View attachment 2882460
Nigeria kuna makabila 371 ila kuna makabila matatu maarufu
1. Hausa = Hili ndio kabila lenye watu wengi zaidi Nigeria na Afrika, Hawa wapo nyuma sana mambo ya elimu na hata huko kwao hakuna sana maendeleo miji imejaa omba omba lakini ndio walioshikilia power ya nchi kwenye siasa, Jeshini wamejazana wao na kazi za serikali nyingi wamejaa wao. Tatizo la hili kabila ni ubinafsi mtu akipata ni yeye na ukoo wake. wengi ni wasilamu na maeneo yao mengi huongozwa kwa mifumo ya kiarabu, machifu wa mikoa yao hujulikana kama Emir. picha ya mfano ipo chini
View attachment 2882467
Nigeria imewahi kufanyiwa mapinduzi mara kadhaa, mara nyingi wahusika wakiwa kabila hili ikitokea hawajampenda rais hasa asipotokea kwao japo mara ya mwisho kufanyika mapinduzi ni miaka ya 90s.
Wananufaika sana kushika power ya nchi sababu hata kama hawana elimu hizi tenda nono huwa wanapeana wao, vyeo vinono wanapeana wao, visima vingi vya mafuta ambavyo mikoa ya mbali isio yao wanamiliki wao, Ndiko anakotokea Tajiri Aliko Dangote.
2. Yoruba - Hawa wapo Kusini Magharibi, ndio wasomi zaidi kwenye taifa hilo, na kwa sasa hata raisi anatokea huko, wengi wanategemea ajira kuendesha maisha yao, elimu kwao ndio kipaumbele japo kuna tatizo kubwa sana la ajira huko Nigeria, Pia wasanii wengi kama kina Davido na wanamichezo wengi hutokea huko. ila udhaifu wao nao hawana umoja sana.
3. Igbo - Hawa licha ya kwamba kwao ni Nigeria ya Mashariki kusini, wametapakaa sehemu nyingi Nigeria hasa kwenye majiji yenye fursa za biashara kama Lagos na Abuja, Hawa ndio wengi tunawaona kwenye muvi, maisha yale ya muvi za kinaijeria yanaonyesga zaidi maisha na tamaduni za waigbo sio wanaijeria wote, muvi hizi zilifanya hata wengi kuamini Nigeria imejaa wakristo ilhali Nigeria ni nchi iliyojaa waislam.
View attachment 2882472
Walitaka wawe na nchi yao wenyewe na kukawa na vita ya jeshi la Nigeria dhidi yao mwaka 1970, Jeshi la Nigeria lilikuwa kubwa sana na lenye nguvu likawachapa, kuanzia hapo Serikali ya Nigeria ilihakikisha hawa watu hawaji kuinuka tena, hakuna maendeleo yanapelekwa huko kwao hata barabara ni changamoto, wana akili za darasani lakini hata wasome vipi suala la ajira wanatengwa sana, kwenye mambo ya siasa nako wanatengwa sana hawapewi vyeo vikubwa, jeshini nako wanachujwa sana.
View attachment 2882474
Vita vilipoisha akaunti zote za wa igbo zilifungwa na kutaifishwa, kabla ya vita waigbo ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Nigeria na wafanyabiashara wengi walikuwa waigbo, vita ilipoanza wafanyabiashara wengi waliuawa na mali zao ziliporwa, akaunti zilifungwa, baada ya vita familia nyingi walipewa noti ya pauni 20 tu na ilibidi wasafiri umbali mrefu kuzibadili ziwe pesa za Nigeria na huko bado walipata usumbufu, hii ilikuwa ni kuwakomoa.
View attachment 2882475
Lakini amini usiamini hata ushindane na samaki kuogelea kwa kumuweka kilomira nyuma bado atakupita tu, wa igbo kufikia mwaka 1990 tayari walikuwa wameshaanza kutengeneza mabilionea, hadi kufikia sasa Nigeria watu wenye pesa nyingi zaidi ni waigbo, wengi ni wamiliki wa viwanda, miji mikubwa imegeuzwa kuwa maeneo ya maduka, n.k. ni kawaida sana kukuta kijana wa Igbo mwenye miaka 35 ana utajiri wa kutisha (Ni kweli wapo wanaofanya biashara haramu lakini ni aslimia ndogo sana ya waigbo wanaofanya biashara kihalali )
View attachment 2882476
Lakini kumbuka kwamba nserikali ilikuwa na lengo la kuwamaliza kabisa wasije kuinuka tena, mafanikio yao yamekuwa ni mwiba na tofauti na ilivyotegemewa, Serikali inayoongozwa na wahausa na wayoruba kwa kiasi flani inaendeleza itikadi za kuwadidimiza, wanabomoa nyumba zao kwa notisi za siku 2 kwa visingizio vya ajabu, wanachoma masoko yao, wanabomoa maduka yao, n.k. lakini hawa jamaa bado wanadunda tu, siri yao ni ushirikianao, umoja na mshikamano.
View attachment 2882479
Wana akili za shuleni lakini wanakosa motisha ya kusoma sana kwasababu wanabaguliwa kwenye system, wengi husoma ili kumalizana tu na mambo ya shule waanza kujitafuta kivyao ama waongeze nguvu biashara za family. Ni tofauti kwa upande wa wayoruba wanapata motisha zaidi ya kusoma sababu wao angalau wanaweza kupata ajira kwenye system japo Nigeria ni nchi yenye tatizo kubwa sana la ajira na bado kuna wale wahausa wanapeana sana ajira za kiukoo bila kuwekea uzito elimu,
Haya ni matokeo ya mtihani wa taifa wa sekondari 2023, hao wote wanne wanoongoza ni waigbo
View attachment 2882509
Siri yao kubwa zaidi tofauti na wenzao ni kwamba wana umoja, wanabebana wakijua muda wowote tatizo likimtokea flani basi kesho linaweza kumkukuta mwengine na pia hawajasahau walikotoka (kila christmas wana utaratibu wa kurudi vijijini kwao), wanajua wanabaguliwa na kufanyiwa figisu hivyo inabidi waaminiane na wasaidiane sana, wana system yao imejizolea umaarudu inaitwa Igbo apprenticeship system, ni kwamba wafanyabiashara wote wa igbo wamejiwekea utaratibu wa kuchukua ndugu zao vijijini kuwaleta mjini wawafundishw biashara kisha baada ya miaka mitano hadi 10 nao wanawapa mitaji kuanzisha biashara zao, hivyo hata moja akifanyiwa figisu kuna wengine zaidi wanaendeleza mapambano na kuboresha mbinu za kibiashara.
picha hii inaonyesha mfano wa hio system, hata iwe biashara ndogo watafundishana na kushirikiana kuikuza, mtu hadi awe na kiwanda unaweza kuta alianza kutengeneza viatu kwa mikono mwenyewe ila alipoleta wenzake wa ziada ndio uzalishaji ukaongezeka, Biasahra inaendelezwa hadi kuanza kuuza viatu nje ya nchi. (Umoja ni nguvu kubwa sana)
View attachment 2882481