Wivu na chuki ya maendeleo mbaya sana: Waigbo wa Nigeria ndio kabila lenye akili na uwezo mkubwa kibiashara, wanakomolewa ila bado wanadunda

Wivu na chuki ya maendeleo mbaya sana: Waigbo wa Nigeria ndio kabila lenye akili na uwezo mkubwa kibiashara, wanakomolewa ila bado wanadunda

Mkuu labda kama unahisi nimesema Hausa huko kwao hakuna maendeleo ngoja nikuthibitishie.

Sokoto na Jigawa ipo wa wa Hausa,

Bayelso ipo Kusini lakini kusini imegawanyika mara tatu yani kusini magharibi kwa wayoruba, kusini Mashariki kwa waigbo na kusini kusini ambako kuna Bayelso,

View attachment 2882522

Sehemu inayoongoza kwa omba omba wengi ni Nigeria ya Kaskazini Magahribi kwa wahausa
Ombaomba ni kwa sababu ya kuwa wengi zaidi .
.Nigeria kwa tajiri mkubwa ni Dangote ila ukienda kwa uwiano matajiri wa kati wengi ni igbo ...
 
Ndio hao kuna article kibao zipo mtandaoni zinaeleza wanajisafisha.
..Aliko dangote anawaburuza maisha yao yote😆😆Aliko ni Hausa....Hao utajiri wao wengi ni wezi kama Hushpup
Hapa nimekusoma 😂😂😂
 
hayo makabila yote matatu yana watu wengi sana, hakuna lenye idadi chini ya watu milioni 30 (nusu ya watanzania wote).

Hausa hawajali elimu na hawana umoja, wapo kiukoo zaidi.

Usiwe mbishi kijana kuwa na taarifa ,mimi jipo nairalanda miaka ...Hujui chochote

Kabila maskini kabisa ni Ezza tribe ambao ni jamii ndogo ndani ya Igbo...Saaa onyesha wapi Hausa ni Maskini ..

Hausa wanaishi maisha ya jamii ya kati sio kibapari...Igbo wanaishi kama hauna kitu hauna thamani .
Screenshot_20240125-165749.png
 
..Aliko dangote anawaburuza maisha yao yote😆😆Aliko ni Hausa....Hao utajiri wao wengi ni wezi kama Hushpup
Kitu cha kwanza kabisa Hush Puppy alikuwa myoruba, kilichomkamatisha wayoruba wanapenda sana ku show off, jamaa anaiba pesa ila anaishi maisha ya kutumbuliwa macho na kila mtu akaingia rada ya FBI.

Ni kweli Aliko Dangote ndiye tajiri ila kumbuka wahausa wamewekewa grisi, tenda kubwa wanapewa wao, power ya nchi kwa kiasi kikubwa ipo kwao,

Huwezi kumweka class moja na waigbo wanaopambana kila kukicha na serikali yao na bado wanapasua
 
View attachment 2882460

Nigeria kuna makabila 371 ila kuna makabila matatu maarufu

1. Hausa = Hili ndio kabila lenye watu wengi zaidi Nigeria na Afrika, Hawa wapo nyuma sana mambo ya elimu na hata huko kwao hakuna sana maendeleo miji imejaa omba omba lakini ndio walioshikilia power ya nchi kwenye siasa, Jeshini wamejazana wao na kazi za serikali nyingi wamejaa wao. Tatizo la hili kabila ni ubinafsi mtu akipata ni yeye na ukoo wake. wengi ni wasilamu na maeneo yao mengi huongozwa kwa mifumo ya kiarabu, machifu wa mikoa yao hujulikana kama Emir. picha ya mfano ipo chini

View attachment 2882467

Nigeria imewahi kufanyiwa mapinduzi mara kadhaa, mara nyingi wahusika wakiwa kabila hili ikitokea hawajampenda rais hasa asipotokea kwao japo mara ya mwisho kufanyika mapinduzi ni miaka ya 90s.

Wananufaika sana kushika power ya nchi sababu hata kama hawana elimu hizi tenda nono huwa wanapeana wao, vyeo vinono wanapeana wao, visima vingi vya mafuta ambavyo mikoa ya mbali isio yao wanamiliki wao, Ndiko anakotokea Tajiri Aliko Dangote.

2. Yoruba - Hawa wapo Kusini Magharibi, ndio wasomi zaidi kwenye taifa hilo, na kwa sasa hata raisi anatokea huko, wengi wanategemea ajira kuendesha maisha yao, elimu kwao ndio kipaumbele japo kuna tatizo kubwa sana la ajira huko Nigeria, Pia wasanii wengi kama kina Davido na wanamichezo wengi hutokea huko. ila udhaifu wao nao hawana umoja sana.

3. Igbo - Hawa licha ya kwamba kwao ni Nigeria ya Mashariki kusini, wametapakaa sehemu nyingi Nigeria hasa kwenye majiji yenye fursa za biashara kama Lagos na Abuja, Hawa ndio wengi tunawaona kwenye muvi, maisha yale ya muvi za kinaijeria yanaonyesga zaidi maisha na tamaduni za waigbo sio wanaijeria wote, muvi hizi zilifanya hata wengi kuamini Nigeria imejaa wakristo ilhali Nigeria ni nchi iliyojaa waislam.

View attachment 2882472

Walitaka wawe na nchi yao wenyewe na kukawa na vita ya jeshi la Nigeria dhidi yao mwaka 1970, Jeshi la Nigeria lilikuwa kubwa sana na lenye nguvu likawachapa, kuanzia hapo Serikali ya Nigeria ilihakikisha hawa watu hawaji kuinuka tena, hakuna maendeleo yanapelekwa huko kwao hata barabara ni changamoto, wana akili za darasani lakini hata wasome vipi suala la ajira wanatengwa sana, kwenye mambo ya siasa nako wanatengwa sana hawapewi vyeo vikubwa, jeshini nako wanachujwa sana.

View attachment 2882474

Vita vilipoisha akaunti zote za wa igbo zilifungwa na kutaifishwa, kabla ya vita waigbo ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Nigeria na wafanyabiashara wengi walikuwa waigbo, vita ilipoanza wafanyabiashara wengi waliuawa na mali zao ziliporwa, akaunti zilifungwa, baada ya vita familia nyingi walipewa noti ya pauni 20 tu na ilibidi wasafiri umbali mrefu kuzibadili ziwe pesa za Nigeria na huko bado walipata usumbufu, hii ilikuwa ni kuwakomoa.

View attachment 2882475

Lakini amini usiamini hata ushindane na samaki kuogelea kwa kumuweka kilomira nyuma bado atakupita tu, wa igbo kufikia mwaka 1990 tayari walikuwa wameshaanza kutengeneza mabilionea, hadi kufikia sasa Nigeria watu wenye pesa nyingi zaidi ni waigbo, wengi ni wamiliki wa viwanda, miji mikubwa imegeuzwa kuwa maeneo ya maduka, n.k. ni kawaida sana kukuta kijana wa Igbo mwenye miaka 35 ana utajiri wa kutisha (Ni kweli wapo wanaofanya biashara haramu lakini ni aslimia ndogo sana ya waigbo wanaofanya biashara kihalali )

View attachment 2882476

Lakini kumbuka kwamba nserikali ilikuwa na lengo la kuwamaliza kabisa wasije kuinuka tena, mafanikio yao yamekuwa ni mwiba na tofauti na ilivyotegemewa, Serikali inayoongozwa na wahausa na wayoruba kwa kiasi flani inaendeleza itikadi za kuwadidimiza, wanabomoa nyumba zao kwa notisi za siku 2 kwa visingizio vya ajabu, wanachoma masoko yao, wanabomoa maduka yao, n.k. lakini hawa jamaa bado wanadunda tu, siri yao ni ushirikianao, umoja na mshikamano.

View attachment 2882479

Wana akili za shuleni lakini wanakosa motisha ya kusoma sana kwasababu wanabaguliwa kwenye system, wengi husoma ili kumalizana tu na mambo ya shule waanza kujitafuta kivyao ama waongeze nguvu biashara za family. Ni tofauti kwa upande wa wayoruba wanapata motisha zaidi ya kusoma sababu wao angalau wanaweza kupata ajira kwenye system japo Nigeria ni nchi yenye tatizo kubwa sana la ajira na bado kuna wale wahausa wanapeana sana ajira za kiukoo bila kuwekea uzito elimu,

Haya ni matokeo ya mtihani wa taifa wa sekondari 2023, hao wote wanne wanoongoza ni waigbo

View attachment 2882509

Siri yao kubwa zaidi tofauti na wenzao ni kwamba wana umoja, wanabebana wakijua muda wowote tatizo likimtokea flani basi kesho linaweza kumkukuta mwengine na pia hawajasahau walikotoka (kila christmas wana utaratibu wa kurudi vijijini kwao), wanajua wanabaguliwa na kufanyiwa figisu hivyo inabidi waaminiane na wasaidiane sana, wana system yao imejizolea umaarudu inaitwa Igbo apprenticeship system, ni kwamba wafanyabiashara wote wa igbo wamejiwekea utaratibu wa kuchukua ndugu zao vijijini kuwaleta mjini wawafundishw biashara kisha baada ya miaka mitano hadi 10 nao wanawapa mitaji kuanzisha biashara zao, hivyo hata moja akifanyiwa figisu kuna wengine zaidi wanaendeleza mapambano na kuboresha mbinu za kibiashara.

picha hii inaonyesha mfano wa hio system, hata iwe biashara ndogo watafundishana na kushirikiana kuikuza, mtu hadi awe na kiwanda unaweza kuta alianza kutengeneza viatu kwa mikono mwenyewe ila alipoleta wenzake wa ziada ndio uzalishaji ukaongezeka, Biasahra inaendelezwa hadi kuanza kuuza viatu nje ya nchi. (Umoja ni nguvu kubwa sana)

View attachment 2882481
Kwa hiyo Igbo ni kama Wakinga wa Tzn si ndio?
 
Usiwe mbishi kijana kuwa na taarifa ,mimi jipo nairalanda miaka ...Hujui chochote

Kabila maskini kabisa ni Ezza tribe ambao ni jamii ndogo ndani ya Igbo...Saaa onyesha wapi Hausa ni Maskini ..

Hausa wanaishi maisha ya jamii ya kati sio kibapari...Igbo wanaishi kama hauna kitu hauna thamani .
View attachment 2882537
Hayo uliyoweka ni makabila madogo sana mkuu, hayana nguvu, makabila makubwa Nigeria ni matatu na kabila dogo kati ya hayo matatu ni waigbo ambao ni nusu ya idadi ya watanzania.

Cheki hayo matatu
 
Kitu cha kwanza kabisa Hush Puppy alikuwa myoruba, kilichomkamatisha wayoruba wanapenda sana ku show off, jamaa anaiba pesa ila anaishi maisha ya kutumbuliwa macho na kila mtu akaingia rada ya FBI.

Ni kweli Aliko Dangote ndiye tajiri ila kumbuka wahausa wamewekewa grisi, tenda kubwa wanapewa wao, power ya nchi kwa kiasi kikubwa ipo kwao,

Huwezi kumweka class moja na waigbo wanaopambana kila kukicha na serikali yao na bado wanapasua
Yorub ndio nembo ya kijeria kweny entertainment zote ... Wakina Dvido ,wizkid ,Burnaboy
 
Hayo uliyoweka ni makabila madogo sana mkuu, hayana nguvu, makabila makubwa Nigeria ni matatu na kabila dogo kati ya hayo matatu ni waigbo ambao ni nusu ya idadi ya watanzania.

Cheki hayo matatu
😆😆😆Hiyo ndio state maskini ni sehemu ya igbo.

Huwezi kuongelea Nijeria kimataifa bila ya yoruba na Hausa..
 
Kwa hiyo Igbo ni kama Wakinga wa Tzn si ndio?
Mkuu hao waigbo sioni hata wakikuyu wa Kenya wakiwafikia hata theluthi.

Wakinga pamoja na kuishi nchi ya amani wameanza kujipata "kibongobongo" miaka ya 2000, na hadi sasa bado hawajawafikia wachaga ambao wanakimbiza "kibongobongo",

Hebu wewe paangalie tu hapa Makete wanakotokea wakinga, Nchi ina amani hii ila wameshindwa kujenga kwao,

1706194318646.png
 
Mkuu hao waigbo sioni hata wakikuyu wa Kenya wakiwafikia hata theluthi.

Wakinga pamoja na kuishi nchi ya amani wameanza kujipata "kibongobongo" miaka ya 2000, napo bado hadi sasa hawajafikia wachaga ambao wanakimbiza "kibongobongo"
Mchaga anamkimbiza nani Bongo hii?

Wachaga wanamiliki Mikoa mingapi hapa Tzn?
 
😆😆😆Hiyo ndio state maskini ni sehemu ya igbo.

Huwezi kuongelea Nijeria kimataifa bila ya yoruba na Hausa..
Maeneo wanayotokea waigbo hayana maendeleo sababu serikali haipeleki maendeleo (wanakomolewa kwa bita ya 1970) lakini bado watu wake wana maendeleo sababu ni jamii ya biashara na pesa wanazotafuta huko kwenye majiji makubwa zinarudi vijijini kutunza ndugu zao wasilale njaa, kujenga shule, kujenga hospitali, n.k.

Wahausa wamejenga mabarabara huko kwao lakini maendeleo ya mtu moja moja bado yapo chini sana, upigaji upo juu sana, omba omba kibao wapo zaidi miji ya wahausa.

Hii ni chat gpt imeweka wazi nigeria ya kaskazini ndio inaongoza kwa umaskini

1706192450556.png
 
Sahihi mleta mada wa Igbo wafanyabishara wakubwa wa Nigeria Tanzania tukipata kumi tu Wahindi na waarabu watafunga virago

Dangote wa Dangote cement ni mu Igbo

Serikali inapotafuta wawekezaji wakubwa isiwasahau wa igbo wa Nigeria .Hawawekezi biashara vidogo vidogo kama duka la mangi au duka la mpemba

Raisi Kikwete ndie alimleta Dangote tusiangalie tu Ulaya au marekani au Asia

Africa tuna potential ya wawekezaji wakubwa wa Igbo wao ni wawekezaji biashara kubwa sio utani .

Raisi Mstaafu Kikwete ana connection ya wa Igbo kupitia Dangote Mu Igbo
 
Dangote ni Muhausa, kwake vyuma vimelegezwa katika biashara zake anateleza.

Ukiwa Muhausa Nigeria na uwe na soiriti ta buashara kuna vikwazo vichache sana, ni bidii yako tu
 
Uzi mzuri,,,,Hawa wapopo wanaongoza kuuza pisi za E,S Africa ughaibuni huko,,,hivi huko kwao kwani hakuna wanawake wazuri,,,
 
Back
Top Bottom