI ZIWE HURU, ZA WAZI NA ZA HAKI KWA KILA MSHIRIKI..

Hii ndio exactly maana ya NO REFORMS, NO ELECTION....

Sasa unataka wajiandae kwa uchaguzi upi maana zilizofanyika 2019, 2020 na 2024 hazikuwa chaguzi zile bali ni uchafu mtupu? Au wewe hukuona hayo?

Nauliza tena: wajiandae kwa chaguzi upi na ili iweje? Wakaeunguliwe? Wakapigwe na polisi na kuuwawa? Ili iweje hasa...????
Hizi ni utopian politics,
Nina mashaka hata kama unaelewa maana ya hiki ulichokiandika...
sii TAL wala Chadema wana uwezo wa kuzuia uchaguzi Mkuu usifanyike!.
Really..?

Huamini siyo? Endelea kutoamini lakini mwisho wa siku haitakuwa kutoamini tena, bali UTAONA KWA MACHO YAKO...!!
Mmoja wa washauri hao wa bure wa kujitolea ni huyu Mwana JF Maarufu sana, Mkuu Mzee Mwanakijiji , msikilizeni hapa amewashauri nini Chadema na amemshauri nini TAL.
View: https://youtu.be/GUjpxNTSdig Ushauri huu ulitolewa kwa TAL miaka 5 iliyopita, Chadema mtafuteni huyu mtu atawasaidia sana!.

Huyu na wewe mna tofauti gani..?

Tayari mmeshakodishwa na Abdul na mama yake a.k.a Chura Kiziwi wa Kizimkazi - Zanzibar , mmeuza utu wenu kwa vipande vya fedha au kwa ujinga tu ili mtetee dhuluma na uonevu...!!
Mimi pia kwa upande wangu, nimeisha wasaidia sana Chadema kwa kuwashauri,

Natoa wito, kwa watu wowote wenye uwezo, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, uchaguzi mkuu wa 2025 ni fursa adhimu kwa Chadema kuichangamkia.

TAL na Chadema Wasaidiwe!.

Paskali
Mr Pascal Mayalla, mengine yote ni ujinga na upuuzi mtupu as for now...

Hoja ni lazima iwe:

TUTAWASAIDIAJE CHADEMA NA TUNDU LISSU KUISHIRIKI NA KUITEKELEZA MOVEMENT YA KUDAI MABADILIKO YA MFUMO WA UTAWALA WA NCHI HII KWA KUPIGANIA MABADILIKO YA MFUMO BORA WA UCHAGUZI ULIO HURU, HAKI NA WAZI KWA KAULI MBIU YA NO REFORMS, NO ELECTION..??

Achana na utopian thoughts zako za kutaka tuendelee kukandamizwa na kulazwa mavumbini na CCM...!!
 
Anayemshauri Lissu alishindwa kuwashawishi wajumbe hata wampe kura sawa na idadi ya vidole vyake vya mikono.
images - 2025-01-23T123355.397.jpeg
 
Wanabodi

Nimemsikiliza TAL kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV kuhusu falsafa yake ya No Reforms No Election.
View: https://www.youtube.com/live/u5PkOqrHdZI?si=Mtma0U4QBfJ8TJ6x

Japo hakuna ubishi kuhusu umahiri wa TAL kama mwanasheria, mwanasiasa, mbunge, mnadhimu mkuu wa upinzani, M/Mwenyekiti wa Chadema, lakini TAL kama Mwenyekiti wa Chadema, anahitaji msaada mkubwa kusaidiwa na watu wenye uwezo, ili aweze kubadilika kutoka TAL mwanaharakati into TAL Stateanship!.

TAL lazime abadilike kuachana na vibwagizo vya uanaharakati, into real politics vinginevyo anakwenda kuizamisha Chadema kwenye a pit latrine!.

Hivyo hili ni bandiko la wito, kwa Watanzania wowote wazalendo wa kweli wa nchi hii, na wenye mapenzi mema na nchi yetu, wenye uwezo, wa kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL ili aweze, na kuisaidia Chadema ili iweze to play the real politics of reality, hii falsafa ya TAL ya "No Reforms No Election" is not real!, ni utopian politics!.
TAL alipoulizwa maandalizi ya uchaguzi, amesema Chadema haifanyi maandalizi yoyote bila reforms ni no election!.
Hizi ni utopian politics, sii TAL wala Chadema wana uwezo wa kuzuia uchaguzi Mkuu usifanyike!.

Mmoja wa washauri hao wa bure wa kujitolea ni huyu Mwana JF Maarufu sana, Mkuu Mzee Mwanakijiji , msikilizeni hapa amewashauri nini Chadema na amemshauri nini TAL.
View: https://youtu.be/GUjpxNTSdig Ushauri huu ulitolewa kwa TAL miaka 5 iliyopita, Chadema mtafuteni huyu mtu atawasaidia sana!.

Mimi pia kwa upande wangu, nimeisha wasaidia sana Chadema kwa kuwashauri,

Natoa wito, kwa watu wowote wenye uwezo, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, uchaguzi mkuu wa 2025 ni fursa adhimu kwa Chadema kuichangamkia.

TAL na Chadema Wasaidiwe!.

Paskali

Lisu siasa hauwezi anaweza uharakati tu.CHADEMA ya sasa imejaa vibaka na matapeli wa kisiasa
 
Nilipoanza kusoma nikaona umeanza kwa kumpa maujiko na vyeo kibao, nikajua tu mwisho utamsagia kunguni mazee....😜
Ila TAL anapaswa kupunguza uanaharakati ili ajikite kwenye siasa na hoja pasipo na jazba..😊
Kuna siasa za upinzani bila harakati hasa kwa nchi zinazoendelea ?
 
CCM ni chama imara na chenye mfumo imara wa kiuongozi. Ni Chama ambacho kwa kila jambo kuna utaratibu wake wa kulishughulikia na kulitatua kwa mujibu wa katiba ,sheria,kanuni, miongozo na taratibu za chama
Huo mfumo imara ndio ule wa kuingiza kura zilizopigwa kwenye masanduku kabla ya zoezi la upigaji kura eh?

Mfumo imara ni wa kufukuza mwanachama akisema mgombea urais kapatikana bila utaratibu.

Hakika ni mfumo imara maana watoto wao wanasoma mitaala ya U.K huku nyie watoto wenu wakisomea mtaala unaowafundisha kusubiri ajira na ajira hazipo hivyo mnageukia uchawa wakati watoto wao wako kazini kwenye ofisi za ubalozi na mashirika ya kigeni.
images (36).jpeg
 
Hakuna mahali popote ambapo Mungu aneagiza tumsamehe Shetani

Lingine usilolijua ni hili, Lowassa hakuletwa na Mbowe, ni Kamati Kuu ndio ilimkubalia kugombea Urais kupitia Chadema, Mbowe hana mamlaka hiyo wala hakuwahi kuwa nayo
Lissu anasema aliletwa na Slaa. Lakini yote hayo hayajalishi. Chama cha Chadema kiliziba pua na kumkubali mtu waliyemuita fisadi papa kuwa mgombea wao wa urais.
Hata sasa hivi, kwa kutumia busara zake, Kamati Kuu ya Chama inaweza kukubali kushirikiana na wakina Halima huku wakiziba pua zao. Mimi huo ushetani wa wakina Halima hata siuoni. Lakini huu ni ushauri tu. CDM itafanya kile ambacho kinaona ni sahihi.

Amandla...
 
Lucas Mwashambwa , Tlaatlaah , Pascal Mayalla
Natamani kuona hizi constructive criticism muwe mnazifanya na huko chamani kwenu CCM.

Muwe unakemea maovu ya huko pia kuliko Ile tabia ya kusifia kupita kiasi haipendezi.

Nawasiliana Sana pia kila lakheli kwenu.

Kwa Sasa kijijini MPUMBWI.
Gentleman,
always mbona tuna jitahidi sana kuicriticize CCM, chadema na vyama vingine vya siasa in a very constructive way?

hata jana nadhani na leo pia nimeeleza wazi kwamba chadema bado kuna fukuto la uhasama miongoni mwa viongoz wake waandamizi, maridhiano yanahitaji kwa haraka sana ili kuimarisha umoja ndani ya chama hicho, na kunusuru migawanyiko zaidi,

Lakini nimeeleza pia athari ambazo chadema itazipata katika hatua ya uteuzi wa mgombea urais, wagombea udiwani na ubunge, kwamba zitaghubikwa na hujuma na kukomoana kwa kiwango kibaya na hatari zaidi ikiwa hawatafanya maridhiano na kuvunja makundi ya kabla ya uchaguzi wao ambayo bado yanaendeleza na kuchochea chuki na mpasuko zaid chadema,

Nimewahi pia kueleza kuhusu tabia mbaya ya kiongozi mya wa chadema ya kuomba kuchangiwa pesa mara kwa mara inavyowaibisha familia, watu wa singinda na inavyowakatisha tamaa wanachadema katika harakati zao,
na nikashauri ni muhimu uongozi mpya wa Chadema kua na mipango mikakati mbadala ya kiuchumi itakayoifanya kujitegemea kujiendesha na kuaminika zaidi kwa wanachama wake, vinginevyo itadharaulika zaidi,

hata mtoa hoja amewahi kushauri mara nyingi kwamba chadema inafaa kuelekeza nguvu na jitihada zao kwenye udiwani na ubunge, kwenye urais wanapoteza muda tu. Je huo ni ushauri mbaya?

Gentleman, je,
hayo yote ni deconstructive criticism kweli au constructive criticism?
Binafsi natamani kuona Tanzania panakuepo united and vibrant opposition, na kwahivyo I'm always positive on issues of politics and democracy 🐒
 
Hivi hili taifa limelaaniwa na nani??sisi wakulima na wafugaji tunamuelewa lisu lakini wenye wamakalili elimu za wazungu hawamuelewi.lisu anaeleweka kabisa huwezi kufanya uchaguzi tz.ni kama nyati mmoja kupita katikati ya simba 200 hawezi pona.wasimamizi wa uchaguzi wote ni makada wa CCM nchi ya kisengee.
 
Nje ya tuvifungu twa sheria, Lissu ni mweupe kabisa.. Mwambie aache kuongelea katiba, ajadili uchumi, structure ya utumishi wa umma, kilimo, pension, solution ya tatizo LA ajira, uvuvi, solution ya tatizo LA machinga, madini, ustawi wa jamii, hapo utamuona anapuyanga tu
Kwani washauri kazi yao ni nini? Samia si ameunda tume ya Ngorongoro? Unahitaji tume kuelewa Ngorongoro?
 
Lissu anasema aliletwa na Slaa. Lakini yote hayo hayajalishi. Chama cha Chadema kiliziba put na kumkubali mtu waliyemuita fisadi papa kuwa mgombea wao wa urais.
Hata sasa hivi, kwa kutumia busara zake, Kamati Kuu ya Chama inaweza kukubali kushirikiana na wakina Halima huku wakiziba put zao. Mimi huo ushetani wa wakina Halima hata siuoni. Lakini huu ni ushauri tu. CDM itafanya kile ambacho kinaona ni sahihi.

Amandla...
Ushauri wako umepuuzwa
 
Back
Top Bottom