Wivu wa mapenzi ni janga kubwa mno, tuchague wa kumove nao sio hawa feminists! Au ma slay queen! Tiririka

MKASA WA DOKTA MELLUS TSHUBE...

Alikuwa kawaida tu.
Hakuonekana kuwa na msongo wa mawazo.
Aliendelea na shughuli zake za kila siku kama kawaida. Hata, Feb 2 mwaka huu, alipost picha akiwa na mkewe katika hali ya mahaba.

Alikuwa baba wa familia ya watoto wawili; kijana Isago Tshube (7) na binti Entle Tshube (2) na mume wa Bi. Boipelo Gala Tshube.

Tunamzungumzia Dokta Mellus Tshube.
Daktari kijana tu aliyeacha simulizi ya kusikitisha sana kwa wakazi wa jiji la Gabarone, Botswana. Jumamosi ya wiki iliyopita.

ILIKUWAJE?
Inasemwa, kulikuwa na kutokuelewana baina ya wanandoa hawa, Tshube na mkewe, mchana wa siku ya Jumamosi.

Huko kutokuelewana kukazalisha vita ya majibizano iliyoendelea mpaka jioni. Vita baina yao ilipochemka barabara na kuiva wakati huo usiku ukiwa umeshabisha hodi, Tshube alimtimua mkewe ndani ya nyumba kisha yeye akajifungia ndani na watoto wao wawili.

Akiwa huko ndani, Tshube alianza kutuma meseji kwa marafiki, familia na majirani. Meseji za kuwajulisha juu ya uamuzi wake wa kuukatiza uhai wake. Aliingia hadi Facebook akaandika majina ya watu aliowatuhumu kutembea na mkewe, akamalizia na neno I'm out! Yaani kama vile anawasusia huyo mwanamke moja kwa moja.

Huku nje, Bi. Boipelo hali ilikuwa moja haikai mbili haisimami. Alikimbilia kwa majirani kwa mayowe ya kuomba msaada akihofia mumewe anaweza kweli kufanya kitu kibaya kwake na watoto aliojifungia nao ndani, huku akituma meseji za kuigongea hodi akhera.

Wakapiga simu polisi.
Ambapo mpaka wanafika, tayari Dr. Mellus Tshube alikuwa ameshawaua watoto wake wawili na yeye kujinyonga.

Walivunja mlango wakaingia ndani. Wakakuta miili ya watoto imelala chini kama vipande vya kuni, ikiwa haina uhai tena. Mwili wa baba yao ukiwa unaning'inia darini, kwenye kile kisehemu ambacho huwa kinabaki kama kimlango cha kuingilia huko darini. Huku vipande vya kamba viwili vilivyobakia baada ya kukatwa vikiwa vinaning'inia karibu yake.

Kwamba, aliwanyonga watoto wake kwanza, walipokata roho akakata kamba alizowanyongea vikabaki vipisi juu, miili ikaenda sakafuni, akapanda yeye kujimaliza. Pasi huruma wala majuto.

Polisi wanasema, simu yake ya mwisho kupiga ilikuwa saa sita na nusu hivi usiku. Alimpigia mwanafamilia.

Basi, ikabidi Boipelo apelekwe nyumbani kwao kwa ajili ya usalama wake. Ilhali, wale waliotajwa na marehemu katika ile post ya Facebook wakitakiwa kuhojiwa ili kuisaidia polisi. - source gazeti la Botswana Guardian.

TATIZO LILIKUWA NINI HASA?

Wivu wa mapenzi?
Wanasema hivyo. Mwanamke alikuwa na watu. Alikuwa ana-flirt nao. Mwingine mpaka Dr. Tshube alikwenda kumwomba akae mbali na mkewe. Ikawa kama kumpigia mbuzi zumari. Yaani, mke wa mwenzake alikuwa kama mkewe ilhali naye ni mume wa mtu.

Hilo, lilimuuma mno Dr. Tshube. Kudharauliwa na mwanaume mwenzake waziwazi. Ilimchoma tumbo na utumbo.

Katika kusakanya taarifa zaidi. Nikagongana na habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa Dr. Tshube ambaye alishare ujumbe wa mazungumzo kati yao. Zilikuwa Meseji za marehemu juu ya hali ya ndoa yake ilivyokuwa.

Katika moja ya meseji alizotuma Dr. Tshube kwa rafiki yake enzi za uhai wake, ilikuwa ni ya malalamiko juu ya tabia ya mkewe.

Katika meseji hizo inaonekana Tshube aliwahi kufanya usaliti a.k.a ku-cheat na kukamatwa na mkewe. Lakini, akaamua kubadilika, kutulia na kujenga uaminifu ili kuimarisha familia yake. Lakini, mkewe sasa akaamua kufanya kitu kama kisasi. Hakushikika!

Yawezekana ndiyo sababu ya Dr. Tshube kujaribu kuvumilia mengi yanayoonekana kutovumilika.

Kuna sehemu aliongea kwa uchungu sana namna ambavyo anajitahidi kupambana na maisha ili kumpa mahitaji yake ikiwemo kuwa wa kisasa mitandaoni na kwenda kila tukio.

Tshube alilalamika, tatizo kubwa ni simu ya mkewe. Mara nyingi inawekwa Flight Mode akiwa nyumbani, na ikitokea simu ikaingia mkewe hawezi kuongea nayo akiwepo. Akakiri wamekwama kwenye usaliti ambao si ajabu ndiyo utakaowamaliza.

Kuna jamaa alimkamata naye, ghafla akawa haonekani simuni. Tshube alipopeleleza akagundua bibie amembadilisha jina kwenye contacts. Mke akajitetea kuwa ni rafiki tu kwa sasa hawakutani tena kimwili. Dokta akasema hadanganyiki. Akaweka kilugha chao hapo, ke lebile hela yaana. Paparazzi nikatoka kapa.

Inaonekana Tshube aliunganisha whatsapp ya mkewe na simu yake kwa hiyo akawa anajua kinachoendelea moja kwa moja. Rafikiye alimsihi aachane na kumfuatilia kwa njia hiyo, kwani itamuua ikiwa yeye Tshube alikuwa kupambana kujiponya msongo.

Tshube alisema itamfanya ashindwe kujua kinachoendelea. Akakiri kukosea na kujitahidi kujirekebisha kwa alichofanya mwanzo. Kwa kudhihirisha hilo, ameiacha simu yake wazi, jambo ambalo mkewe ameshindwa. Aliitafuta password mpaka kaipata na kuongeza password ya kidole kwenye simu ya mkewe bila mke kujua.

Alisema, anaona jitihada ndogo mno kwa mkewe kumdhihirishia kuwa anarekebisha makosa yake kama yeye alivyojitahidi kujirekebisha baada ya kukosea kwa sababu anajua anahitajika kurejesha ule uaminifu wote. Kwa namna msongo ulivyomtafuna hata Therapy aliiona kama uzushi tu. Hatari sana!

Tshube na watoto wake wamezikwa leo Tar. 4 Machi, 2023
-------------

Ni mkasa ulioacha maswali mengi.
Kwa nini Dr. Mellus Tshube aue watoto?
Amefanya hivyo ili kumwadhibu mkewe, Bi. Boipelo?
Adhabu inayoondoa maisha ya watoto wasio na hatia?
Ameishi na hii hali na msongo huu akiteseka kwa muda gani?

Kila kitu kimezama. Namna hiyo.
Kila kitu kimeenda; ndoto, furaha, mipango na kila alichokipambania.

Aliyeonekana kuwa kawaida, hakuwa kawaida.
Walioonekana kuwa na furaha , hawakuwa na furaha.
Watoto wasiohusika kwenye usaliti, wameadhibiwa pasi na kosa.

Usaliti unauma sana. Usaliti ni kitu rahisi ukitenda si ukitendewa.

Sijui mkewe ana hali gani baada ya tukio hili. Wanaume wenzake wanajisikiaje sasa?

Wanasema mkewe kama alishindwa kusamehe, asingelipa kisasi hivi.
Wanasema wanawake tulieni basi. Hapa wanasema wanapoondoa dhana kuwa mwanaume alicheat. Kuna wanawake utulivu ni sifuri.

Basi walau kama Dokta hakuona mabadiliko kama aliyoyafanya yeye baada ya kukosea, angemtaliki tu.

Wanasema... wanasema... wanasema hivyo lakini ndiyo imeshatokea.

Huu ndiyo mkasa wa Dr. Mellus Tshube.
Mbotswana aliyeua watoto wawili na kujiua sababu ya mkewe.

Laura Pettie
4 March, 2023
Baharini.View attachment 2537475
FB_IMG_16779635971960685.jpg
View attachment 2537474
 
Wanawake tulieni basi. Hapa wanasema wanapoondoa dhana kuwa mwanaume alicheat. Kuna wanawake utulivu ni sifuri.

Basi walau kama Dokta hakuona mabadiliko angemtaliki tu.
Wanasema... wanasema... wanasema hivyo lakini ndiyo imeshatokea.

Huu ndiyo mkasa wa Dr. Mellus Tshube.
Mbotswana aliyeua watoto wawili na kujiua sababu ya mkewe.

Dr.Kibabu na binti
4 March, 2023
Mdogo mdogo somo la KATAANDOA litaeleweka.
#KATAANDOA
 
Watoto wapumzike kwa amani, nmejiskia vibaya kwa ajili yao. Nadhani aliamua awamalize watoto ili kuondosha furaha kwa mkewe jumla.
Depression ni mbaya sana. Wengi wanapofikiria kujiua huwa wanafikiria pia kuhusu shida watakazozipata wale wanaowapenda siku hawapo. Hivyo kuwanusuru na hizo shida wanaona bora waondoke nao katika kifo. Ugonjwa wa akili ni mbaya sana ukikomaa kwenye kichwa kwa mtu anayeonekana yuko normal.
 
Aanzae haonekani,
Aanzae mmalize

Katika vitu hatari ni mwanamke aliyejeruhiwa kihisia, mnapotusaliti na kuchukulia poa ni vile watoto, na kuogopa jamii ila ndani fukuto lake ndo hilo, tuna visasi kama koboko, kuepusha mabaya ni kuachana tu,
Huyu kaka alianza ye usaliti usikute mke alikuwa mwema tu kwake, sasa kaamua kumywesha kile alichomnywesha yeye, wanaume mna roho nyepesi, kujihalalishia kuchepuka itawagharimu sana, hakikisha tusiujue uchepukaji wenu la sivyo mtakufa muishe
 
Mie naona majority wanaume sasa hivi kama wamechanganyikiwa vile wanalia lia wee...wachache mno wanaoweza kuwahandle wake zao wakawa kwenye mstari...na wanaisha kweli...waishi na sisi kwa akili..
 
Noma sanaa, back in the days nkiwa college nlikuaga na dem ambae nlimpenda sanaa, bc ktk pita pita za kiume nikam cheat na kitoto cha 1st yr af akajua, bana wee alinisamehe ila kisasi chake nlijutaa na mapenz yalikuja kufa kwa ugomv mkubwaa sana baada ya kugundua nae aliamua kumpa papa jamaa mwngne.

Asee skuiz mapenz sitak kbs kuyachkulia sirias.
Sasa wee ilikuuma nini demu wako kumpa mbususu jamaa mwengine?
Ulipaswa kumualika huyo jamaa mgonge threesome
 
Mie naona majority wanaume sasa hivi kama wamechanganyikiwa vile wanalia lia wee...wachache mno wanaoweza kuwahandle wake zao wakawa kwenye mstari...na wanaisha kweli...waishi na sisi kwa akili..
Mwanamke ni mvumilivu sana ila wanachukulia uvumilivu km udhaifu ndo hapo wanapofia, aaah watumie akili tu, ila tukichukia tunatisha nilishawahi kuchukia kiwango hicho sitaki tena kuwa ktk hali hiyo heri chui au simba aisee
 
Aanzae haonekani,
Aanzae mmalize

Katika vitu hatari ni mwanamke aliyejeruhiwa kihisia, mnapotusaliti na kuchukulia poa ni vile watoto, na kuogopa jamii ila ndani fukuto lake ndo hilo, tuna visasi kama koboko, kuepusha mabaya ni kuachana tu,
Huyu kaka alianza ye usaliti usikute mke alikuwa mwema tu kwake, sasa kaamua kumywesha kile alichomnywesha yeye, wanaume mna roho nyepesi, kujihalalishia kuchepuka itawagharimu sana, hakikisha tusiujue uchepukaji wenu la sivyo mtakufa muishe
Wwanaume wengine wajinga sana. Sasa mke kutombwer kweli ni kitu cha kujiua? Kwanza mke mwenye sii ajabu alimkuta tayari breki mbupuz
 
Mwanamke ni mvumilivu sana ila wanachukulia uvumilivu km udhaifu ndo hapo wanapofia, aaah watumie akili tu, ila tukichukia tunatisha nilishawahi kuchukia kiwango hicho sitaki tena kuwa ktk hali hiyo heri chui au simba aisee
😉😄😄 kama nakuona .hatari sana
 
Mwanamke ni mvumilivu sana ila wanachukulia uvumilivu km udhaifu ndo hapo wanapofia, aaah watumie akili tu, ila tukichukia tunatisha nilishawahi kuchukia kiwango hicho sitaki tena kuwa ktk hali hiyo heri chui au simba aisee
Sasa hizi fix mwezetu🤣🤣🤣🤣
 
Duh
Wanandoa mpk mmeamua kuoa/ kuolewa maana yake si mshaonja onja mkatosheka?

Si mtuliege huko ndani jamani 🥹🥹
Hiyo onja onja ndio sababu ya wanandoa kutotulia
 
Back
Top Bottom